Ukaguzi wa mahesabu vilabu Vikuu

Ukaguzi wa mahesabu vilabu Vikuu

wajibisha

Member
Joined
May 16, 2021
Posts
90
Reaction score
215
Habari za asubuhi wakuu.

Hivi kwa nini mkaguzi mkuu wa mahesabu ya Serekali (CAG) akagui mapato na matumizi ya vilabu vya soka hapa nchini hasa vile vyenye maslahi ya umma kama Simba, Yanga, Mbeya City na kadhalika.

Ni haki ya mashabiki wa mpira kujua vilabu vyao vinaingiza mapato kiasi gani na matumizi ya mapato hayo.

Bado kuna usiri mkubwa kwenye uendeshwaji wa vilabu hivi na kwa bahati mbaya sana mashabiki wengi wamejikita kwenye kushangilia viwanjani wakisahau msingi mkubwa wa matokeo ya uwanjani ni pamoja na jinsi vilabu vinavyoendeshwa kifedha.

Pia suala la uwelewa kwa mashabiki wengi inaweza kuwa ni sababu nyingine kwa nini kuna usiri mkubwa wa kuweka wazi mapato na matumizi.

Karibu tujadili.
 
Back
Top Bottom