Joshua Deus
Member
- Jul 16, 2021
- 50
- 21
Tanzania ilikumbwa na hofu ya sintofahamu kuhusiana na ugonjwa ulionekana kuwa mpya ambao, wengi hawakuwahi kuuona Wala kuusikia hali iliyopelekea maneno ya hofu wengine wakisema Sasa ni mwisho wa ulimwengu wa Sayari hii ya dunia, kwa mujibu wa mafundisho ya kidini, Hasa yakielezea dalili za siku ya mwisho,ukweli Ni kwamba ugonjwa huu si Mara yakwanza kutokea duniani,unaweza kujiuliza Nini maana ya mgunda, nini hasa chanzo Cha ugonjwa huu unambukizwa vipi na kwa namna gani unaweza kujikinga.
Binadamu anaweza kuathirika moja kwa moja kupitia maji ambayo wanyama walikunywa na kujoa humo,kugusa udongo pale alipokojoa mnyama wa namna hiyo aua chakula kilicho changanyika na mkojo wa viumbe hao walio athirika.
Kutokana na kutozingatia kanuni za Afya wengi wetu tumejikuta tukipitia nyakati za Magonjwa ya Mlipuko na yakumbukiza tikitumia gharama kubwa kwa ajiri ya matibabu,hata kupingukiwa nguvu kazi ya taifa kutokana na vifo.
Tunashuhudia Hadi Leo Karne ya 21 yapo baadhi ya makabila yanakula wanyama ambao hawajahalalishwa kwa chakula unaweza kusema Ni uroho wa nyama ambao inapelekea kupata Magonjwa ya wanyama binadamu wa kawaida
Ikiwa watu wote wata adhimia kuacha kula hovyo kila mnyama huenda baadhi ya Magonjwa ya wanyama yakaepukika.
Unaweza kuwa unaniuliza nini maana ya jina ambalo umebeba ugonjwa huu,maana yake Ni pamoja na hizi zifuatazo
Mgunda kwa tafsiri ya lugha ya Kiswahili fasaha inamaanisha shamba au konde hii ndio maana ya neno hili wengi waliniuliza kwanini umeitwa hivo ugonjwa huu hatari jina lake. Kitaalamu unaitwa Leptospirosis, ugonjwa huu huambikizwa kutokana na mkojo wa mnyama aliyeathirika, miongoni mwao ni Panya, nyani , Popo n.k
Dalili zinazoweza kuonekana kwa Mgonjwa wa Mgunda. kwa mujibu wa shirika la Afya duniani na CDC Ni pamoja na
Mlipuko ya leptospirosis au Mgunda kwa kawaida husababishwa na maji machafu, kama vile maji ya mafuriko. Maambukizi ya mtu kwa mtu ni nadra sana.
Leptospirosis au Mgunda unaweza kujiuliza unatibiwa kwa namna gani endapo umetokea mtu amepata maambukizi ya ugonjwa huu unatibiwa kwa anti bayotiksi kama doxycycline au Penicillin ambayo unatakiwa kupewa mapema ugonjwa ukiwa katika hatua ya awali.
Antibayotiksi hizi anapewa mtu ambaye tayari dalili zimejionesha wazi wazi kwa mtu ambaye bado anahtaji uangalizi na utafiti wa matabibu zaidi
Leptospirosis au Mgunda inapatikana zaidi maeneo ya kitropiki(Joto),shirika la Afya duniani (WHO) limekadiria zaidi ya watu 10 wana ambukizwa kila baada ya 100000 kila mwaka.
Watu wanaosafiri kwenda kwenye maeneo ya kitropiki nao wako hatarini kupata ugonjwa huu.
Leptospirosis au Mgunda,una athiri moja kwa moja,Moyo,Ini,na ,figo,usipotibiwa kwa haraka huenda ukasabisha kufeli kwa figo pia kuathiri Ubongo na uti wa Mgongo ukiathiri Ute Ute unauzunguka Ubongo na uti wa Mgongo. ambapo inaweza kupelekea ugonjwa wa ukichaa,usingizi ulio kithiri
Maeneo ambayo yanaweza kukumbwa na ugonjwa huu Ni ukanda wa mashariki nusu Jangwa wa Sahara, Australia, Amerika ya Kati na Carrebesn, Kusini mwa bars la Asia.
Nini chakufanya ili kuepukana na Magonjwa ya namna hii?
USAFI
Mara nyingi tumekuwa watu wa mshtukuko ambao husabishwa na Magonjwa ya namna hii tunapaswa kuamka na kukemeana sisi kwa sisi tukiyatunza mazingira,tunayo ishi na kutuzunguka,kuhakikisha tuna nawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kila baada ya kumhudumia wanyama wetu au kushika sehemu yeyote huenda isiwe salama kwa Afya yako.
KUACHA KUCHANGIA MAJI NA WANYAMA
Nchi yetu Ina majj ya kutosha lakini Cha kusikitisha Ni kwamba baadhi ya maeneo katika nchi yetu binadamu wanachangia maji na wanayama wakufuga na waporini,hili Jambo Ni hatari kwa Afya zetu,maana hatuwezi kuwa na uhakika na Hali za kiafya za wanyama hao,Seeikali inapaswa kuweka nguvu kwa maeneo ambayo hakuna maji kujenga visima vya kisasa kwa ajili ya maji kwa matumizi ya binadamu.
KUCHEMSHA MAJI NA CHAKULA
Tunapaswa kuhakikisha maji tunayokunywa na chakula tunachokula Ni salama kwa Afya zetu kuchemsha huenda kutasaidia kuua bacteria au.vijidudu ambao wanaweza kua wamebeba ugonjwa huo.
KUACHA KULA WANYAMA PORI AMBAO HAWAJA IDHINISHWA
Si kila mnyama anaruhusiwa kuliwa,wataalamu wa viumbe na wanyama pori wanatakiwa kutoa elimu juu ya wanyama Hawa kwani wakati mwingine baadhi Yao Ni hatarishi kwa Afya zetu,ikiwa tuta amua kuachana na kula nyama iliyo pimwa na miruhusiwa itasaidia kuondokana na Magonjwa haya.
KUVAA MAVAZI NA VIATU
Kwani ugonjwa huu kuambukizwa kwake hupitia Katika ngozi pia ya binadamu kuvaa viatu na nguo zizo funika sehemu kubwa ya mwili hii Ni njia moja wapo ya kujikinga na ugonjwa huu hatari wa Mgunda(Leptospirosis) tahadhari kabla ya hatari Ni Jambo la msingi maana ukisubiri upate ugonjwa ndio ujitibu au kuchukua tahadhari utakua umechelewa na itakugharimu.
Mgunda au Leptospirosis Ni ugonjwa ambao tuweza kuudhibiti kwa nguvu zetu ikiwa tutaamua kupiga Vita ugonjwa huu ambao Ni hatarishi kwa Afya na maisha ya binadamu,Linda Afya yako na ya mtu mwingine saidia kumkinga ugonjwa huu mtu mwingine, ambaye unaweza kumsaidia apukane na ugonjwa huu.

- Homa Kali
- kichwa kuuma.
- Kutokwa damu
- Maumivu ya misuli
- Kutapika na macho mekundu.
- Kuhara
- Kukohoa.
- Bakteria wanaweza kuingia mwilini kupitia ngozi au utando wa (macho, pua au mdomo), hasa ikiwa ngozi ina mikwaruzo.
- Kunywa maji machafu pia kunaweza kusababisha maambukizi.

Upvote
1