Ujumbe wa SMZ watembelea miradi mitatu ya kimkakati ya NHC jijini Dar es Salaam

Ujumbe wa SMZ watembelea miradi mitatu ya kimkakati ya NHC jijini Dar es Salaam

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Ujumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC) umetembelea miradi mitatu ya kimkakati inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC.

Ziara hiyo iliyoratibiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanyika leo tarehe 17 Disemba 2024 katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, ujumbe huo umepewa maelezo ya kina kuhusu maendeleo ya mradi wa Seven Eleven (711) ambapo Msimamizi wa Mradi, Samuel Metili aliongoza ujumbe huo kutembelea eneo hilo la mradi.

Mradi wa Seven Eleven (711) Kawe umerejea rasmi kwa mkandarasi @esteemconst ction kurejea eneo la ujenzi kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ulioanza mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika rasmi Desemba 2018.

Mradi huo upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fukwe za bahari ya Hindi sambamba na karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni.

Pamoja na Mradi Kawe 711, Miradi mingine inayotekelezwa na NHC ni Mradi wa Samia Housing Scheme pamoja na Morocco Square jijini Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom