RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
đź“–Mhadhara wa 21:
Wakati watanzania wenye akili timamu wanajiuliza hili swali; Tupate wapi njia za kuwanasua watoto wetu kwenye wimbi baya la ubakaji, ushoga, usagaji, na ulawiti? - lakini wanaibuka watu ambao tunawaamini ni kioo cha jamii (wasanii wa bongo fleva) wanakwenda studio kurekodi nyimbo zenye maudhui mabaya au maneno makali ambayo kwa namna moja ama nyingine zinahamasisha hayo matukio maovu.
Huenda nyimbo ambazo si za mapenzi hazina soko zuri, lakini haimaanishi kuimba mapenzi ni lazima utumie maneno ya wazi wazi au maneno makali. Wasanii wa zamani hasa wa kutoka Zanzibar waliimba nyimbo za mapenzi pasipo kutumia maneno makali, wala hawakutumia maneno ya kuwadhalilisha wanawake, hakika walitumia maneno matamu sana. Kwa kweli wasanii wa zamani wapewe maua yao.
Labda kilichowakwamisha wasanii wa zamani kutokuwa matajiri ni kwa sababu wakati ule matumizi ya soko la mitandaoni halikuwepo au lilichelewa kufika nchini, lakini si kwasababu hawakutumia matusi.
Lakini wasanii wa siku hizi (si wote ila ni wengi) wakiimba nyimbo za mapenzi huwezi hata kusikiliza mbele ya mtu mwingine, na hata kama utasikiliza pekee yako utaishia tu kufyonza na hutoweza kuendelea kusikiliza.
Right Marker
Dar es salaam
Sept 27, 2024.