Ujio Mpya Wa Q-Chief / Q-Chilla naona ni balaa

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari.

Leo asubuhi na mapema nimekutana na wimbo nahisi ni mpya wa nguli wa mziki wa zamani Q-Chief au unaweza muita Q-Chilla kwenye kipindi cha 360 kupitia clouds.

Naona ni ujio mpya maana kwa zamani alikuwa na vibao vyake vingi zamani vilitamba sana.

Baadhi ya mashairi ya wimbo huu ni

I call him designer, I call him creator
You are the greatest the greatest of all
I call him designer, I call him creator
You are the greatest the greatest of all



Sijajua jina la huu wimbo ila nimeona ni kazi nzuri na kama amerudi rasmi basi nampa kongole kwa hilo

Nawasilisha.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Qchief yupo vizuri sana ila tatizo NYUNGA.
 
Apambane sana kupanda kileleni! maana soko la muziki kwa sasa limeshikiliwa na waimba matusi.
 
Madawa na kujifanya kuimba kiingereza,vinampoteza.
 
Hamna kitu hapo , ataishia kusikilizwa na watu wa age yake 40-60 , watu ambao hata kwenye shoo hawaji hata YouTube hawashindi , video itaishia kuwa na view 100k, Kuimba kama upo msibani sa hv hamna , hapo tunaassume kama kwaya tuu, wanazengo tunataka ugonge beat nzito weka mashairi konki , changamka , wala hakuna haja ya kuweka matusi , kinachobaki ni promo Tu watu tunakuelewa chap....
 
Mziki ulivyo kila mtu ana time yake,time yako ikipita kama hujafanya la maana utaishia kulalamika kila siku na kila mtu utamwona mbaya.

Hata hawa wanao tamba sasa hivi,kuna muda nao watakaa pembeni kwani siku zote maji hata yawe ya moto vipi lazima ya urudie ubaridi wake.
 
Upo sahihi mkuu. Vijana wa sahivi wanaoshinda YouTube, wanaoingia show, wanaoshinda Instagram umri wao 17-25 wengi wakati Chilla ana hit hawakua wanamjua.
 
Ilitakiwa awe amemove on kama kina Fa,Ay,prof Jay,Sugu na wakongwe wengine ila hiyo ya kusema atarudi kwenye piki kama huko nyuma its a big no...kina Ay wanafanya music for fun sasa yeye ndio biashara ataziwezea wapi hekaheka za kina Diamond kila zama na kitabu chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…