Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Obama kafanikiwa kutetea kiti chake cha urais. Uchaguzi umeenda haraka na kwa uwazi na matokeo yametoka bila kigugumizi. Mshindani wake kakubali matokeo na mwisho wa siku maisha yanaendelea.
Bila ya shaka ni kwamba idadi kubwa ya watu nje ya Marekani walipenda kuona tena kuwa Obama anamalizia muda wake. Bila kujali vyama vyetu tulitamani hivyo na imekuwa.
Democrats ni chama tawala na Republican ni wapinzani. Walio nje ya Marekani wengi watu tulitaka chama tawala kiendelee na utawala na upinzani upotezewe.
Tuko katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu hapa Tanzania. Chama kikuu cha upinzani ni cdm, na chama tawala ni ccm. Tulio wanachama na mashabiki wa cdm tulitaka chama tawala Marekani-Democrats waendelee na upinzani-Republican washindwe, na tukafurahi. Hii inaleta picha gani kwetu? Ni nini hasa nguvu ya chama tawala? Labda mazingira yanatofautiana, lakini siasa ni zile zile.
Kwa nini tupende chama tawala kiendelee kwa wenzetu wakati kwetu tunataka kuking'oa?