Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam Wakuu,
Kusasisha simu ni hali ya kukubali/ kuruhusu mabadiliko ya mfumo wa simu au App iliyo katika simu au kifaa cha kijidijalikwenda katika mfumo mpya. Mabadiliko haya yanaweza kufanyika kwenye vifaa vingine vya kidijitali iliwamo Computer Smart TV na android TV. Mada hii itajikita kufafanua umuhimu wa kufanya Updates kwa upande wa simu za mkononi.
Kuna updates za aina mbili kwenye simu
- Masasisho ya kiusalama (security updates)
- Sasisho kutoka toleo moja kwenda lingine (updates from one version to another).
2. Masasisho ya matoleo huhusisha mabadiliko kutoka katika mfumo fulani wa uendeshaji wa simu kwenda mfumo mwingine. Mfano, kutoka Android 8 kwenda 8.1. Updates hizi hizi hukuongezea features kwenye simu na kubadili muonekano.
Umuhimu wa kufanya Updates kwenye simu yako
- Husaidia kuifanya simu yako kuwa salama na ngumu kushambuliwa na virusi mbalimbali.
- Husaidia kupata mambo mapya yaliyoongezwa kwenye simu au App fulani ukitazama Change log utabaini mambo mapya yaliyoongezeka.
- Kutatua matatizo yaliyopo kwenye mfumo wa simu (Oparating System) iliyopo mfano ulaji wa chaji, matatizo kwenye kamera na mengine.
- Kuweza kutumia au ku-access ya baadhi ya Apps. Kuna baadh ya Apps huwez install kwenye OS za chini lazima uwe na OS mpya.
Namna ya Kusasisha (Update) simu yako
- Kwanza hakikisha simu yako imeunganishwa na mtandao (Intaneti) kwa kutumia data binafsi au Wi-fi
- Fungua Play Store ama App Store.
- Gusa upande wa kulia juu sehem ya kuweka picha kwenye account yako.
- Gusa sehem iliyoandikwa Manage App and Device
- Gusa sehem iliyoandikwa see details Ili kuona App zinazohitani kusasishwa
- Gusa sehem iliyoandikwa Update all, hapo utakuwa umeupdate Apps zote za kwenye simu yako au la unaweza kugusa App Moja Moja ikiwa hutaki kusasisha zote kwa mkupuo.
Note: Unapogusa hiyo App utaona ishara kuwa inaanza kupakua. Ikimaliza utaona inaondoka kwenye orodha za Apps zinazohitaji kusasisha. Kumbuka ufafanuzi huu umejikita kwa simu za mfumo wa Android
Kwa kufanya mchakato huu utakuwa tayari umeupdate Apps zako. Kuna baadhi ya simu hukupa taarifa iwapo OS au kuna Updates kwenye App fulani.