Efatha Foundation Ltd ilipomiliki eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondoka mwaka 2005, wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd. Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhamaw akafungua kesi mahakamani dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa. Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hili thamani yake ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro Plus Industries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali. Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus Industries Ltd kama ilivyodaiwa.