Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Wakuu.
Teknolojia kwenye sekta ya magari inazidi kukua kwa kasi sana.
Ni miaka 10 tu iliyopita gari likiwa na Bluetooth, reverse camera, DVD, au cruise control ilikua vitu fancy, ila sasa hivi sio vitu vya kujivunia tena.
Magari yamekua na Teknolojia kubwa sana kumpa comfort dereva na abiria.
Teknolojia inayosumbua makampuni ya magari sana hivi ni advanced driver-assistance system (ADAS).
Hii ni teknolojia inayomsaidia dereva wakati wa kuendesha gari, na ina level kuanzia ndogo kabisa Level 1 (mfano ikiwa ni cruise control ambapo gari linaongeza au kupunguza speed kama matakwa yako) hadi kubwa kabisa Level 5 (ambayo ni full autonomous, ata gari inakuja bila steering, kuiweka ni option tu)!
Kwa sasa magari yenye ADAS level ya juu yapo Level 4, ambapo gari linaweza kujiendesha kuanzia point A hadi B bila msaada wa dereva (ingawa lazima mtu awepo amekaa seat ya dereva pale).
Hii Level 4 itaperform kila kitu kuanzia kusimama kwenye zebra crossing, kwenye red light, kukwepa ajali, kutafuta parking spot, kukwepa njia iliyo kwenye matengenezo au iliofungwa etc. Inatumia geo fencing kwahiyo ni inatumika zaidi mjini na kutumia ramani (yaani mfano ww unavyotumia Google Map)!
Dereva unaweza ukalala ila gari likikuhutaji kuna alarm litapiga, likiona kimya linapark pembeni na kujizima hadi uamke.
Sawa, izo ni features tu, sasa tuje kwenye hii inayokuja hivi karibuni (huu mwaka hauishi) ambayo ni ADAS level 5.
Imeshaanza, lakini akiileta Tesla ndio itakua maarufu. Ndio maana tarehe 10 October, Tesla atakua na event pale Warner's Bros Studio Los Angeles, ambapo mbali na kutangaza magari yake mbalimbali (sana sana Tesla Model Y Juniper, Roadster 2.0 na ile Semi), pia atakuja na huduma yake mpya inayoita Cybercab (jina halijawa confirmed though).
Inasemekana gari zake zitakua hivi:
Kama ilivyoonekana juzi juzi hapa ila ikiwa full camo ili wambeya msiijue hadi tar 10.
Hii Cybercab ni Robotaxi inayokuja kwaajili ya biashara ya huduma ya ride sharing kama Bolt, Uber etc, tofauti pekee ikiwa ni kwamba hii hauitaji kua na dereva, kwahiyo unaita gari linakuja bila dereva, unapanda linakupeleka unapotaka kwenda unashuka imeisha (makato juu kwa juu kwenye kadi)!
Kwa sasa makampuni mengine yapo kwenye majaribio, mfano Waimo na Cruise wamekua wakifanya autonomous driving kitambo sana kabla ya Tesla.
Hawa Waimo kumbuka sio kampuni la magari, ila wao ni kampuni la Teknolojia kwahiyo wanaungana na makapuni ya magari mfano Mercedes Benz etc kisha wao wanatoa teknolojia.
Mfano mwingine hapa chini kampuni la Zoox wana hii gari yao ya seat nne (4).
Ingawa kana shape mbaya ila ndio ivyo, mnakaa abiria tu hamna dereva.
Okay sasa effect ni zipi?
Imagine zitakapopewa vibali (baadhi ya majimbo USA, na miji mikubwa nchi nyingine ikiwepo China na Europe wameshaipa kibali hii huduma, na magari yanaendelea kufanyiwa testing), itakua na madhara pande zote mbili, hasi na chanya.
Kwa hasi, issue ya ajira kwa madereva itakua serious sana kwasababu ni watu wengi sana wamejiajiri kupitia hizi ride sharing service kama madereva wa Uber au Bolt.
Pia, baadhi ya huduma mfano kusafirisha mizigo midogo midogo ndani ya mji kama vyakula au parcel ndogo ndogo hakutahitaji tena dereva, ni mzigo unawekwa kwenye gari unaweka address inafika mahala tajwa.
Kwa nchi zetu itachelewa kufika, ila itafika na wala sio mbali kwahiyo tujiandae kujabiliana nayo. Inaweza kuanza kutuathiri sisi madereva wa STL boss analewa gari linalojiedesha ni yeye kusave address tu: Home, Work, Mchepuko, etc chuma inampeleka.