Ujue mchezo wa Formula One

Moja ya michezo ambayo sijawahi kuielewa, ni sawa sawa uende barabarani uanze kushangilia magari yanayopita [emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuwa uende barabarani uanze kushangilia magari yanayopita[emoji848][emoji848]
 
Inasikitisha sana.wewe mwenye maelezo marefu tunaomba utueleza hapa.uliombwa kutukana
Mkuu usikatishwe tamaa. Sisi wafatiliaji wa F1 tumekuelewa na tutakuwa tunapeana updates za kinachoendelea. Ikumbukwe msimu mpya wa F1 2023 ndio huo unafunguliwa rasmi iyo march 5 huko Bahrain
 
Sioni tofauti mkuu [emoji16]
Ni mchezo tu kama mingine. Kuna jumla ya timu kumi zinazoshiriki kushindania Ubingwa. Kila timu inakuwa na madereva wawili na kila mmoja anakuwa na gari lake. Kwaio kwa timu hizo kumi kunakuwa na madereva 20 wanaoendesha magari 20. Kunakuwa na points na mwisho wa msimu mwenye points nyingi ndio anayekuwa bingwa.
Sema kunakuwa na ubingwa wa aina mbili, kunakuwa na ubingwa wa dereva mmoja mmoja, hapa namaanisha dereva atakayekuwa na point nyingi kuliko madereva wote 20 ndio anakuwa mshindi. Na pia ubingwa wa timu hapa namaanisha timu itakayokuwa na jumla ya point nyingi kwa madereva wake wote wawili..

Hebu fatilia ni moja ya mchezo mtamu sana. Sky sports F1 channel wanarusha live
 
Shukrani mkuu kwa ufafanuzi ila huo mchezo hapana kwakweli..
 
Ningezaliwa ulaya ningekuwa tajiri,ninavyokimbiza bajaj nikipewa hayo magari ya langalanga yangepaa
 
Sio juzijuzi mzee inafika hata miaka saba tangu apate hiyo ajali na nadhani hadi leo bado yupo kitandani..

Umenikumbusha mbali sana nilikuwa na skafu yangu nzuri sana miaka ile ya 2012 imeandikwa Schumacher niliisahau kwenye basi la Taqwa wakati naenda Uganda mwaka fulani hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…