Ujumbe kwa wanandoa watarajiwa!



...kuna ule msemo watu wanasema huyu uliyemuoa wala sio type yako,....
hebu mtu mzima ichambue hii, naamini ushawahi isikia...!

Naweza na mie nikajaribu kujibu? Pleaaaaase. . . .!!

Nwy acha nijibu tu.

Wanaweza wakawa sahihi kwa maoni yao kwasababu wanaona zile tofauti. Wapo watu wanaotofautiana sana lakini tofauti zao ndio zikawafanya waelewane sana. Yani tofauti za mmoja zikiwekwa na za mwenzake zinatengeneza kitu kilichokamilika.

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/164443-mimi-na-wewe.html#post2369774

Niliwahi kuanzisha mada inayosema sisi ni kama vipande vya puzzles, tulivyo, tabia zetu, muonekano, akili, fikra ndio hivyo vipande vya puzzles. Na tunapochagua wenzi tunatakiwa tuangalie ambae vipande vyetu vitaendana na vyao kutengeneza picha kamili.

Wengine, kutokana na walivyo inabidi wapate wanaofanana nao, wengine tofauti ndizo zitakazowaweka pamoja. Ukilazimisha kwa mtu unaefanana nae (kama hao walimwengu wanavyotaka) wakati kiukweli unahitaji wa tofauti ndipo matatizo huanza. Ndio maana mimi nadhani ni muhimu watu wakachagua wenyewe kuendana na mataka/mahitaji yao bila ya kujali walimwengu wanawaonaje pamoja.
 
Babu DC, asante kwa neno hili! Nimeona mtu amekuwa na BF kwa miaka 7, wanaishi mji mmoja lakini mdada hajui boifrendi anapoishi! Hii si kwa wanaume tu, hata wanawake! Kuna hajui BF anaishi wapi, anafanya kazi wapi, anafanya kazi gani, hajui marafiki zake wala ndugu zake! Kwanza inaonesha jinsi usivyomjali mwenzio!
 

Duh!!
Watu wanakutana kimjini mjini, wanamalizana kimjini mjini na kuagana kimjini mjini. Sasa huyo dada ni kwamba hajawahi kuuliza ama? Mimi hata rafiki ambae sijui anapoishi na hajawahi kunialika kwake(si lazima niende) siwezi kumwita rafiki wa karibu.
 


...kuna ule msemo watu wanasema huyu uliyemuoa wala sio type yako,....
hebu mtu mzima ichambue hii, naamini ushawahi isikia...!

Hiyo ni haki yao kwa sababu kila mtu yuko entitled kuwa na opions zake bila kuomba ruhusa ya mtu mwingine. Ila mhusika mwenyewe ndiye anayejua kwa nini ameamua kuwa na mwenzi wake aliyenaye....Hata hivyo kuna watu ama wanajikuta wametumbukia kwenye mahusiano kwa sababu ambazo hazikizi vigezo vyao vya msingi au pressure ya wanajamii na ndugu...Hilo kwa maoni yangu ni hatari kuliko ukoma!!

Ni vizuri mtu mwenyewe ajichagulie ili aweze kubeba dhamana ya matokeo ya uamuzi wake!! Na katika kufikia azma hii anaweza kusikiliza au kutosikilza maoni na ushauri wa mtu mwingine yeyote!! Na ingekuwa vizuri jamii ikapunguza tabia ya kuingilia mambo ya ndoa za wenzao!
 
Reactions: Mbu


Safi sana Lizzy,

Ndiyo maana juzi nilisema kwamba tayari wewe umehitimu...Tunasubiri kukupa cheti na kuona praktiko!!

Mungu atembee na wewe popote unapoenda,

Ni dua za,

Babu DC (1947)!!
 

Hii ni irresponsibility ya hali ya juu kabisa...

Hivi ukijikuta unadate serial killer aliyejaza vichwa vya watu kwenye freezer nyumbani utamlilia nani?

Kwanza vijana watambue kuwa mtu anayekupenda kweli atataka kukufahamu in and out na wewe pia kama unapenda uta-respond positively!!

Mtu wa namna hiyo anahitaji ama kucharazwa bakora au kupigiwa maombi ya mwezi mzima....He/she is a loser!!


Mtu anayekuficha mambo yake ya msingi anawezaje kuwa rafiki??

Inabidi watu wajitahidi kufikiria kwa kutumia vichwa vyao halisi!!
 
Babu DC ujumbe mzuri sana huu naamini utawafaa na kuwaongoza sana wanandoa watarajiwa
 
Ujumbe ni mzuri sana babu DC.
mm binafsi nimechukua ki2 hapa.
asante sana dark city.
 
no 7 maximum iwe three month
 
Hiyo point kwamba usimhurumie mtu mpige chini tu ni muhimu sana kuizingatia hahaha ahsante kama binti huna mpango nae usikae nae sana lala mbele fasta.
 
Babu DC ujumbe mzuri sana huu naamini utawafaa na kuwaongoza sana wanandoa watarajiwa


Hahahahahahah,

Hujambo dogo? Heri ya mwaka mpya!!

Wewe ni wa pili after Lizzy, kuwapasia wengine mpira badala ya kuucheza!!

Vyovyote vile, naamini umeambulia kitu cha kukufaa kama silaha muhimu mbele ya safari inayokukabili!!

Usisahau kula na wenzio akina Hus!!

Babu DC!!
 
Asante sana Babu huu uzi utakuwa na manufaa sana kwangu...
 
Ujumbe ni mzuri sana babu DC.
mm binafsi nimechukua ki2 hapa.
asante sana dark city.

Poa ndugu yangu,

Hebu basi na wewe ongezea kidogo ili wenzio wafaidi uzoefu wako.

Kwa mfano, unalionaje suala la kutegesheana mimba ili kulazimisha ndoa??

Babu DC!!
 
no 7 maximum iwe three month

Poa tu kama wadau watakubaliana na wewe.....!!!

Unaweza kushauri nini kifanyike na kipi kisifanyike ndani ya hiyo miezi 3???

Mfano, ni fair kupeana tunda katika huo muda mfupi??

Babu DC!!
 
Hiyo point kwamba usimhurumie mtu mpige chini tu ni muhimu sana kuizingatia hahaha ahsante kama binti huna mpango nae usikae nae sana lala mbele fasta.


Kaka usiwe mbinafsi,

Hata wadada wanatakiwa kuwapiga chini watoto wa mama wanaokuja kwa GFs wao na kuanza kulilia kama midoli inayotumia betri za Tiger!!

Babu DC!!
 
Asante sana Babu huu uzi utakuwa na manufaa sana kwangu...

Kumbe na wewe bado upo upo, unashangaa shangaa????

Haki ya nani, lazima mwaka huu tuwatambue Boys na Girls wote ili tunapoongea mambo ya watu wazima tuwaombe watupishe kwanza!!!!

Babu DC!!
 
Hapo kwa mwaka utakuwa na relationship ngapi??

Kwani maximum unatakiwa kuwanazo ngapi ndugu??

Kama hamtangulizi tamaa ya kubanjuana, nadhani ni strategy nzuri ili kuwajua waegeshaji!! Ila kama mtatanguliza libeneke basi hapo lazima wototo watachakaa kabla ya umri wao!!

Babu DC
 
Kuna falsafa moja inasema;Uongo uliwahi kuwa ukweli wakati fulani,lakini pia ukweli jambo ambalo halijapata jambo lingine la "kupruvu" otherwise.Yaani ukweli ni uongo mtarajiwa!
 
Asante sana babu nimepata somo,limeniingia sawia...na nitalizingatia.😛oa
Mungu akubariki sana...Happy new year to u!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…