Ujue Wasifu wa Hayati Kenneth Kaunda wa Zambia

Ujue Wasifu wa Hayati Kenneth Kaunda wa Zambia

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
MFAHAMU HAYATI KENNETH KAUNDA(KK).

Na Elius Ndabila
0768239284

Taarifa iliyoripitiwa hivi leo na vyombo vya ndani vya Zambia ni kuwa Rais wa Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth KAUNDA ambaye kule wanapenda kumwita Baba wa Taifa ameaga Dunia.Mzee Kaunda ni pekee yake kati ya Wazee wa Mwanzo waasisi wa Uhuru barani Afrika aliyekuwa bado hai.

Mzee Kaunda ana historia ndefu na ya kuvutia, leo nitajaribu kukupa historia yake fupi huyu moja ya miamba ya Afrika aliyefariki Leo akiwa na miaka 97 na miezi karibia 2.

Wapo wanaosema Mzee Kaunda ni mtu wa Malawi ambaye alienda kusaidia Zambia kupata Uhuru.Leo nitakujuza kudogo na kukupa majibu juu ya utata huu ambao watu wengi wanao.

Kabla sijamzunguzia Hayati Kaunda, ninaomba nijibu kwanza hoja ya utata wa mahusiano ya Kaunda na Malawi na kwa nini Kaunda alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Rais wa Kwanza wa Malawi Mzee Banda? Jibu la hili ni kuwa Baba yake Kenneth KAUNDA alikuwa ni mzaliwa wa Malawi. Baba yake Kenneth KAUNDA Mzee David Kaunda na Mama yake Kenneth KAUNDA walikuwa ni Walimu. Walichukuliwa kwendq kufundisha Nothern Rhodesia/Zambia kutoka Nyasalanda/Malawi. Wakiwa huko ndipo walibahatika kumzaa Kenneth KAUNDA Kama sehemu ya watoto wao nane. Hivyo Kaunda ni Mzambia kwa kuzaliwa lakini akiwa na asili ya Malawi.Ninadhani hapo tumeelewana. Mama yake alikuwa ni mwanamke wa Kwanza Afrika kufundisha katika shule za kikoloni.

Tumtazame sasa Kenneth KAUNDA.

Ukisoma maandiko mbalimbali ya Zambia Hayati Kaunda hajaandikwa sana. Hivyo ninaweza kusema ni mtu ambaye pamoja na umaarufu wake mkubwa lakini hajawekwa sana kwenye kumbukumbu za kwenye maandishi. Kidigo kwenye mtandao wa Britannic.com wamejaribu kumuelezea kinagaubaga.

Keneth Kaunda alizaliwa 24/4/1924 katika Kijiji Cha Lubwa ambacho kipo karibu na mji wa Chinsali Kaskazini mwa Zambia.

KK alisoma shule ya msingi katika shule waliyokuwa wakifundisha wazazi wake. Alihitimu masomo ya sekondari mwaka 1940. Kama ilivyo kwa Waafrika wengine ambao walau walikuwa wamepata elimu ya kati, Kaunda naye alienda kuwa Mwalimu. Aliwahi kufundisha Zambia na Tanganyika/Tanzania katika ya miaka ya 1940.

Mwaka 1949 Kaunda alirejea Zambia na akawa Mkalimani na mshauri wa Sir Stewart Gere-Browne a leberal white Settler ambaye pia alikuwa Mbunge. Huko Kaunda alijifunza vitu vingi ikiwepo siasa.

Mwaka 1950 Kaunda alijiunga na chama Cha ANC's na baadaye akawa katibu mkuu(Mtendaji mkuu). Nafasi hii ilimuongezea exposure na akawa maarufu sana. Hata 1958_59 ANC ilipoanza malengo ya kudai Uhuru Kaunda ndiye alipewa majukumu makubwa ya kutengeneza program.

Baadaye alikuja kuwa kiongozi mkuu wa taasisi hiyo na kuanza kufoji baadhi ya nyalaka za kizungu katika makoloni ya Uingereza hasa Zambia, Malawi na Zimbabwe. Alijitahidi kuwashawishi wananchi kupigania Uhuru lakini wengi wakawa waoga. Akaanzisha kitu kilichoitwa "Positive nonviolent action" ambacho kilihusika na raia kutokutii maagizo ya sera za ukolini. Matokeo haya hili yalikuwa mawili ambapo mojawapo alikamatwa yeye na wenzake na kwenda jera. Hii iliwapa ushujaa na kipindi hicho afrika nzima ilikuwa kwenye mapambano ya kudai Uhuru.

January 1960 aliruhusiwa kutoka magereza na akachaguliwa kuwa Rais wa UNDP( UNITED NATIONAL INDEPENDENCE PARTY) ambacho kilizaliwa mwaka 1959 ba Mainza Chona.

Mwaka 1960 mwishoni Uingereza ilimualika kuhutubia baraza Hilo Londan kueleza kwa nini anataka Uhuru?

Uchaguzi ulipofanyika 1962 chama chake kilishinda. Na mwaka 1964 ikapata Uhuru kamili Kaunda akiwa Rais.

Kama yalivyomaeneo mengine, baada ya Zambia kupata Uhuru vilizuka Vita vya ukabila, hasa ukizingatia Kaunda alikuwa na asili ya Malawi. Na uchaguzi ulipofanyika mwaka 1968 Kaunda alishinda. Alipoona mbele haoni kuendelea kuwa Rais hasa ukizingatia Vita ya ukabila na Utaifa, mwaka 1972 alifutilia mbali mfumo wa vyama vingi na mwaka 1973 akatengeneza katiba.

Mwaka 1970 Zambia ikuwa black nationalistic guerrillas led by Joshua Nkomo( Nitaandika next time).

Mwaka 1990 Kaunda aliruhusu Mfumo wa vyama vingi na mwaka 1991 Kaunda na Chama chake Cha UNIP walushindwa vibaya kwenye uchaguzi na Chama Cha Movement Multiparty Democracy (MMD) ilishinda kwa ushindi wa kishindo(landslide) na Fredrick Chiluba kuwa Rais.

Kaunda amefariki akiwa na miaka 97.

RIP Kaunda.

Zaidi, soma:

1). News Alert: - Kenneth Kaunda afariki dunia akiwa na miaka 97
 
Mkuu tupe wewe madini sahihi ili tuelimike, maana huyu ni mmoja miamba ya Africa.
Hii makala niliandika miezi michache iliyopita Mzee Kaunda alipofikisha miaka 97:

KENNETH DAVID KAUNDA NA ALLY KLEIST 1953

Leo Kenneth Kaunda katimiza miaka 97.

Nimeangalia picha ya Kenneth David Kaunda na picha hii ikanikumbusha uhusiano wa Kaunda na Ally Kleist Sykes wakati Afrika ilipokuwa katika harakati ya kupigania uhuru wake.

Usiku umekuwa mwingi In Shaa Allah kesho nitaeleza vipi Ally Sykes na Kenneth Kaunda walifahamiana miaka ya 1950 wakati Northern Rhodesia sasa Zambia na Tanganyika zilipokuwa zinapigania uhuru wake.

Ally Sykes mzee wangu nimemvulia kofia katika kutunza kumbukumbu.

Faili la safari yake yeye na Dennis Phombeah kwenda Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Ikweta naamini ndilo faili mwenyewe akilipenda kuliko mafaili yake yote yenye taarifa za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ndani ya faili hili kuna ''cuttings'' ya magazeti zikieleza mkasa mzima wa safari yake kutokea Dar es Salaam hadi Salisbury ambako yeye na Phombeah walitiwa mbaroni na makachero wa Kikaburu kama ''Waafrika Wakorofi,'' na kufungiwa ndani ya banda nyuma ya nyumba ya Mzungu usiku kucha.

Asubuhi wakaachiwa na kuamriwa kurudi Tanganyika kama wahamiaji wasiotakiwa.

Hii ni movie ni ''block blaster,'' ambayo itahitaji waigizaji mahiri kucheza nafasi ya Ally Sykes, Denis Phombeah, Kenneth Kaunda, Harry Nkumbula, Charles Mzengele kachero, kibaraka wa Wazungu walowezi wa Southern Rhodesia, kachero kibaraka wa Waingereza Tanganyika, Alexander Thobias, Trevor Huddleston Mwingereza muungwana aliyekuwa rafiki wa Waafrika.

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa ANC na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini.

Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC.

Hapa ndipo Kaunda akaanza kuwatafuta wanasiasa wenzake waliokuwa Tanganyika, Kenya na Afrika Kusini na kuwaalika kwenye mkutano Lusaka, Northern Rhodesia ambao ungewakutanisha wapigania uhuru kutoka nchi za Afrika chini ya Ikweta.

Hivi ndivyo Kenneth Kaunda na Ally Sykes walivyokuja kufahamiana kwa kuandikiana barua ambazo Ally Sykes alizihifadhi hadi mimi kuja kuzisoma miaka mingi baadae.

Katika kusoma nyaraka kama hizi ndipo nikamwelewa Ally Sykes pale alipokuwa akiniambia, ''Hawa walioandika historia ya TANU hawana moja wanalolijua.''

Mkasa wa safari hii ya Ally Sykes na Denis Phombeah kuhudhuria mkutano wa Lusaka ni kisa kirefu sana lakini chote nimekieleza katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Nimeweka picha ya Charles Mzengele kachero kibaraka wa walowezi ikifuatiwa na picha ya Kenneth Kaunda na Harry Nkumbula kama walivyokuwa katika miaka ya 1950.

Ally Sykes alikuwa akitamka jina hili kama ''Mzengele,'' lakini usahihi wa jina la huyu kachero ni Mzingeli.
 
Aliwahi kufundisha Zambia na Tanganyika/Tanzania katika ya miaka ya 1940.
Ungetaja maeneo aliyofundisha hapa nchini kama wengine walivyoandika juu ya marais wengine kusoma Tanzania na vyuo au shule walizosoma.
 
Mkuu upo vizuri sana, vipi Harry Nkumbula alishindwa kabisa kufurukuta na kushindwa kuwa Rais wa kwanza wa Zambia maana huyu ni mzawa wa Northern Rhodesia.
 
IMG-20210617-WA0240.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi alitaka kuleta longolongo, lakini kama si busara ya Hayati mwalimu Nyerere katika kutatua hizo longolongo zake tungemsahau siku nyingi. Mwalimu aliwaweka sawa na wapinzani ambao ulishinda uchaguzi na kwa pamoja walikubaliana awe Baba Taifa.
Aliongoza kwa haki thus ameishimiakamin
 
WEWE MUONGO Joshua Nkomo hana unasaba na harakati zozote za Zambia.

Joshua Nkomo ni Mzimbabwe ambaye alikuwa katika harakati za kudai uhuru na akina MUGABE ROBERT, BISHOP ABEL MUZOLEWA .

Kwa kumtaja MZIMBABWE joshua Nkomo kuwa Mzambia ni ushahidi kuwa ulichoandika chote ni UONGO TUPU.
 
Back
Top Bottom