Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Inaonekana safari ya DRC kuingia EAC imeiva. Bado hatua chache tu lakini technically ni imekubaliwa.
Inasemwa kuwa lengo la Kenya kwenye EAC ni kupata soko la bidhaa zake, kuwekeza mtaji wake unaozidi na kupata ardhi. Rwanda, na labda Burundi, malengo yao ni kupata sehemu ya kupeleka watu wanaozielemea. Tz na Ug, Hazisomeki, labda zinaona ni fasheni kuwa kwenye jumuia. Pengine ndiyo maana Tz imekuwa mpinzani mkubwa wa mambo mengi ndani ya EAC.
Kwa SS, labda wanaona watakuwa salama ndani ya EAC.
Sasa ujio wa DRC unazipa nchi kama Kenya na Rwanda wanachotaka. Ardhi, fursa za kuwekeza na soko kubwa. Na Tshekedi ameacha milango wazi. Tayari kakaribisha majirani kufaidika na madini ya DRC. Pengine ile ya Tz kujidai kuwa hakuna EAC bila Tz itakufa. Nchi sita zinaweza kwenda vizuri bila sisi. Pengine labda ni wakati wa Tz kuunda mkakati wa kufaidika na EAC badala ya kuwa huko kama fasheni.
Labda niulize, Tz inafaidikaje/inapanga kufaidikaje na EAC?