Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mkandara.

acha nao hawa.
Mkapa alipelekewa malalamiko na waislam kuwa primary school Dar waislam ni wengi sana inakuwaje ukienda juu hawapo?yaani huko mbele kuna wakristu wengi?

kwa majibu ya Mwanakijiji na Yebo yebo basi waislam wanaonewa kwani wao ni wengi huku chini ila juu hawaonekani. na wana kila sababu ya kudai wao wengi kwanza wana wake zaidi ya mmoja hivyo population yao ni kubwa. lakini jibu alilotoa mkapa si kweli kama kuna uonevu.
 
Wazeee MMJ na Yebo2,

Kwa mantiki yenu hapo juu, ina maana kwamba kabila leny wancnhi wengi ndilo liruhusiwe kutawala mashirika ya umma na serikali au?

Sasa tukiiikubali sera ya majimbo itakuwaje? au ndio maana kumbe ndugu zetu wanaililia sana hiyo sera, yaani ni kwa sababu wao ni wengi kuliko makabila mengine?

Na wenzetu UN wanaolalamika na Mama Tibaijuka kuajiri Wahaya wengi huko mnaionaje hiyo, au nayo ni Wahaya wengi mno duniani kuliko makabila mengine duniani?
 
Es.
Hiyo Sera Ya Majimbo Anaoipigia Debe Ni Phillimon Mikael Na Chama Chake Cha Chadema. Kifupi Umajimbo Ni Ukabila.
 

mimi kabila gani?
 
Duuuh Mswahili,
Nimependa sana hizo hesabu zako...Unajua kweli kama huna upeo unaweza kuamini kuwa waislaam ni wengi zaidi tena mara mbili ya wakristu kwa sababu wao wana wake zaidi ya mmoja hadi kufikia wanne kuna kila possibility ya wao wawe wengi.... Anyway tuachane na haya maanake naona sasa hivi tumeondoka kabisa huko TRA.
Na wachangiaji wameshindwa kuelewa kuwa hata mimi nilimkatalia Mswahili kwa hili lakini aliponipa ushahidi ambao hauna ubishi kabisa kuwa huo ni ukabila...Unless hawa jamaa wanaweza kuja mna maelezo ya kutufundisha sisi hizo ajira za Ukabila huwa zinatolewa vipi tofauti na sisi tunavyofikiria.

Mzee Es,
Hii ndio nilikuwa naipigia kelele sana kule kwenye majimbo na sasa umeona mwenyewe jinsi inavyoweza kupambwa ikaonekana hakuna ubaguzi!
 


Aasáx [aas] 350 (1999 Jeff Carr
Alagwa [wbj] 30,000 (2001 Kiessling
Arabic, Omani Spoken [acx] Ethnic population: 195,000 in Tanzania (1993 Johnstone).

Aramanik [aam] 3,000 (2002)
Asu [asa] 500,000 (2000).

Bena [bez] 670,000 (2001 Johnstone and Mandryk
Bende [bdp] 27,000 (1999
Bondei [bou] 80,000 (1987).
Bungu [wun] 36,000 (1987).
Burunge [bds] 13,000 (2002).

Datooga [tcc] 87,798 (2000 WCD
Dhaiso [dhs] 5,000 (1999).
Digo [dig] 88,000 in Tanzania (1987).
Doe [doe] 24,000 (1987).

Fipa [fip] 200,000 in Tanzania (1992 UBS).
Gogo [gog] 1,300,000 (1992 UBS).
Gorowa [gow] 50,000 (1999 R. Kiessling).
Gujarati [guj] 250,000 in Tanzania (1993 Johnstone).
Gweno [gwe] : 2,000 or more.
Ha [haq] 990,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Hadza [hts] 800 (2000 Brenzinger).
Hangaza [han] 150,000 (1987).
Haya [hay] 1,200,000 (1991 UBS).
Hehe [heh] 750,000 (1994 UBS).
Ikizu [ikz] 28,000 (1987).
Ikoma [ntk] 15,000 (1987).
Iraqw [irk] 462,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Isanzu [isn] 32,400 (1987).
Jita [jit] 217,000 (1987).


Kagulu [kki] 217,000 (1987).
Kahe [hka] 2,700 (1987).
Kami [kcu] 16,411 (2000 WCD). More information.
Kara [reg] 86,000 (1987).
Kerewe [ked] 100,000 (1987). More information.
Kimbu [kiv] 78,000 (1987).
Kinga [zga] 140,000 (2003). More information.
Kisankasa [kqh] 4,670 (1987). Alternate names: "Ndorobo", "Dorobo". Dialects: A distinct language from others called "Dorobo": Aramanik, Mediak, Mosiro. See also
Kisi [kiz] 10,200 (2001).
Konongo [kcz] 51,000 (1987).
Kuria [kuj] 213,000 in Tanzania (1987).
Kutu [kdc] 45,000 (1987).
Kwaya [kya] 102,000 (1987).
Kwere [cwe] 98,000 (1987).
Lambya [lai] 40,000 in Tanzania (1987).
Langi [lag] 350,000 (1999 Hartung and Stegen).
Luguru [ruf] 692,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Luo [luo] 280,000 in Tanzania (2001 Johnstone and Mandryk).
Maasai [mas] 430,000 in Tanzania (1993).
Machame [jmc] 300,000 (1992 UBS).
Machinga [mvw] 36,000 (1987).
Magoma [gmx] 9,000 (SIL 2003).
Makhuwa-Meetto [mgh] 360,000 in Tanzania (1993)
Makonde [kde] 1,140,000 in Tanzania (2001 Johnstone and Mandryk).
Malila [mgq] 65,000 (2003 SIL).
Mambwe-Lungu [mgr] 97,000 in Tanzania (1987).
Manda [mgs] 22,000 in Ludewa District (2002).
Maraba [ymk] 10,000 in Tanzania (2003
Matengo [mgv] 150,000 (1987
Matumbi [mgw] 72,000 (1978 MARC).
Mbugu [mhd] 7,000 (1997).
Mbugwe [mgz] 24,000 (1999).
Mbunga [mgy] 29,000 (1987).
Mediak [mwx] 5,268 (2000 WCD).
Mochi [old] 596,656 (2000 WCD).
Mosiro [mwy] 5,268 (2000 WCD).
Mpoto [mpa] 80,000 (1977 Voegelin and Voegelin
Mwera [mjh] 6,000 (2004).
Mwera [mwe] 469,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Ndali [ndh] 150,000 in Tanzania (1987
Ndamba [ndj] 55,000 (1987
Ndendeule [dne] 100,000 (2000 Deo Ngonyani
Ndengereko [ndg] 110,000 (2000
Ndonde Hamba [njd] 10,000 to 20,000 (2002 PBT).
Ngasa [nsg] 200 to 300 (1983).
Ngindo [nnq] 220,000 (1987).
Ngoni [ngo] 170,000 in Tanzania (1987
Ngulu [ngp] 132,000 (1987)
Ngurimi [ngq] 32,000 (1987
Nyilamba [nim] 440,000 (1987
Nindi [nxi] 100.
Nyakyusa-Ngonde [nyy] 750,000 in Tanzania (1992 UBS
Nyambo [now] 400,000 (2003)
Nyamwanga [mwn] 87,000 in Tanzania (1987
Nyamwezi [nym] 1,200,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Nyaturu [rim] 556,000 (1993 Johnstone )
Nyiha [nih] 306,000 in Tanzania (1987).

Pangwa [pbr] 95,000 (2002
Pimbwe [piw] 29,000 (1987
Pogolo [poy] 185,000 (1987

Rufiji [rui] 200,000 (1987)
Rungwa [rnw] 18,000 (1987)
Rwa [rwk] 90,000 (1987)
Safwa [sbk] 158,000 (1987).
Sagala [sbm] 79,000 (1987)
Sandawe [sad] 40,000 (2000)
Sangu [sbp] 75,000 (1987
Segeju [seg] 7,000 (2003 SIL)
Shambala/Sambaa [ksb] 664,000 (2001 Johnstone and Mandryk )
Shubi [suj] 153,000 (1987).
Sizaki [szk] 82,000 (1987).
Suba [suh] 30,000 in Tanzania (1987).

Sukuma [suk] 3,200,000 (2001 Johnstone and Mandryk).
Sumbwa [suw] 191,000 (1987).
Swahili [swh] 540,837 in Tanzania (2000 WCD

Temi [soz] 30,000 (2002 SIL).
Tongwe [tny] 13,000 to 15,000 (2001)
Vidunda [vid] 32,000 (1987).
Vinza [vin] 10,000 (1987)
Vunjo [vun] 300,000 (1992 UBS) More information.
Wanda [wbh] 24,000 (1987).
Wanji [wbi] 28,000 (SIL 2003

Yao [yao] 492,000 in Tanzania (2001 Johnstone and Mandryk
Zanaki [zak] 62,000 (1987).
Zaramo [zaj]656,730 (2000
Zigula [ziw] 355,000 (1993 Johnstone).
Zinza [zin] 138,000 (1987
 
Mzeee MMJ,

Heshima mbele na takwimu zako, lakini what does it have to do na TRA, Hazina, na Foreign kuwa na wachagga wengi?

I mean more respect kwa data!
 
Mwanakijiji,
hata sielewi unacho jaribu ku-prove hapa.
Udogo sio hoja kabisa isipokuwa tunachosema sisi ni nafasi za kazi TRA ambayo inashughulika Tanzania nzima sio toka kitongoji cha Kilimanjaro peke yake!
Wamarekani weusi ni asilimia 10% ya population ya Marekani, hii haiwezi kutumika kama kigezo cha kutoajiri weusi ama kusema hawawezi kuwa na elimu, uwezo na ufanisi na ndio maana nikasema kuhusu population. (on that basis). Wachagga hata nusu ya mfano huo hawapo.
Kila naposoma mawazo yako ni kama vile unasema Wachagga ndio wanaostahili nafasi za kazi kuliko makabila mengine.. ila unafunika na viji sababu ambavyo hautuonyeshi uhalali wa madai yako kuwa TRA ni lazima iwe na wachagga wengi!.. Nyerere aliweza kutupa sababu kwa nini wachagga, Wanyakyusa na Wahaya walishika nafasi za juu... leo wewe unatazama upande mwingine kabisa kutoa hoja zako.
Mwanakijiji,
Hapa unatumia sana siasa za Kibongo maanake unapowauliza swali kuhusu chama chao (Chadema ama CCM) wao badala ya kujibu hoja, utawasikia waki - point wengine mbona nao wanafanya ama hawafanyi kuhalalisha mabaya yao.
 



mhhhhh sijui nisemeje kuhusu hizi data
 



kupata elimu mapema ?
what a joke

kwani nchi ina muda gani tangu iwe huru? na kupa MBA inachukua miaka 40 NAYO AU?
 
Dr.WHO,
kama nimemuelewa vizuri Mswahili yeye kazungumzia matatizo yaliyoletwa na hawa jamaa wawili Msoffe na Lauwo ktk utoaji wa ajira wao. Binafsi kulingana na maelezo ya mswahili kusema kweli ingebidi nimtazame vizuri huyu Msoffe pia kuipitia board nzima ya ajira TRA. Huko juu hakuna taabu kabisa matatizo yanaanzia hapa kwa sababu ya kuwepo mtu anaye practice Ukabila.

Wanachojaribu akina mwanakijiji kusema hapa ni kama vile samaki mmoja akioza basi kapu zima, kisha wanatumia mifano ya kuwa kama kuna samaki aliyeoza mbona mnakula?...mimi nasema huyo samaki aliyevunda lazima atolewe ktk kapu hao tunaowala hawajavunda bado!... jibu litarudi haiwezekani kabisa kapu kuwa na samaki wazuri na mmoja kavunda.
Hii ndiyo ngoma inayotembea kwa sababu Ukabila inachukuliwa kwa upana wa kitaifa badala ya kuangalia mtu ama kikundi fulani cha watu.
 
Mwanakijiji.

ina maana hata kabila lako nikutajie mimi?wewe ni mtu maarufu na mwandishi si vyema nikuanike sana. nitakutumia kwenye PM.

Mkandara.

naomba uwasaidie tena hawa waficha ukabila. shule ya Marian girls iko bagamoyo-mkoa wa pwani na hapo bagamoyo ni asilimia kubwa sana ni waislam na makabila ya pwani.

lakini katika vijana waliomaliza kidato cha nne hata cha sita hao waislam au wakwere/wazaramo hawafiki hata watano. tena toka nchi nzima hakuna waislam watano wala usiseme wenye bagamoyo wenyewe kama wapo.


au Nenda ST.Anthony pale mbagala jee kuna wazaramu wangapi wanasoma?au makongo wanaosoma ni watoto wa wanajeshi tu?

kwa hoja za kina Mwanakijiji na YEBO YEBO watasema bagamoyo waislam wamepiga hatua kwani wana shule na wanazidi kusoma.

Kifupi TRA kunatakiwa kumulikwa na hawa wanaopinga wengine ndio wakwepa kodi kwa kutumia ukabila.

nakupa mfano hai Reginald Mengi anadaiwa kodi na TRA zaidi ya billion 5 lakini kutokana na sera za ukabila nani atamshitaki? ukigeuka kuna Kittlya. Laowo, mmanda, salim yusuf, maleko.

Mwanakijiji

najua wewe ni msafiri kuna baadhi ya nchi hasa ulaya unaulizwa utaje wewe ni mtu gani mzungu, mhindi.mwafrika n.k hadi kwenye fomu za vyuo vikuu na wanakwambia tunachukua takwimu hizi ilikuona equal opportunity inachukua nafasi yake.hawa wenzetu wameshtuka, sisi tukisema tuanzishe utaratibu huo Mwanakijiji utakuja juu. na hili suala hata kiusalama wa nchi si zuri. leo jeshini wawe wakurya watupu na itokee professor Sarungi kagombea urais akashindwa ndani ya chama alichoombea halafu aamuwe kuingia msituni kwa kutumia influence ya mkoa wake kuwa na wanajeshi wengi kutakalika?

kwa kila nukta iwe ukabila utafutiwe neno kujuana bado ni jambo baya na la kukemewa sio kufumbiwa macho na kulibatiza majina mengine.

fuatilia Nigeria waliiachia suala hilo leo linawaumiza vichwa.

narua tena Tanzania ya sasa tuna wasomi wengi toka makabila yote, hadi kalani atoke moshi ndio TRA ifanye kazi?

mwaka jana kulitokea nafasi za kazi Hazina zilkuwa 600 na application zaidi ya elfu kumi tena makabila mbalimbali na hata sasa kuna nafasi zingine zimetoa fuatilia kama wanaomba wachagga tu.

pia uliza nafasi 13 zilizotangazwa na mambo ya nje tizama walijaza wangapi? na waliochukuliwa ni kina nani?

na hata miji ya mwanzo kuwa na shule ni Tanga kama wasomi basi wangekuwa waTANGA au hamjui kama wajerumani walianza Tanga?
uliza mkuu wa mwanzoCHUO CHA MZUMBE alikuwa mchagga?ni familia ya mwapachu.
 
"Kweli TRA ina watumishi wengi katika nafasi nyeti ambao ni Wachaga, lakini hili ni suala la historia, huwezi kulikwepa, kumbuka Wachanga ni kabila ambalo watu wake walipata elimu ya juu mapema kabla ya watu wa makabila mengine'.

Mwanakijiji hayo juu ni maelekezo ya MMANDA anakiri kuna wachagga wengi tena sehemu nyeti. sikuelewi unavyopinga na kusema nikuletee orodha ya wachagga ina maana kama unapinga na kuona nazua.

hata heading ya habari MManda anatetea wengi wa wachagga TRA hakupinga na hilo gazeti ni la phillimon mikael lilijaribu kuweka mambo sawa.

mwanakijiji kuendelea kupinga tu nitakuwasikulewi wenye TRA yao wanakiri. na justification kuwa hata madaktari ni wachagga kwa hiyo tukubali tu. au tukashangae jeshini.
 

give me a break! Wakristu wangapi wana mke mmoja lakini wana watoto wengine pembeni? Yaani kuwa na mke zaidi ya mmoja = population kubwa! Nipe ushahidi mzee, Kila mwanamke ana watoto wangapi? Je kila Muislamu mwenye mke zaidi ya mmoja ana watoto kwa wastani wangapi? Nipe data mwanangu!!! mkono mtupu haulambwi!

I can see.. mnataka kutoka kwenye ukabila mkajifiche kwenye udini.. go ahead make my day!! Kokote mtakojificha nuru ya ukweli itaangazwa na huko!!

Wazeee MMJ na Yebo2,

Kwa mantiki yenu hapo juu, ina maana kwamba kabila lenye wananchi wengi ndilo liruhusiwe kutawala mashirika ya umma na serikali au?

hata kidogo!! hayo sasa ni maneno yako na wala huwezi kupata hoja hizo toka kwangu, mimi si mkabila! Kama ningesema hivyo Wasukuma basi ndio wangetakiwa kuwa katika nafasi nyingi. Mzee ES kwanini Wasukuma hawako kwenye nafasi nyingi za juu wakati wao ndio makabila makubwa zaidi nchini? Kuna tatizo gani eneo hilo la watu wa mwanza, shinganya, na tabora? Makabila yenye watu wengi waliosoma ndio watakuwa wengi katika nafasi za kazi na ajira period. Na itaonekana hivyo zaidi kama makabila hayo pia yana watu wengi kiidadi!!! Kama Wanyakyusa wako karibu milioni moja na wengi waliosoma ni kama laki tatu, wakati Wagogo nao wako kama milioni moja lakini waliosoma ni laki moja.. hivi sehemu za kazi zitaonekanaje? Ni nyinyi mnaokwepa hoja zilizowazi kwa kutulazimisha tuone ukabila mahali ambapo haupo!

Sasa tukiiikubali sera ya majimbo itakuwaje? au ndio maana kumbe ndugu zetu wanaililia sana hiyo sera, yaani ni kwa sababu wao ni wengi kuliko makabila mengine?

Hilo la majimbo mnajuana nyinyi wenyewe miye simo.. lakini anayetaka majimbo ana kila sababu ya kujenga hoja kwanini na wale wasiotaka wajenge hoja kwanini, hoja bora na ishinde!

Na wenzetu UN wanaolalamika na Mama Tibaijuka kuajiri Wahaya wengi huko mnaionaje hiyo, au nayo ni Wahaya wengi mno duniani kuliko makabila mengine duniani?

Anajuana nao?

Mzee ES na Mkandara!

Suala la TRA na hivyo vitengo vingine nimeshalizungumza na nitarudia.

a. Ni kesi ya kujuana zaidi au ni ukabila?
b. Hakuna ushahidi wa kutosha kuniambia TRA yote imetawaliwa na Wachagga. Of course, I can pick any department in any part of the country and prove that a certain tribe is dominant! Kesi ya TRA mnaweza kabisa kunishawishi endapo (i) mtanipa composition ya vitengo vyote, mikoa yote, na idara zote (ii) mtanithibitisha kuwa siyo kujuana kuliko wapatia watu hao nafasi (iii) waliopo hawana elimu ya kufanya shughuli hizo (kunipa mfano wa mtu mmoja katika idara ya wati mamia ni kuchezea akili zangu)!
c. Kama hoja ni vitengo vichache na siyo nchi nzima, tunaweza tukakaa na kuzungumza hilo, ila kudai Tanzania kuna TATIZO LA UKABILA nakataa na nitaendelea kukataa hadi ushahidi wa kisayansi unithibitishie vinginevyo!

Mkandara, je Wahindi ni idadi gani katika Marekani? Kitakwimu watu wa asili ya Asia ni asilimia 4 tu ya watu wa Marekani. Hata hivyo, kwa sensa ya 2000 wanaongoza Marekani kwa kuwa na shahada ya kwanza (44%) wakifuatiwa na Weupe (26%), Weusi (14%). Kwanini lakini Watu wa Asia wanaonekana katika mahospitali mengi, na nafasi nyingi za kitaalamu wakati wao ni asilimia ndogo ya population? Wanaongoza kwa kipato kuliko hata watu weupe! Nenda kwenye vyuo uone jinsi gani watu wenye Asili ya Asia walivyojazana! Kwanini watu weusi ambao ni karibu asilimia 13 ya population hawaonekani?

Kama idadi ndogo ya watu waliosoma inaweza kuwa na impact kubwa kwenye taifa kubwa kama la Marekani, itakuwaje pale ambapo idadi kubwa ya watu waliosoma toka kwenye makabila makubwa itakuwa kwenye sehemu mbalimbali? Nakuhakikishia kuwa kama Warangi wangekuwa wamesoma zaidi enzi zile, nisingeshangaa kuwakuta wengi TRA, kama Wafipa ndio wangekuwa wamebobea katika mambo ya biashara na elimu ya biashara nisingeshtuka kukuta kumi au ishirini wako kwenye kitengo kimoja!!!

Aliyosema Mmanda siyo msahafu, suala la kuwa na wachagga wengi kwenye nafasi "nyeti" laweza kuwa issue. Lakini sijasoma aliposema kuwa kuna "wachagga peke yao" kwenye nafasi nyeti.

Labda nirudie tena, hakuna hata mahali pamoja ambapo nimezungumzia "nani anastahili na nani hastahili" kupata nafasi yoyote. Yule mwenye uwezo na elimu ya kufanya kazi fulani apewe nafasi hiyo na kama anaifanya kazi hiyo kwa uadilifu. Kama kuna Wazigua ishirini na wote ni mahiri katika utafiti wa kilimo, nitafurahi sitashangaa nikiwakuta wanafanya kazi Uyole au pale Sokoine!! it just make sense! Kama kuna watu walioajiriwa TRA ambao hawana ujuzi, uzoefu na umahiri katika nafasi walizopewa watajeni na mkianza hivyo isiwe kwa kuchagua "wachagga kwanza" tuangalie makabila yote TRA na tuulize nani yuko competent na nani mwenye elimu! Huwezi kuondoa idadi ya watu wa makabila fulani kwa kuchagua makabila mengine!! Kama ni merits basi iwe merits across the board, na tukifanya hivyo na kukuta bado tunaajiri Wahaya, Wachagga, na Wanyakyusa wengi tufanye nini tena?

Pendekezo langu:

Kwa vile tatizo lenu ni idadi ya wachagga na makabila mengine sehemu mlizozitaja, napendekeza kuwa (kwa sababu nyinyi wenyewe hamtaki kupendekeza).

a. Kusitisha mara moja ajira za wachagga, wahaya, wanyakyusa katika ofisi hizo.

b. Kabla Mhaya, Mnyakyusa, Mchagga hajakubaliwa kuajiriwa huko aulizwe kwanza mtu wa kabila jingine kwanza.

c. Tufanye uhakiki wa Wachagga wote TRA na kuuliza vyeti na elimu yao tusiulize kama wanajuana na mabosi (kwani hilo siyo la msingi). Wachagga wote ambao haturidhiki na elimu, na uzoefu wao basi watemwe.

d. Tukishamaliza TRA, tuhamie idara nyingine zote ambazo zinawachagga wengi na tufanye hivyo hivyo.

e. Tukimaliza serikali tutagundua kuwa bado hata katika jamii yetu bado Wachagga wana nafasi kubwa, wanabiashara nyingi n.k Hii inawanyima nafasi watu wengine wengi hivyo tujaribu kwa namna yoyote ile kupunguza kumiliki kwao biashara. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuwanyima vibali vya biashara hadi tutoe nafasi hiyo kwa watu wa makabila mengine kwanza.

f. Bila ya shaka kuna wachagga (Wahaya na Wanyakyusa pia) kwenye vyuo vyetu vingi, tuwaombe ndugu zetu hao waamue kwa angalau miaka mitano kusimamisha masomo ili nafasi zao zichukuliwe na makabila mengine ili nao waaelimike. Hii itaonesha ni jinsi gani ndugu zetu wameamua kupigana na tatizo la ukabila.

g. Hata hivyo baada ya kufanya hayo yote hawa jamaa wanaweza kuanzisha shule zao wenyewe na vyuo vyao na hivyo bado wakaendelea kuelimika, hatuna budi tutafute jinsi ya kupunguza uzao wao. Kwa mfano tunaweza kuwapangia kuwa Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa wasizae zaidi ya watoto 4 na wakati huo huo tuwatie moyo watu wa pwani waoe wake wengi na kuzaa watoto wengi kwani nafasi za Elimu ziko nyingi na wazi.

h. Tukiona bado Wahaya, Wanyakyusa na Wachagga bado wako wengi na wanaendelea kuonekana kwenye vitengo mbalimbali tunaweza kuwatafutia sehemu nyingine Afrika (kama Botswana au Namibia) ambako tunaweza kuwasihi wahamie ili kutengeneza nafasi kwa watu wa makabila madogo madogo. Tunaweza kutumia fedha za madini kuwalipia tiketi.


Haya nimewapa na suluhusisho la ukabila mnaouona nyinyi.
 
Mzee Mwanakijiji,
Hilo la kwanza umelivamia!... Alivyosema mswahili alikuwa akijibu hoja zenu za kutazama population kama ndio ratio ya wasomi nchini. Kama maelezo yenu yana ukweli basi waislaam watakuwa wengi pia kuliko wakristu kwa sababu wao huoa wake wengi na possibility ya wao kuwa na watoto wengi ni kubwa!...Haaa haa haa!.. sijui kama umeelewa hapo.

Now, maadam umekubali kuwa hili sio kweli basi achana na hizo hesabu za population kupima elimu kwa sababu hazina ukweli.
Hayo mengine ni maneno yako wewe mwenyewe ambayo unataka kuyaingiza ktk ndimi za watu. Ukiambiwa hukuchana nywele haina maana wewe mchafu ama wewe mbaya - ugly!.. kachane nywele imekwisha.
 

Hakuna mahali nilipopima population mimi.. nilikuwa naonesha ukweli fulani. Nitaurudia:

a. Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa siyo makabila makubwa zaidi Wasukuma na Wanyamwezi ndio wengi zaidi

b. Haiwezekani makabila yenye watu wachache ambao wamesoma zaidi kulinganan na makabila yenye watu wengi ambao nao wamesoma. Ukisomesha Wakwere wote bado hawawafikii ukisomesha nusu ya Wanyakyusa wote! So, wingi wa watu wa makabila hayo siyo tu kwa sababu ya elimu bali pia wingi wao.

c. Kama makabila yote yamesoma sana tangu 70s (kama ulivyosema) iweje Wasukuma, Wagogo, na Wanyamwezi wasiwe wengi zaidi wakati walikuwa na nafasi sawa?

That was my point
 
Mzee Mwanakijiji,
Je, Unajua kama kipengele chako cha kwanza A kinapingana na kile cha pili B?. maandishi yako mwenyewe. Kwa maana hiyo inaonyesha wazi wasukuma lazima wawe wengi wasomi kuliko wanyakyusa! kisha unakataa kwa sentesi ya kwanza!
Kisha hiyo C umesema huna data za kusema Wasukuma, Wagogo wengi hawakusoma ama wamesoma!.. sielewi maswali yako yanalenga wapi.
 
Sehemu ya kwanza ni sehemu ya maswali na hiyo sehemu ya mwisho ni siyo maswali ni mapendekezo ya jinsi ya kuondoa tatizo la idadi ya wachagga wengi TRA na ofisi nyingine nyeti... Chagueni mnayoona yanafaa.
 
Sasa unachozungumza ni nini hasa ikiwa cha kwanza na cha pili vinagongana... sielewi?
Umeuliza swali kisha ukapendekeza kitu kinachopingana na swali mimi nikujibu nini? Kumbuka umesema unaonyesha UKWELI fulani.
 
Mzeee MMJ,

Wasukuma na wanyamwezi, na watu wa Magharibi kuacha Wahaya,huwa wako very sensitive, ndio maana hata Mwalimu alipokuwa madarakani aliwaweka watu wa kwao sehemu nyeti tu, je can you imagine rais akiwa Mchagga?

Je unaijua kazi ya Mama BM, jinsi alivyowajaza jamaaa, na ku-steeer kila charity group toka majuu kuelekea hukooooooo!

Data unazoziweka ni nzuri kidarasa, lakini sio ku-justify kabila moja kuwa wengi kuliko mengine katika shughuli za kikazi, na hata maelezo ya MManda kule nyuma ni absolutely pure NONESENSE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…