Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Watanzania wana maumivu mengi na hasira kubwa dhidi ya CCM, chama ambacho kimekuwa kama syndicate ya kuwaumiza watanzania walio wengi na kuzineemesha familia chache kupitia kodi za hao wengi wanaoumizwa.
CCM imekuwa na kiburi kisichoelezeka. Wananchi, kupitia tume ya Warioba walisema wanataka katiba mpya, syndicate hii ya CCM imekataa. Wananchi kupitia tume ya Warioba walisema wanataka Tume Huru ya Uchaguzi, kikundi hiki ndani ya CCM kimekataa.
Kikundi hiki kimejimilikisha nchi na kila kitu kilichomo. Wanauza na kugawa rasilimali za nchi na kutapanya rasilimali za nchi hovyo. Wao ndio Tanzania na wao ndio CCM.
Fikiria kuwa sasa hivi, kwa kupitia Rais Mstaafu, wamefikia hata kutamka wazi kuwa 'wachawi ndani ya CCM wamekufa"!!. Ina maana viongozi walioaminiwa na watanzania kushika nafasi za juu katika nchi, walikuwa ni wachawi dhidi yao wao waliojimilikisha CCM. Hii inaongezea kwenye ile kauli ya, "wazuri hawafi".
CCM na hii syndicate, wanatakiwa kupumzishwa. Tanzania irudishwe kwa Watanzania, na CCM irudishwe kwa wanaCCM. Hilo halitawezekana kama hakutakuwa na chama chenye nguvu cha upinzani, chama kilicho madhubuti, na kinachoongozwa na watu madhubuti, watu walionyooka, watu wasiohongeka, watu wakweli wa kauli na nafsi zao, watu walio tayari kuteseka kwa njaa, huku pembeni kuna watu wanaowahonga chakula alimradi tu watoke kwenye misimamo yao thabiti.
Kwa sasa chama kilicho tegemeo pekee ni CHADEMA, lakini ndani ya CHADEMA, ile syndicate ya CCM imekwishajipenyeza, ndiyo maana tunashuhudia baadhi ya wagombea ndani ya CHADEMA, wakipigiwa kampeni kali na machawa wa syndicate ya CCM.
Wajumbe, zingatieni ukweli huu,
"Mkiona mgombea yeyote anapigiwa kampeni na kushabikiwa na machawa wa syndicate ya CCM, hamtakiwi kujiuliza mara 2, pigeni chini huyo mgombea, kwa sababu huyo atakuwa miongoni mwa hao walioletwa na syndicate ya CCM ndani ya CHADEMA kwaajili ya kulinda maslahi ya hiyo syndicate ya CCM, na kuua matumaini ya Watanzania.
kupigiwa kampeni, chapuo na machawa wa syndicate ya CCM, ni disqualification ya moja kwa moja ya kutompa kura mgombea huyo.
Wajumbe leteni uongozi imara utakaoitengeneza CHADEMA mpya, itakayowapa uwanja wananchi wa kuonesha hasira zao dhidi ya syndicate ya CCM, msilete uongozi utakaoifanya CHADEMA kuwa CCMB