Hakuna anayekukatalia ila hifadhi nayo ina utaratibu hasa ikitaka kuanzishwa eneo ambalo tayari shughuli za binadamu zimeanza kufanyikaWakati wanataka kulima waluomba kibali? Sheria ipo wazi haijarishi Kuna ukame kiasi gani kama ni eneo halitakiwi kwa shughuli za kilimo basi inatakiwa mheshimu.
Hata hiyo hifadhi Ina faida yake, ungeelewa kuhusu "ECOLOGY" Wala usinge leta hapa hayo malalamiko Yako. Siku nyingne mfate Sheria. Poleni.
Hawa ndiyo aina ya Viongozi unaowatetea kila uchwao!POLENI SANA MKUU
Poleni...bahati mbaya haya hayatawezekana mkiendelea kuwaunga mkono chama cha majambazi na mauaji....Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo mgogoro mkubwa kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la Bushenya na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera.
Jina “Bushenya” lina historia na maana ya kina.
Kwa lugha ya Kihaya, kushenya humaanisha kuchanja kuni, yaani shughuli ya kukata na kuchanja kuni kwa matumizi ya nyumbani. Hivyo, Bushenya ni eneo ambalo wazawa walilitumia tangu enzi na enzi kuchanja na kupata kuni, nishati muhimu ya maisha ya kila siku. Maana hii inaonesha wazi kuwa eneo hili limekuwa likitumiwa na jamii kwa manufaa halisi kwa vizazi vingi, muda mrefu kabla hata ya kufikiriwa kuwa hifadhi ya msitu katika miaka ya hivi karibuni.
Bushenya ni eneo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa takribani hekta 9,000. Kwa zaidi ya miaka kadhaa, wananchi wamekuwa wakilitumia eneo hili kwa shughuli za kilimo cha chakula na kilimo cha biashara, hasa miwa, kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hadi sasa, wananchi wamekwisha kuendeleza na kulima takribani hekta 4,000. Maeneo haya tayari yamepandwa miwa na mazao mengine. Zaidi ya hapo, Kagera Sugar Limited imekwisha tengeneza barabara zinazofika karibu kila shamba la mkulima, jambo linalothibitisha kuwa shughuli hizi zilifanyika waziwazi na kwa muda mrefu bila pingamizi.
Kinachozua maswali mazito kwa wananchi ni hili:
👉 Kwa nini Halmashauri iliruhusu yote haya yafanyike kwa miaka mingi, halafu leo ijitokeze ghafla kudai eneo hilo ni hifadhi ya msitu?
Leo hii, Halmashauri ipo katika mchakato wa kulitangaza eneo la Bushenya kuwa hifadhi ya msitu, bila ushirikishwaji wa wananchi waliolima na kuendeleza ardhi hiyo kwa miaka mingi na halmashauri za vijiji vilivyozunguka eneo hilo.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba:
• Kesi kuhusu mgogoro huu zipo mahakamani;
• Hata hivyo, Halmashauri imeanza kuingia mashambani kwa kutumia vikosi vya ulinzi;
• Mazao ya wananchi yanafyekwa na kuharibiwa;
• Wananchi wanatimuliwa bila fidia, bila maridhiano, na bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Hatua hizi zinatafsiriwa na wananchi kama:
• Dhihaka kwa utawala wa sheria;
• Ukiukwaji wa haki ya kumiliki na kutumia ardhi;
• Matumizi mabaya ya madaraka kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi, badala ya maslahi ya wananchi.
Wananchi wa maeneo ya Bushenya hawaipingi hifadhi ya mazingira. Wanachokataa ni:
❎Kubughudhiwa
❎Kunyanyaswa
❎Kuondolewa kwa nguvu bila haki na fidia
Wananchi wanataka:
✅Heshima ya sheria
✅Mazungumzo ya haki na uwazi
✅Fidia stahiki endapo ardhi itachukuliwa
✅Kusitishwa mara moja kwa uharibifu wa mazao
Bushenya si suala la msitu pekee.
Ni suala la historia ya jamii, maisha ya wananchi, haki za ardhi, na utu wa binadamu.
📣Haki itendeke. Sheria iheshimiwe. Wananchi wasikilizwe.
View attachment 3518091
View attachment 3518092
Who care?Kwa kusikitisha zaidi, viongozi hao wa wilaya wamefikia hatua ya kuyafyeka mazao ya chakula, yakiwa yamefikia takribani miezi mwezi mmoja na nusu wa ukuaji. Kitendo hiki kinaonesha wazi kutokujali jasho la mkulima na kutozingatia athari za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wanaotegemea kilimo hicho.
Inasikitisha sanaSerikali imetangaza kuwepo kwa ukame katika baadhi ya mikoa nchini. Hata hivyo, licha ya taarifa hizi za kitaifa, viongozi wa Wilaya ya Missenyi wamepuuza uhalisia uliopo katika Mkoa wa Kagera—hasa Bukoba na Missenyi—ambapo kumekuwa na mvua za kutosha na mazingira mazuri kwa uzalishaji wa chakula.
Kutokana na mvua hizo, wananchi wamejituma kulima mazao ya chakula, hususan mahindi na mtama, katika eneo la Bushenya. Licha ya ukweli kwamba eneo hili si hifadhi wala msitu tengefu, viongozi wa Wilaya ya Missenyi wameshindwa kutambua juhudi za wananchi na kuchagua kuchukua hatua zisizo na tija wala huruma.
Kwa kusikitisha zaidi, viongozi hao wa wilaya wamefikia hatua ya kuyafyeka mazao ya chakula, yakiwa yamefikia takribani miezi mwezi mmoja na nusu wa ukuaji. Kitendo hiki kinaonesha wazi kutokujali jasho la mkulima na kutozingatia athari za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wanaotegemea kilimo hicho.
Inashangaza kuona viongozi wa Wilaya ya Missenyi wakishindwa kuvumilia kwa muda mfupi ili mazao yavunwe kwanza, kisha wakae mezani na wananchi kujadili kwa busara na haki suala la umiliki au matumizi ya eneo husika. Kukosa uvumilivu huu ni ushahidi wa uamuzi wa haraka usiozingatia maslahi ya wananchi.
Hatua ya kuharibu chakula wakati nchi inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa chakula ni kosa kubwa la kiuongozi. Viongozi wa Wilaya ya Missenyi wanapaswa kuwajibika kwa kitendo hiki ambacho kimewaumiza wananchi, kimekatisha tamaa wakulima, na kupingana na juhudi za taifa za kuhakikisha usalama wa chakula.
Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza na kuwawajibisha viongozi wa Wilaya ya Missenyi waliohusika na maamuzi haya, na kuhakikisha kuwa haki ya mkulima inalindwa, maamuzi yanazingatia utu wa binadamu, na maslahi ya wananchi yanawekwa mbele.
View attachment 3518065
View attachment 3518066
View attachment 3518067
Pamoja na yote lakini kwa sasa ndo inajukumu la kuhakikisha kero za raia wake zinapungua au kuisha kabisa. Kuna watendaji hasa wa huku chini wanatia doa sana serikali ujue kwa masrahi binafsi wakati mwingine.Baba hii serikali haramu. Hakuna wa kumsikiliza mkulima wote wanamuona kama nguruwe huyu mtanzania
Umeharakisha kujibu ungeuliza kwanza. Kesi zipo mahakamani kinachoshangaza nikuona uharaka wa halmashauri kukata mazao wakati kesi bado zinaendelea. Ndo sababu hasa ya kuona kama kuna nia siyo njemaWakati wanataka kulima waluomba kibali? Sheria ipo wazi haijarishi Kuna ukame kiasi gani kama ni eneo halitakiwi kwa shughuli za kilimo basi inatakiwa mheshimu.
Hata hiyo hifadhi Ina faida yake, ungeelewa kuhusu "ECOLOGY" Wala usinge leta hapa hayo malalamiko Yako. Siku nyingne mfate Sheria. Poleni.