Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mimi nilikuwa sijui kama usemalo ni kweli. Muhimu zaidi GANGA yajayo kusudi makabila yote yajazane ofisini.
 
sioni tatizo kwa wachaqgga kua na nafasi nyingi maofisini ukweli ni kwamba hata uende vyuoni wachaga ni wengi ii inaonyesha kua wanasoma na kwa sasa wachaga katika vyuo vya elimu ya juu wanawazidi hata wahaya katika nafasi ya pili, wanyakyusa wa tatu na watu wa kanda ya ziwa wa nne uo ndio ukweli!

kwa iyo wao wanajali sana elimu hasa wazazi wa kichaga wanpeleka wattoto wao shule makini kwa garama yoyote ile na iyo ni rasha rasha tu kwa idadi yao katika vyuo vya elimu ya juu hali itakua ngumu sana kwa makabila mengine huko mbeleni hasahasa wenzetu wa pwani watalia sana faulo play ila ukweli ndio uo.

mimi binafsi si wa makabila hayo ila na wa admire hasa wazazi wao jinsi walivyo willing kwenda extra mile ku fund elimu za watoto wao na pia wanakua wana akili binafsi mwaka niliomaliza pale mlimani walikua wengi sana na walikua wanauwezo mzuri huwezi watuhumu kua wako pale kwa upendeleo
 

nimecheka basi,tubanane nao tuu na tukaze musuli tutafika

tena wewe thibitisha 1.makampuni ya BIA almost yote top officers utacheka.

ila nilipo mboni hawako kiivo wamejaza akina nanihii waleeee wengine wale
kila kilicho juu kilianzia chini!!
 

asante sana umejibu hili kwa ufasaha!!
tuko njiani na karibia tunafika
 
Jamani Jamani Jamani ! Nadhani inabidi tukumbushane tulipotoka.

Back in Memory Lane............(Nyerere's Voice)

"Vinchi vidogo, vidogo hivi .. ...,
Vya watu 27 million.....,
Tunazungumza Makabila ! (silence and uproar)...,
Tunazungumza lugha ya Makabila !...
Mtuingize katika karne ya 21, Mnapanda basi la Makabila !.."

Youtube clip :

B.P 2010
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka jitihada alizofanya baba yangu mzazi kutupatia elimu ktk family yetu naelewa sasa wengi wanachosema kuwa wazee wa kichaga wanathamini sana elimu. Ilimgharimu kula mchicha chukuchuku angalau wanawe wafike F4. Aliuza ng'ombe, miti, alikopa fedha wanawe wasome. Baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali tz nimegundua kuwa hii spirit ni adimu sana sana kwa makabila mengine.

Nilipokuwa Versity nilishangaa jinsi ambavyo wachaga walikuwa wanawapeleka puta wenzao watokao makabila mengine. Kwanza, tulipoingia 1st yr, zile kozi za computer wao waliona kama kumfundisha mwanafunzi wa F4 kuhesabu a, e, i, o, u. Ndugu zao, wajomba, shangazi, wazazi wao wana mwanga wa elimu tayari, wengine wana computer nyumbani hata zaidi ya moja. Wakati wewe unajifunza kushika mouse mwenzako yuko mbaaaali kweli kweli.

Swala si kusoma tu darasani na kuwa na cheti, exposure ina nafasi kubwa sana sana. Kama dada yangu ni mhasibu, ni rahisi kunishawishi nisome uhasibu, kwani anafahamu mtandao wa kupata kazi. Huwezi kulinganisha na jamaa ya Mwanafunzi ambaye yeye ndiye msomi kwenye familia yao na hakupata ushauri nasaha kabla ya kuchagua kozi ya kusoma. Kuwa na mtandao ni kitu muhimu sana haswa ktk dunia hii ya utandawazi. Swala si upendeleo tu, ingawa siwezi kupinga moja kwa moja kuwa upo, bali kuwa na taarifa sahihi hilo nalo ni jambo la msingi sana.

Kabla ya kusema kuna upendeleo fanya uchunguzi kwanza ya mazingira yote yanayoruhusu kabila moja liwe dominance.
 
ETI NINI...? MNASEMA WAMESOMA...? NA WANASIFA KUWAZIDI WENGINE......?
haya majajiji wa JF AMUENI....! CHIEF WA TANROADS AITWAYE MREMA......! ANA SIFA STAHILI....?
 
NGOOJA NGOOJA! FANYA UTAFITI. MREMA SI MCHAGGA. Mnashangaa? Ni mtu wa Arusha. Fanyeni utafiti tafadhali.
ETI NINI...? MNASEMA WAMESOMA...? NA WANASIFA KUWAZIDI WENGINE......?
haya majajiji wa JF AMUENI....! CHIEF WA TANROADS AITWAYE MREMA......! ANA SIFA STAHILI....?
 
Hawa wachagga ndio waliotufikisha hapa tulipo wachoyo,wapenda mali kuliko uzalendo hawa ndio walio pewa mashirika wakayazika mbele za uso wetu angalia walipokuja kushika tanesco,Bima,Benki ya Taifa,Mbuga za wanyama,Uvuvi,misitu,madini,kilimo hawafai kabisa kusogezwa mahari popote ndio walio wengi katika nafasi za TRA unaona mwenyewe misamaha ya kodi inavyo jitokeza ndio wezi wakuu wa viwanja vya wazi wachafuzi wakubwa wa mazingira makontena mijini biashara za barabarani mioto na uchafu mwingi mwingi ni wao ni sawa na mafia hawa
 
Benk ya crdb mwanza waliifilisi wao sasa pesa za epa zote zilipita crdb wakati benki zinazoongozwa na wazungu walikataa pesa hizo hawafai wachaga kabisa katika vyanzo vya fedha
 
tatizo siyo wachaga nk...tatizo ni mtu kutokuwepo kwenye mtandao unaoongoza nchi. kwa bahati hao ndg wamefanikiwa kuwa katika mtandao wa viongozi na ndg zao. kwa mfano mashirika mengi yamejaa watoto wa wakubwa kwa kigezo hicho cha kusoma. ukweli ni kwamba kuna tabaka la wakubwa na vizazi vyao ndio watakaopata kazi nzuri mpaka atakapotokea nabii fulani kutuokoa. meanwhile tuendelee kuvumilia tu au uchukue chako mapema.
 
Kuwepo au kutokuwepo kwa Ukabila kunatoka na mwamko wa Elimu katika mikoa Tajwa......Chukua mfano mdogo K'Njaro kuna VYUO VIKUU vifuatavyo 1.Muccobs 2.Mwenge 3.Kcmc 4. Masoka na Vyo vya ualimu vya kutosha tu mabavyo ukivijumlisha unapata idadi inakua less or Equal na shule za SEKONDARI mkoa wa KIGOMA....Huko huko atokako kaka yangu mbunge Machachari ZK.....Sasa hapo tutegemee nini??????
 

Bima ilijaa Wanyakyusa ilipokuwa inaongozwa na Nsekela na Mwaikambo. Matatizo ya Bima yalianza miaka hiyo. Kwahiyo usiwalaumu Wachaga.

Pia kuhusu hawa Wanyakyusa, tunazungumzia kabila gani? Tunazungumzia pia Waluguru na Wapogoro ambao ni ndugu zao? Wanyakyusa walitoka Morogoro na nimesikia kwamba wengi wao hata leo kule Rungwe na Mbeya wanajiita Walugulu. Wengine wanasema ni Wapogolo (nimeambiwa hakuna herufi ya "r" katika lugha ya Kinyakyusa). Lakini pia wanajiita Wanyakyusa ingawa wanasema ni Walugulu na Wapogolo. Ebu nifafanulie hapa. Hata leo kuna Wanyakyusa wengi sehemu za Morogoro ingawa wengi wao walihamia kusini magharibi sehemu za Rungwe na Malawi labda karne nyingi zilzopita.
 
Nilikuwa sijachangia hii topic ingawa nimeiona siku nyingi. Ni kweli wachaga wamesoma lakini ukabila wanaufanya pale penye maslahi, mfano vyeo na nafasi nyingine, hili liko wazi zaidi na hili lilifikia kileleni enzi kwenye utawala wa Mkapa.

Na kama wasingefanya, nobody would have noticed them given ukubwa na nchi hii na makabila yalivyokuwa mengi na diversity na balancing Mwalimu aliyoifanya hasa kwa kusomesha kila kabila bila ubaguzi.

Lakini pia, kila utawala nchi hii, ukiondoa awamu ya kwanza, unakuja na upuuzi wake wa kibaguzi, kwa mfano, awamu ya sasa ni uislamu, hata vibonde kibao wanapata kazi nyeti zinazohitaji umahiri na utendaji demanding kwa misingi ya udini..

HII NDIYO REGIME TULIYOMO, lakini je tutendelea hivyo mpaka lini. Wote hao wana-take advantage ya makabila madogo kama la kwangu na mengine makubwa ambayo hayakubahatika kupelekewa shule za wamisionari. Now, is that Tanzania we need, ndivyo Mwalimu alikuwa akifanya? Tunachezea shilingi ******, ndicho ninachokiona..it may not last forever.

Kila tunapo-deviate kwenye misingi ya Mwalimu, i see a potential danger. Tusidhani sisi ni invicible wa machafuko, nono..ni suala la muda, this country may be up in flames before we know it! Let's not open pandora's box as we will pay dearly! Kina Rwanda na wengine tunaowacheka, inaweza kuwa zamu yao kutucheka!
 


Baelezeeeeeeee MM, nami kesho ntabaelezeapo
 
Mwanakijiji asante sana kwa maelezo yako marefu, mazuri na yenye kusisimua, but kwa kiasi fulani hapo niko kinyume kidogo na wewe kwa jinsi unavyojaribi kupinga kwa nguvu zote kuwa hakuna ukabila. Ukabila upo kwenye taasisi nyingi za serikali na unakuwa tena kwa kasi ya ajabu tukatae au tukubali lakini huo ndiyo ukweli.

Nakubaliana na wewe kuwa hayo makabila matatu ndiyo yaliyotangula kwenda shule na kuelimika, lakini kwa sasa kuna makabila mengi hata wazaramo wengi wameenda shule na kuelimika vizuri, lakini kilichopo sasa hivi ni kuwa haya makabila matatu kwa kuwa walitangulia kwenda shule na kushika nafasi nyingi kubwa na nyeti, imekuwa ni rahisi sana kwao kuwavuta wakwao hata kama wanasifa pungufu kuliko makabila mengine. Hiyo yote ni kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka ya kuajiri pia.

Mwanakijiji wewe uko marekani japo kuwa uko karibu sana na media za bongo na kufanya utafiti mwingi but yanayoendelea ndani ya hizo taasisi sidhani kama unayafahamu kiundani zaidi. Nashauri tuache ushabiki bali twende na ukweli halisi.
 

asante kwa nukuu hizo hata asiyelewa akisoma nukuu za mwalimu zinajitosheleza. Tukisema enzi za mwalimu haaaaaaaaaa haziishi.
 

Tupieni jicho na Tume ya Mawasiliano.
:smile-big:
 
Swali alilouliza Mwanakijiji bado halijajibiwa.

Ni kweli au ni uongo, Hakuna jibu la hili swali, so far!

Ila maoni yangu ni kwamba kama kuna wanaoona kwamba ni tatizo, na kwamba limewaathiri kwa kiasi fulani, wajitokeze, kwa sababu na vigezo na vielelezo ...; Mahakamani, vyombo vya habari .....

Nasema UWAZI, UWAZI UWAZI tu ndo unaweza kukomesha vitendo vya ubaguzi kama vipo na kuwafanya wanao-propagate hayo waone aibu. Siyo vya ukabila tu bali hata vya udini, jinsia, rangi, maumbile, - anything up-professional , (toa vielelezo) n. k.

Isije ikawa wapo wanaotaka awepo mtu wao ili "na sisi tule", au na sisi ni zamu yetu n. k.

Nafikiri kuna tabia pia ya kutojiamini na uwezo mdogo wa ku-network kati yetu WaTZ across mipaka hiyo ya kikabila na kidini n.k. Labda kwa sababu wengine tumekulia vijijini na inakuwa vigumu kuwazoea watu uliokutana nao ukubwani. Kwa wale waliozaliwa na kukulia mijini, hili swala la boundaries litakuwa dogo sana, unless kama wazazi wali-propagate huo upuuzi. Leo tunaona watu wanaoana across makabila, watoto wanaotokana nao watakuwa ni WaTZ tu!

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…