Ukaguzi wa magari: Vimulimuli, Ving'ora, Chesesi namba na Sportlight

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Wiki ya nenda kwa usalama imeanza katika baadhi ya mikoa, ambapo itaambata na ukaguzi wa vyombo vya moto pikipiki, gari ndogo na kubwa na baada ya ukaguzi mmiliki analipia stika (pikipiki) Sh 1,000.00 (gari ndogo) Sh 3,000.00 (gari kubwa) Sh 5,000.00

Ombi langu kwa mamlaka husika katika ukaguzi huo madereva na wamiliki wa vyombo vya moto, watakaofika kwenye ukaguzi na wasiofika wapewe elimu juu uwekaji vimulimuli, chesesi, sportligh na ngao madhara yanayoweza kupatikana na sheria ya usajili wa vyombo vya moto inatamkaje.

Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo vya moto karibuni (kama mwaka mmoja) kujiamilia kuweka vimulimuli kwenye dashbodi kwandani kuelekea nje kwenye kioo cha mbele, ( rangi nyekundu na bluu) kama magari ya misafara ya viongozi.
 
Utopolo mtupu. Wanakagua nini kwa ujuzi upi kama si kukusanya tozo tu?
 
Sio kama tunaharibu biashara, pia hao wenye kufanyabiashara ya kuuza vimulimuli waorodheshwe wa watambulike. Ikumbukwe miaka ya nyuma kulishamiri magari makubwa na mabasi ya kwenda mikoani walikuwa wanaweka kwenye magari yao vile vinavyofanana na magari ya wagonjwa (ambulance) na ya kuzima moto ( fire & rescue)

Baada ya kulalamikiwa sana ikabidi Waziri mwenye dhamana atoe tamko kuanzia wauzaji, mafundi, wamiliki na madereva atakaeonekana anauza, anaweka, au gari lenye kimulimuli afikishwe mahakamani, hapo ndio ukawa mwisho wa uvunjaji wa sheria.
 
Kwani hivyo vimulimuli viliingilia wapi? Serikali ikachukua kodi kwanza? Halafu ndiyo ikaenda kuwazuia wasiuze na walionunua wasitumie?

Huu si ndiyo wizi wenyewe wa kutumia nguvu?
 
Back
Top Bottom