Ukabila, udini, maji na mazingira.

Ukabila, udini, maji na mazingira.

kasinge

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2011
Posts
1,259
Reaction score
319
Habari za majukimu ya kujenga Tanzania Imara.
Mchango wangu kuhusu katiba ijayo.
1. Kwa kuwa viongozi wetu wameshindwa kukemea suala la ukabira na udini, ninaona kuna haja ya kuvipa kipaumbele katika katiba ijayo. Mwalimu alijaribu kutuchanganya makabila mbalimbali shuleni hasa zile za boarding, na tulikuwa tukiishi pamoja na kwa upendo hadi tunapoanza kazi baada ya kuhitimu. Kwa sasa suala la ukabila na udini vinashika kasi. Nyinyi kama wadau wa sheria, mnaweza kuangalia jinsi ya kuliweka kikatiba ili tusiendelee kugawanyika. Ni sensitive kwangu kiasi cha kustahili kuingia kwenye katiba sababu tuna ushahidi wa nchi jirani zilivoathirika na ukabira pamoja na udini. Kiwekwe kifungu kumbana mtu yeyote anaebainika kueneza ukabila na udini.
2. Kwa kuwa maji na mazingira ni nyeti na vimewekewa sheria ndogondogo ambazo ni dhahiri watu walio wengi wamezikiuka na kuharibu vyanzo vya maji na mazingira makusudi, na kwa sababu tunavitegemesa sana vitu hivi, naona ni muhimu kuingizwa katika sheria mama. Ningefurahi kama mchango huu ungepeta nafasi kujadiliwa kwa kina na kitaalamu zaidi.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom