Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,271
- 1,052
Waliomwadhibu wangeachwa peke yao wakauke kama vigae na nyongo zao.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, alilitangazia taifa kuwa dili ya Richmond ilikuwa safi na taifa halikupata hasara yoyote.
Baada ya ukweli kujulikana sambamba na hasara kubwa kubainishwa, mawaziri walijiuzulu, mkataba ukavunjwa na kwa ajili hiyo serikali yote ilivunjwa ikaundwa upya.
Huu ni mwaka wa ngapi, Hosea yupo palepale. Sasa anawakamata wenzake. Anaendelea kulipwa fedha za wale wale wananchi aliowadanganya.
Sasa hivi wanasikia serikali inafanya mpango wa kumlipa gumegume mmoja tu shilingi bilioni 222 ili achapishe vitambulisho, kazi ambayo Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali anasema anaweza akaifanya kwa shilingi bilioni 95 tu. Kwa nini walimu wasisimame kidete kudai kuokolewa kwa shilingi bilioni 127 ambazo ni zaidi ya kuboresha maisha yao wote!Waliwaambia serikali haina fedha, sasa fedha hizi hapa zimeonekana. Kama Spika Samuel Sitta amezuia hoja ya kumjadili Lawrence Masha ili haya yote yasijitokeze, kwani Urambo kwenye jimbo lake hakuna walimu? Hakuna wanafunzi? Hakuna wazazi? Akija nendeni nyumbani kwake si mbunge wenu (kijana wenu) mkamuulize awaeleze ilikuwaje?
DC, Albert Mnali hakuwachapa walimu wote aliokutana nao na aliowachapa hakuwachapa kwa ualimu wao. Aliwachapa walevi, watoro, na ambao hawakutimiza wajibu wao. Anayetetea uozo huu ni sehemu ya uozo wenyewe.