Ujumbe wa Simu Wamuumbua Mume Mkware

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Monday, June 08, 2009 3:50 AM
Mwanaume mmoja mkware nchini Uturuki aliumbuka vibaya baada ya kugundua kuwa mwanamke aliyemfungia safari kwenda kukutana naye baada ya kutongozana kwa kutumia ujumbe wa simu kwa muda mrefu alikuwa ni mkewe aliyekuwa akimchunguza kama ana kimada nje. Mke wa mwanaume huyo mkazi wa mji wa Trabzon, nchini Uturuki alikuwa akimshuku mumewe kuwa na kimada nje kutokana na mabadiliko ya tabia zake aliyoyaona.

Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina moja la Hulya alisuka mpango wa kupima uaminifu wa mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Murat.

Hulya mwenye umri wa miaka 22 ili kujua kama mumewe ana kimada nje aliamua kuchukua simu ya ndugu yake na kuanza kumtumia mumewe meseji za kimapenzi akijifanya kuwa yeye ni mwanamke aliyevutiwa naye na anataka wawe na uhusiano wa kimapenzi.

Mumewe imani ilimshinda na alinasa kwenye mtego huo na kuanza kujibu meseji hizo kwa meseji kibao za mapenzi mpaka kufikia kupanga siku na sehemu ya kukutana ili waanze kujivinjari.

Mume huyo bila kujua kuwa mwanamke aliyekuwa akitumiana naye meseji alikuwa ni mkewe, alimuaga mkewe kuwa anatoka kidogo usiku kuonana na rafiki yake na atachelewa kurudi.

Huku akiwa na shauku kubwa ya kumuona mwanamke aliyekuwa akitongozana naye kwa simu, mume huyo mkware alipigwa na butwaa baada ya kuona mwanamke aliyejitokeza alikuwa ni mkewe tofauti na hesabu zake alizokuwa akipiga.

Kwa hasira mume huyo alimshushia kipigo mkewe hapo hapo na kusababisha polisi waliokuwa wakipita karibu na eneo la tukio kuingilia kati na kumkamata mume huyo.

Hulya hakuwa na nia ya kumfungulia mashtaka mumewe pamoja na kwamba alimjeruhi lakini polisi waliomkamata mumewe waliamua kumfungulia mashtaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…