Kuna mwengi behind pazia jamani do not just starting blaming them.
Kuna gender issues - forced sex or rape kwa wanana na waume zao. Kumbukeni katika familia nyingi habari ya uzazi wa mpango bado ni ndoto za alinacha, Mzee amerudi ana 'hitaji" we mama unakimbilia kumsomesha kalenda anaelewa? unamletea mipira anakuelewa? yeye yuko high anachotaka ni kutimiziwa- inakubamba.
Wamama tunafundwa ukiolewa huna amri na mwili wako, huruhusiwi kulala na nguo ya ndani, mzee anarudi na mbili baridi moja moto kichwani, utamwelewesha?? ukimgomea kesi!
Wengine wanaingiliwa hata wakiwa ndo wametoka kujifungua, wakilalamika kuwa wana vidonda wanaambiwa watoe mlango mwingine, wakisema wako MPs wanaambiwa kuna lango mwingine.
Above all abortion ni dhambi, imenasa unafanyaje?? Jamani tambueni kuwa wanawake wenye say ni wachache sana tena kati ya hao wanaojiita wasomi ambao kwa bahati mbaya katika hili wanaonekana hawana maadili. Nenda NBS tizama TDHS ya mwaka 2010 bado inaonyesha watu wenye watoto wengi ni wale ambao wake hawana elimu kubwa.
So kabla hujaanza kuwanyooshea vidole na kuwakaripia kwa sauti ya ukali, wape nafasi wajieleze yanayowasibu.