Ujumbe wangu kwa watanzania kuhusu katiba mpya

Ujumbe wangu kwa watanzania kuhusu katiba mpya

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Mchakato wa katiba mpya umeingia doa baada ya udini, itikadi za siasa kutawala. Nimejaribu kujiuliza maswali mengi kuhusu utaratibu mzima wa kutoa maoni, kuunda mabaraza na hatimaye bunge la katiba.

Wakati wa kutoa maoni taarifa hazikutolewa, mchakato wa kuupata wajumbe wa kuunda mabaraza ya katiba upo kinyemela. pamoja na kuwaamini sana baadhi ya wajumbe katika tume ya kuunda katiba mpya ila kwa hali ilipofika sina imani nao tena akina Warioba, Butiku, mwesiga Baregu. Hivi wamekubali historia iwahukumu kwani mchakato umejaa ubabaishaji mkubwa.

Kwa nini waliamua viongozi kama wenyeviti wa mitaa na wale wa baraza la maendeleo ya kata wasimamie uchaguzi huu wakati wanajua wengi ni watiifu kwa vyama vyao? halafu mbona wamewatoa wajumbe wengine katika baraza la maendeleo la kata kushiriki katika mchakato huo kama vile walimu wakuu, wataalamu mbalimbali?

kwa nini wasingeunda tume huru ambayo ingeongozwa na walimu na wataalamu wengine wasio na mlengo wa kiitikadi.

Naomba watanzania tuungane katiba ni roho ya taifa letu tuukatae uccm, uchadema, u cuf nk bali tuweke utanzania mbele katiba ituunganishe itoe usawa katika rasilimali za nchi. Niwaulize wenyeviti ambao leo hii wana maisha duni pamoja na watoto wao wanapata faida gani kwa kusikiliza na kuwa watii kwa CCM na wako tayari kuharibu mchakato wa katiba mpya kwa lengo tu la kutetea udhalimu wa viongozi, watanzania tutakuwa wajinga hadi lini?

Leo hospitali hakuna dawa, viongozi wanatibiwa nje, shule hazina vifaa watoto wanaoumia ni wa watoto wa kipato cha chini, watanzania wengi wanalia huku viongozi wetu wakisomesha watoto wao nje kwa pesa za watanzania.

Naomba rais kama untaka kuheshimiwa tafadhali ingilia kati mchakato huu vinginevyo ni aibu maana inaonekana ccm wamejipanga kutengeneza katiba ya ccm wala si ya Tanzania. Hv viongozi vitu vingine hamuoni hata aibu maana vitendo vilivyofanyika katika sehemu nyingi ni aibu.
 
Back
Top Bottom