Ujumbe wa Mwaka Mpya 2011 Ulionivutia na Kunichekesha

Ujumbe wa Mwaka Mpya 2011 Ulionivutia na Kunichekesha

IshaLubuva

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2008
Posts
250
Reaction score
11
Ni kawaida kila inapofika nyakati za mwisho wa mwaka watu hutumiana ujumbe kwa njia ya simu na mitandao kutakiana kheri ya Noeli na mwaka mpya. Binafsi nilipikea ujumbe mwingi tu, lakini kati ya yote niliyoipokea, ujumbe huu ulinipa burudani. Ujumbe unasomeka hivi:

"Naomba uniazime sh. 300,000/- tu nina shida nazo hasa siku ya kesho. Help me please, I know you have them. Alisikika mlevi mmoja akiiomba mashine ya ATM saa 6 usiku!!.

Khaa!!! ulivyostuka ulifikiri nakuomba wewe, ukaanza kuandaa fiksi za kunitolea nje!. Nakutakia kheri ya mwaka mpya 2011"

Huu ujumbe nilivyoupokea kwanza nilisoma hadi kwenye sentensi yenye rangi nyekundu, fikiria ilikuwa ni usiku tarehe 31/12/2010, nikabloo mapigo. Nikaanza kutafakari hiyo sentensi yenye rangi nyekundu kwa jinsi ilivyokuwa na uzito. Nilivyosoma sms kwa mara ya pili hadi mwindo ndo nikapumua na kujua kwamba jamaa alikuwa kanitega.

Hebu na wewe lete uzoefu wa sms ulizokumbana nazo
 
Hiyo ilikuwa kali. hembu sikia na hilo swali nililoulizwa la kufungia mwaka labda mnaweza kunisaidia majibu. swali lilikuwa hivi,
MTIHANI WA MAARIFA YA DUNIA
SECTION G:
Swali la 5 marks 60 Muda dk 10.
a)Kama hela hazioti kwenye miti kwa nini benki zina matawi?
b)Kwa nini gundi haigandi kwenye chupa yake?
c)Kama tunatakiwa tusiendeshe gari wakati tumelewa kwa nini bar zina sehemu ya kuegeshea magari?
d)Kama neno "Abbreviation"linamaanisha kifupisho kwa mbona lenyewe ni refu hivyo?
e) Kama kujamiiana ni wakati wa ndoa tu kwa nini tunakua kabla ya ndoa?

Naimani mtanipatia majibu katika mwaka huu mpya.
 
Nilipata hii mwaka mpya. Pole sana na uchovu wa ujenzi wa taifa.Ripoti yako ya mwaka 2010 imetoka! Ni kama ifatavyo:
kuoga - B
wivu -B
uvumilivu -D
ulevi -B
utu wema -C
uchonganishi -C
upole -D
kuzurura -A
kujituma C
mapenzi -A
uongo -B
kuropoka -C
kusali -F

Unacheka ? unafikiri vizuri ? Jirekebishe 2011. Tatizo alienitumia simjui naona alikosea namba.
 
ninacho kitaka kina A lakini ningependa KUZURURA NA KUSALI zibadilishane halafu kila kitu shwari...
 
Hi ilinifurahisha: (esp. kama unajua kichagga!)

Shimbony, Happy easter!
ote, Happy eid mubarak!
Mbutaa, Ngachanganyikiwo bana!
ooh, happy Birthday!
Wai ngasuko ulalu, happy chagga day!
Cha!
Ngamkumbuo mlya,
"Merry x-mas na maka mhya!" naiyo cha!!!!
 
Na hii imebadilishwa tu iendane na wakati uliopo!
Kwa mwaka huu mpya wa 2011 nakuombea;
Furaha yako iongezeke kama ahadi za kikwete,
Mashaka yako yapungue kama kura za ccm 2010,
umaarufu wako uongezeke kama Dr. Slaa,
hekima zako zizagae kama mabango ya kampeni ya ccm,
wanaokuombea mabaya wapotee kama fedha zetu za kodi,
uwepo wako kila mahali uwe wa thamani kama notisenti hamsini ya nyerere,
na shida zikuondoke ghafla kama umeme wa tanesco,
uwe na amani!
 
tutafsirie basi..... sasa mwataka mfaidi wachaga kwa wachaga tuu???
Hi ilinifurahisha: (esp. kama unajua kichagga!)

Shimbony, Happy easter!
ote, Happy eid mubarak!
Mbutaa, Ngachanganyikiwo bana!
ooh, happy Birthday!
Wai ngasuko ulalu, happy chagga day!
Cha!
Ngamkumbuo mlya,
"Merry x-mas na maka mhya!" naiyo cha!!!!
 
Nipo internet nasoma majina ya watu watakaoingia 2011. Jina lako halipo nahakuna 2nd selection. tuma vocha ya elfu 10 ili tukachakachue jina laoki liwe Na. 1. Happy new year
 
Hi ilinifurahisha: (esp. kama unajua kichagga!)

Shimbony, Happy easter!
ote, Happy eid mubarak!
Mbutaa, Ngachanganyikiwo bana!
ooh, happy Birthday!
Wai ngasuko ulalu, happy chagga day!
Cha!
Ngamkumbuo mlya,
"Merry x-mas na maka mhya!" naiyo cha!!!!
hiyo hata mie ilinifurahisha sana!
 
Na hii imebadilishwa tu iendane na wakati uliopo!
Kwa mwaka huu mpya wa 2011 nakuombea;
Furaha yako iongezeke kama ahadi za kikwete,
Mashaka yako yapungue kama kura za ccm 2010,
umaarufu wako uongezeke kama Dr. Slaa,
hekima zako zizagae kama mabango ya kampeni ya ccm,
wanaokuombea mabaya wapotee kama fedha zetu za kodi,
uwepo wako kila mahali uwe wa thamani kama notisenti hamsini ya nyerere,
na shida zikuondoke ghafla kama umeme wa tanesco,
uwe na amani!

hii nimeipenda sana
 
Back
Top Bottom