Ujio wa internet explorer 9

Kilongwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
423
Reaction score
116
Hatimaye Microsoft wametoa toleo jipya la Internet Explorer, toleo hili linajumuisha mwendo kasi wa vtendea kazi vya kompyuta, msaada wa viwango vya tovuti na muonekano mpya ambao umetilia mkazo zaidi kwenye kuhakikisha website inakuwa kama system,hii ni kwa sababu siku hizi mambo mengi yanafanyika online kwa kutumia browser.

Hebu tuangalie mambo mapya yaliyomo kwenye Internet Explorer 9.


Installation


Binafsi nimeinstall Internet Explorer kwenye Windows 7,32Bit bila matatizo tena ndani ya dakika chache mekamilika Hii tumefanikisha baada ya kudownload toka MICROSOFT utapata kopi yako moja.




Baada ya kuistall tulitakiwa kureboot ili kukamilisha kazi,hii ni kwa sababu kuna baadhi ya mafaili huwa yanatumika na programu nyingine hivyo basi ni lazima urestart ili kuweza kukamilisha hatua nzimia.


Muonekano mpya, matumizi, na ubora wa kazi


Kusema kweli Internet Explorer kwa sasa ina muonekano mzuri na wa kuvutia,kitu kinaonekana kinang’aa mno. Sio tena kama ilivyokuwa kwenye ie 8,ingawa ukweli ni kuwa kuna wengi wetu bado tupo kwenye ie 6.Tunakushauri kuupgrade hadi kwenye ie 9 kwani hata AfroIT inaonekana murua kwenye ie 7 hadi 9.



Baada ya kurestart na kuiwasha kwa mara ya kwanza tunaulizwa kama tunataka kuziweka addons,binafsi nimechagua baadae ili kuhakikisha kitu kinaanza kwa mwendokasi wa haraka.



Uzuri kwenye ie 9 ni kuwa,kama kuna kitu chochote inataka kukuuliza basi hufanya hivyo kwa kutumia kijibox kilichopo chini. Hii ni bomba kulinganisha na matoleo yaliyopita,kwani kwa sasa kama kunatokea chochote ambacho browser inataka maamuzi yako basi kinaonekana kwa chini na sio kwenye ukurasa wa kusomea kama ilivyokuwa kwenye matoleo yaliyopita.


Mengineyo: Ni mengi mno ambayo yanapatikanika kwenye ie 9,hivyo kama umevutiwa basi jaribu kuinstall na uijaribu internet explorer 9 leo.
Matatizo:

Binafsi katika kompyuta moja internet explorer 9 imegoma kufanya kazi,kila nikifungua website naletewa errors na ikanilazimu kuiondoa,ila nilipoenda kwenye kwenye add and remove sikuona kitu hivyo basi nimekutayarishia Video Jinsi ya kuondoa ie 9 kwenye kompyuta.

Ona video ya jinsi ya kuondoa Internet Exploer 9

karibu kwa maoni je umeipokeaje internet explorer 9
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…