Ujue umuhimu wa bulks sms katika kukuza biashara yako

Ujue umuhimu wa bulks sms katika kukuza biashara yako

Joined
Jul 24, 2017
Posts
31
Reaction score
17
Bulk SMS ni huduma ya kutuma ujumbe wa SMS kwa watu wengi kwa muda mfupi.

Kwa kutumia huduma ya bulk sms unaweza kutuma idadi ya sms moja kwa watu wengi zaidi kwa wakati mmoja.
Huduma hii ufanywa kupitia mfumo maalumu tofauti na ule wa SMS za kawaida.

KWANINI SMS NI MUHIMU SIKU HIZI?
• Kuna ongezeko la matumizi ya simu
• SMS zina kiwango cha 98% cha ufunguaji kwa watumiaji wa simu
• SMS zinasomwa ndani ya dakika 3 za kwanza baada ya kupokelewa
• Ujumbe wa SMS ni dhana ya uuzaji huria na rahisi kulinganisha na TV,RADIO, MTANDAO
• SMS zinaweza kupokelewa kwenye simu yoyote ile

FAIDA /MANUFAA YA BULK SMS
1. Uwezo wa kuwafikia wateja mara moja
2. Uhakika wa kupokea malipo kwa wakati
3. Okoa muda na tumia mtandao kutuma ujumbe wa SMS
4. Husaidia kupunguza gharama kwa kununua SMS kwa bei ya jumla.
5. Ongezeko la kujulikana kwa biashara yako
6. Husaidia kukuza biashara yako kwa haraka zaidi.

SEKTA ZINAZOWEZA KUTUMIA BULK SMS
1. TAASISI ZA KIDINI NA VIKUNDI
Taasisi za kidini zinaweza kutumia sms ili kuwasiliana na watau wao na kutoa habari kama ukumbusho wa sms za malipo,mikutano,wafadhili n.k

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Huongeza kujulikana kwa bidhaa

Mfano wa taasisi za kidini ni makanisa na misikiti
Vikundi ni vikundi vya michezo, vikundi maalum

2. TAASISI ZA KIELIMU
Taasisi za elimu zinaweza kutumia SMS ili kuwasiliana na walengwa wao kwa lengo la kufanya:-
• Matangazo
• Ukumbusho. Mfano malipo na mikutano au vikao
• Taarifa mpya za kozi,usajili na uandikishaji

Taasisi za elimu ni kama shule,vyuo vikuu, vyuo, taasisi za mafunzo, vituo vya malezi, kozi za ujuzi n.k

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Hukuza huduma
• Inaokoa gharama

3. MASHUGHULI
Waandaaji wa hafla wanaweza pia kitumia SMS ili kuwasiliana na walengwa wao na kutoa habari kama
• Matangazo ya hafla
• Ukumbusho wa matukio,tarehe,ukumbusho wa ukumbi,michango

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Huongeza kujulikana kwa huduma
• Inaokoa gharama

Mifano:
Sendoff,waandaaji wa matamasha,harusi n.k

4. MAWAKALA
Mawakala wa uuzaji wanaweza kutumia SMS ili kutoa habari kwa walengwa wao kama vile:-
• Ofa
• Ukumbusho
• Tahadhari mbalimbali
• Mabadiliko mapya
• Shughuli
• Taarifa

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Huongeza kujulikana kwa huduma
• Inaokoa gharama

Mfano:
Mashirika ya uuzaji, mashirika ya ajira

5. VIWANDA VIDOGO
Waandaaji wa hafla wanaweza pia kitumia SMS ili kuwasiliana na walengwa wao na kutoa habari kama
• Ukumbusho wa malipo, maonyesho n.k

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Huongeza kujulikana kwa huduma
• Inaokoa gharama

6 WAJASILIAMALI, WAFANYA BIASHARA MBALIMBALI
Hawa wanaweza kutumia huduma ya sms ili kuwasiliana na wateja wao pamoja na kutafuta wateja wapya.
Wanaweza kutumia sms kutoa taarifa kama
• Uwepo wa bidhaa mpya sokoni
• Ukumbusho

Manufaa:
• Kuwafikia walengwa kwa haraka
• Huokoa muda
• Huongeza kujulikana kwa huduma
• Inaokoa gharama
Hii huwasaidia kuweza kuwa karibu na wateja wao na kuweza kukuza biasha yao.

Mfano: stationary, supermarket, network marketing, n.k

ZIADA
Bulk SMS zinazo tolewa huwa hazina expire date kama ilkvyo kwa sms za kawaida. Buli huexpire kwa kuisha kwake.

Ahsante

images.jpg
 
Ndiyo wale jamaa wa "ile pesa itume kwenye namba hii 07********! hutumia aina hii ya meseji au?
 
Acha kuwa na negative atitude hasa kwenye maswala ya muhimu. Kama una shaka uliza upewe maelezo

Hiyo alama ya kuuliza hujaiona, au! Nimeuliza kwa nia njema kabisa tofauti na mtazamo wako. Jibu kistaarabu tu. Au lengo la hii mada yako ni nini?

Sijamaanisha ya kwamba wewe ni tapeli! Nimeuliza tu kujua iwapo na wale matapeli hutumia aina hiyo ya sms kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja au wanatumia mfumo mwingine. Wewe ni mtaalamu, nifafanulie tu.
 
Nimeiona. Ila uliza yako ni ya kejeli
 
Gharama yake ni sh ngapi mkuu?/packages?

Mnaweza tuma msg kwa watumiaji wa mkoa mmoja tu?

Mnashirikiana vipi na mitandao ya simu?

Nawezaje kukuamini kuwa kweli msg zinawafikia walengwa?
 
Gharama yake ni sh ngapi mkuu?/packages?

Mnaweza tuma msg kwa watumiaji wa mkoa mmoja tu?

Mnashirikiana vipi na mitandao ya simu?

Nawezaje kukuamini kuwa kweli msg zinawafikia walengwa?
Kwa maelezo zaidi piga simu au tucheki whatsapp kwa hiyo namba hapo.
 
Hapo ndo wafanyabiashara mnapokwama
Umeamua kujitangaza shida iko wapi ukitoa taarifa zaidi hapa pia?

Mf walau wateja tujue packages zikoje
Na km mahitaji yangu naweza yapata kwenu
Ndio maana kumewekwa mawasiliano ndugu. Siwezi jibu kila kitu hapa. So kama upo serious use that Number.
 
Aki-panic tu jua ni yeye
Hiyo alama ya kuuliza hujaiona, au! Nimeuliza kwa nia njema kabisa tofauti na mtazamo wako. Jibu kistaarabu tu. Au lengo la hii mada yako ni nini?

Sijamaanisha ya kwamba wewe ni tapeli! Nimeuliza tu kujua iwapo na wale matapeli hutumia aina hiyo ya sms kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja au wanatumia mfumo mwingine. Wewe ni mtaalamu, nifafanulie tu.
 
Anataka kusanya contacts za watu ndio maana anagoma kujibu maswali kwenye jukwaa
 
Hiyo alama ya kuuliza hujaiona, au! Nimeuliza kwa nia njema kabisa tofauti na mtazamo wako. Jibu kistaarabu tu. Au lengo la hii mada yako ni nini?

Sijamaanisha ya kwamba wewe ni tapeli! Nimeuliza tu kujua iwapo na wale matapeli hutumia aina hiyo ya sms kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja au wanatumia mfumo mwingine. Wewe ni mtaalamu, nifafanulie tu.
Ni ajabu sana mtu ana huduma ya kusaidia process nzima ya 'sales' lakini yeye mwenyewe hana sales skills & ethics, mfano emotional intelligence
 
Gharama yake ni sh ngapi mkuu?/packages?

Mnaweza tuma msg kwa watumiaji wa mkoa mmoja tu?

Mnashirikiana vipi na mitandao ya simu?

Nawezaje kukuamini kuwa kweli msg zinawafikia walengwa?
"Sina lengo la kumuharibia biashara"..

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, Hii haina tofauti sana na ile ya kutuma emails.
Wanaenda kununua bulk sms (kama vifurushi) kwa makampuni ya simu na wanakuwa na namba za watu wengi kwenye database yao. Then wanachofanya ni kutuma tu

kuhusu impact kwa biashara yako, labda utume nyingi sana (thousands) na ufanye mara kwa mara.

NB
Njia bora japo siijui biashara yako ni kuwa na daftari maalumu la kuweka record ya kila mteja anaeingia dukani/ biasharani kwako (uwe unaingiza katika electrical way kama excel pia kwa ajili ya record nzuri).

Hao ndio wateja wa uhakika so, nenda kwenye mitandao ya simu kama voda au tigo then wakupe hiyo huduma.
Utatuma kwa wateja wako kuhusu huduma au mzigo mpya.

Hii ndo best way kwa upande wangu
 
Gharama yake ni sh ngapi mkuu?/packages?

Mnaweza tuma msg kwa watumiaji wa mkoa mmoja tu?

Mnashirikiana vipi na mitandao ya simu?

Nawezaje kukuamini kuwa kweli msg zinawafikia walengwa?

Tigo wana hii huduma inaanzia kiasi cha sh elfu 50 mpk kuendelea kulingna na coverage yako.

Yani iko hivi wanakupa code ya sms yako mfano 15529 code hii unawapa dizain ya tangazo lako mfano kwa wafanya biashara ujumbe unabeba product, price, location na Contact zako then kulingana na pesa yako wanakupa coverage inayokua kwa mfumo maalumu labda ujumbe utafikia watumiaji wa mtandao wa tigo tu waliopo maeneo ya Salenda bridge, makumbusho, mwenge, sinza , magomeni tu
 
Back
Top Bottom