UK yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Shahawa

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.

Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.


Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.


Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.


Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.


Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.

Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005. chanzo.BBC
 
Du si wangekuja huku jamani wakaweka vyombo maalum kwenye while za boarding za wavulana?
 
Du si wangekuja huku jamani wakaweka vyombo maalum kwenye while za boarding za wavulana?
Wazungu washenzi hawataki kushirikiana damu na watu weusi Wazungu ni wabaguzi wanahiyari wakose watoto kuliko kushirikiana Damu na watu weusi Wazungu ni wabaguzi wa Rangi. Wengi wa Wazungu hivi sasa ni Mashoga wameruhusu Ushoga wataweza tena kuzaa? Mungu amewapiga laana hiyo.
 

Nakubaliana nawe kwa asilimia zote ushoga sasa ulaya ni kitu cha kawaida kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…