Ujumbe wangu kwa Edo Kumwembe

Ujumbe wangu kwa Edo Kumwembe

A swahili Kid

Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
39
Reaction score
38
"Habari brother!!!!

Habari za leo Edo Kumwembe? Pole sana na majukumu mazito sana ya Uchambuzi hapo Wasafi!!!Pole na kazi nzuri sana ambazo umekuwa ukizifanya kwa nyakati tofauti tofauti zinazowa 'inspire' vijana.....Hongera pia kwasababu wewe ndio uti wa mgongo wa vijana wengi wachambuzi na waandishi wa makala za michezo Tanzania (nikutoe hofu mimi sio miongoni mwao).

Ila,niwe muazi kuwa ninafurahishwa na hicho ambacho umekuwa ukajifanya kwa bidii kiasi cha kukirithisha kizazi na kizazi kwa ukubwa na Uzuri zaidi.

Bila shaka,kuna mengi sana mazuri ya kusimuliwa kutoka kwako na kutoka kwenye kalamu yako Mungu mlezi akupe umri mrefu ili vijana wengi zaidi warithi ujuzi wako.

'Meseji' yangu hii kwako ni kukujuulisha kitu kimoja kaka...UNAKWAMA SEHEMU.

Tupo kwenye 'era' ambayo ulihitajika zaidi kuwaweka vijana kwenye mistari Kama 'legend' sio na wewe kutoka nje yake

Kwenye 'era' hii ya akina Wilson Oruma,Jemedari Said,Dominic Salamba,George Job ulihitajika zaidi wewe kuwaweka kwenye mistari mnyoofu.

Kuwakumbusha 'Uchambuzi' ni kazi ya wito na nguvu ni ajira pia ya kukirithisha vizazi na vizazi.....
Ulipaswa kuwakumbusha 'Uchambuzi' sio kivuli cha kuichafua 'taasis' fulani,kumvunjia moyo na kum attack mtu/mchezaji fulani sio na wewe uingie kwenye mkumbo huo.

Kwenye 'era' hii ambayo wachambuzi 'wanahisiwa' kupokea fedha kutoka kwa viongozi wa vilabu vyetu vya Kariakoo ili kumsifia mchezaji ambaye hawajawahi kumuona Ila kasajiliwa na hivyo vilabu,au kumponda mchezaji ambaye ameteleza mara moja au mara mbili ulipaswa kabisa kuwa mfano kwao kwa kufanya tofauti na wao

Brother Edo!!!kadiri tunavyofundishwa na Skysports na DSTV uchambuzi sio ubashiri,ndio maana hakuna mchambuzi hata mmoja kwenye hivyo vituo anaweza akasema 'team' fulani haiwezi kumfunga 'team' fulani,badala yake wata Anisha mifumo, mbinu, key players na quality wataishia hapo (kwenye uchambuzi).

Suala la nani 'favorite' kila siku wamekuwa wakisisitiza kila siku wachambuzi wa Skysports kuwa hilo sio swali la kiuchambuzi ni suala la kihisia na hakuna mchambuzi anapaswa kuruhusu hisia nyakati anazopaswa kufanya uchambuzi

Haiwezi kueleweka hata siku moja,kusema mchezaji fulani hawezi kuitwa national team ya Taifa fulani (huo sio uchambuzi).

Brother!!Nyakati ambazo unapaswa kuwaweka kwenye mistari kina Wilson Oruma wewe unaamua kuwa Wilson Oruma aliyezeeka?

Nyakati ambazo inafikirika wachambuzi kupokea BAHASHA wewe unaamua kuwaonesha wanazengo kuwa Kuna baadhi ya hizo BAHASHA zinapitia kwako pia

Brother!!!Ninajua unajua kuwa thamani ya uzee ni busara na hekima jaribu kuishi navyo.

Kama inashindikana kuwakosoa kina George Job na Gift Macha basi jitofautishe nao kimaongezi na kimatendo.

Kwa umri wako kiigizo chako kizuri kimaongezi na matendo kilipaswa kuwa Ally Mayai na sio hao akina Salamba

Thamini heshima ambayo umetumia muda mrefu mno kuijenga".

Ahsante sana kwa kusoma Meseji yangu.

Screenshot_20230321-125236_1.jpg
 
Nyie hata hamjui kitu, unadai kutazama Skysports na BBC wakati nao huwa wanabashiri matokeo kulingana na namna wanavyoona ubora na udhaifu wa timu zote mbili zilivyo, mchambuzi kukosea kubashiri haliwezi kuwa kosa la jinai, wao sio miungu, hebu acheni ushamba wenu.
 
Nyie hata hamjui kitu, unadai kutazama Skysports na BBC wakati nao huwa wanabashiri matokeo kulingana na namna wanavyoona ubora na udhaifu wa timu zote mbili zilivyo, mchambuzi kukosea kubashiri haliwezi kuwa kosa la jinai, wao sio miungu, hebu acheni ushamba wenu.
Hao pia wanaegemea timu wanazozishabikia.
 
Back
Top Bottom