SoC02 Ukahaba na ukuzaji wa pato la Taifa

SoC02 Ukahaba na ukuzaji wa pato la Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

MWANAHARAMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
4,041
Reaction score
10,699
Nani asiyefahamu hii ni moja ya biashara kongwe duniani ambayo imeshindwa kufutika toka dahari.
Karne mpaka karne mamlaka mbalimbali duniani zilijaribu kuitokomeza aina hii ya biashara ila zikaambulia patupu, hivyo kufanya ishamiri licha ya marufuku ya serikari mbal;imbali ulimwenguni.

Tanzania ikiwa ni moja ya Nchi ulimwenguni haikuachwa na kadhia hii, licha ya mahubiri ya Viongozi wa dini, Wazee wa Mila na desturi hadi viongozi wa serikari kuasa, ila hii biashra haikuzizima bali kushamiri.

Biashara hii kwa sababu inafanywa kwa uficho basi huchochea maambukizi ya magonjwa mbali mbali, hasa ya Zinaa. mfano Ukimwi, Kaswende ,Gonorea, Pangusa na mengineyo bila kusahau homa ya ini inavyosambaa kupitia hii biashara.

Kuongezeka kwa matumizi ya intaneti na kuibuka kwa social media imechangia biashara hii kwenda kidijitali hivyo kupata wigo mpana zaidi kati ya watoa huduma na wateja wao kiasi kwamba serikari imekosa udhibiti wa kuitawala ikiwemo kuiangamiza kabisa biashara hii haramu.

Wapo wanaofanya hadharani yaani ni maeneo ambayo yanajulikana na hakuna udhibiti wowote na jamii kwa sasa unaichukulia kama sio kosa, hivyo kuja na lugha ya kupunguza makali wenyewe wanaita kudanga.

Kwa sasa karibia kila mji Tanzania una maeneo wanayo jiuza: kwa uchache ukiyataja ni:

DAR ES SALAAM maeno kama Mwananyamala, Uwanja wa fisi, Kigamboni, Riverside, Tandika, Mbagala,Gongo la Mboto, Temeke kwa sokota, Temeke Sudan, Sinza, Posta, Chamazi kwa kuyataja kwa ufupi.

MPANDA: Uwanja wa fisi

SIMIYU: Sweet corner

MBEYA:Mafiati na maeneo yote ya starehe

Hivyo kijamii imerasimishwa kama jambo lisilo na ubaya wowote na huu ndio ukweli mchungu ila madhara yapo pale pale.


NINI KIFANYIKE?

Hatuwezi kupambana na biashara hii, kwa njia zile za kizamani, maana bila shaka zimeonyesha haziwezi kumaliza au kupunguza ukubwa wa shughuli hii.

Hivyo nilikuwa napendekeza hatua zifuatazo zifuatwe ili kupunguza tatizo hili:

(1) KURASIMISHA
Ndio inabidi irasimishwe ili kuondoa sintofahamu na serikari kushindwa kujua ukubwa wa shughuli hii,yaani watoa huduma wawe wanasajiriwa na kutambulika na Mamlaka ikiwemo kupimwa na kujua hali zao kiafya.


(2) KUPEWA LESENI ya MUDA MAALUMU. KWA KULIPA KIWANGO CHA PESA.
Wapewe leseni tu kwa wale watakao thibitika wapo vizuri kiafya hivyo hawatoweza kusambaza magonjwa na watajilinda wao wenyewe wasiambukizwe, kumbuka sasa haitofanywa kinyemera.


(3) KUKAGULIWA AFYA ZAO MARA KWA MARA.

Ndo tukiri kwamba wale tu watakao fuzu vipimo vya afya pekee, wataruhusiwa kuendelea na biashara yao maana hali ya sasa ni holela.


(4) KUTENGWA KWA MAENEO MAALUMU KWENYE KILA MJI/JIJI NDANI YA TANZANIA

Ipite sheria ambayo itadhibiti holela iliyopo sasa hivi, kwamba makazi ya watu ambako kuna watoto, hivi vitendo vinaendelea kufanyika kiasi kwamba unawaathiri watoto kwenye makuzi yao ambao ndio Taifa la kesho.

Mfano: Pattaya huko Thailand.

(5) KODI MAALUMU KWENYE HII BIASHARA.

Ndio duniani hakuna biashara itakayo fanyika bila ya kukatwa kodi na serikari hivyo itawalazimu wapange bei wakijua kila muamala utakatwa kodi na serikari ilisimamie hilo.

Mji mdogo wa Bariadi una wanao jiuza wanawake zaidi ya 200. Kila mmoja akilipa kodi ya shilingi 100,000 nchi itaingiza kiasi gani.


(6) ZIPIGWE MARUFUKU HUDUMA ZA MASSAGE, SALUNI KUTOA HUDUMA HII MPAKA ZIWE NDANI YA ENEO TENGWA

(7)ELIMU IZIDI KUTOLEWA JUU YA ATHALI AZPATAZO MWANAMKE AKIFANYA BIASHARA HII.


Faida nyingine kuongezeka kwa utalii kwenye maeneo hasa ya ufukweni. Nchi ya Gambia hii ni sekta kubwa katika kuingiza pato la Taifa na fedha za kigeni
 
Upvote 0
Back
Top Bottom