Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Ujio wa gari zinazotumia nishati ya umeme hautoathiri sekta ya gesi asilia Tanzania.
Hii inaandikwa na mimi mwenyewe.
Tanzania tuna hifadhi kubwa ya gesi asilia ila kwa bahati mbaya hatuna mafuta. Tunahifadhi ya gesi ya methane na helium.
Sasa kama tunavyo jua ujio wa gari zinazotumia nishati ya umeme zinakwenda kuua soko la biashara ya mafuta ya petroli na dizeli. Hivyo kampuni zinazofanya biashara ya mafuta duniani na Tanzania kwa ujumla zinakwenda kusimama kufanya biashara hiyo na kuhamishia mitaji katika biashara nyingine.
Lakini pia kampuni zilizowekeza katika biashara ya kutafuta na kuzalisha mafuta zitasimama kufanya kazi hiyo. Kampuni nyingi zitajikita katika kutafuta gesi asilia kwasababu gesi asilia bado itaendelea kuwa na soko.
Gesi asilia ina matumizi mengi: kupikia, viwandani, kuzalishia umeme, kuzalishia mbolea na kadhalika.
Hivyo wale wanaofanya kazi kwenye kampuni zinazo uza mafuta mwendelee kujipanga katika siku za usoni.
Na ubaya zaidi biashara ya mafuta haitegemeii soko la ndani tu. Na kibaya zaidi huko tunakotegemea kuyauza ndiko gari za umeme zinako anzia.
Unaweza kuona huo ugumu katika jambo hili.
Karibuni kwa maoni wakuu. Wewe mtazamo wako ni upi katika biashara ya mafuta. Hasa kwa Tanzania unadhani hali itakuwaje.