GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nilishaona hilo likifanyika nilipokuwa mdogo. Jirani yetu aliyekunywa sumu alinyweshwa mkojo wa binadamu kwa ajili ya kumtapisha.
Miaka mingi baadaye, nikiwa nimeshahitumu Chuo, tukio kama hilo lilitokea tena jirani na kwetu. Binti mmoja alikunywa sumu, na kabla ya kukimbizwa hospitalini, alinyweshwa mkojo wa binadamu na kisha kutapishwa.
Sikufikiri kama na mimi ningekuja kuliunga mkono hilo wazo. Hata sikujua kama nilikuwa ninaamini kwamba mkojo unaweza kutumika kama "dawa". Lakini unapokuwa katika dharura, ndipo kile unachokiamini huweza kuthihirika. Aliye vitani katika mazingira ya hatari hachagui silaha.
Miaka ya 2000, nilikuwa nikifanya kazi katika shule fulani mikoani "huko".
Siku moja, wakati wa mapumziko, wanafunzi walinifuata na kuniambia mwenzao wa kiume kanywa sumu bwenini! Nilifuatana nao hadi bwenini alimokuwa huyo mwanafunzi.
Nilipofika na kumkuta amelala sakafuni haongei, nilipatwa na taharuki. Haraka niliwaambia wambebe, nikakimbia nao hadi kwenye gari na kumwambia dereva atukimbize hospitalini.
Nakumbuka nilikuwepo mimi, dereva na wanafunzi kadhaa wa kiume.
Ndipo wazo la mkojo liliponijia. Lakini nilipowaambia wanafunzi niliokuwa nao wampe mwenzao msaada wa mkojo, ni kama vile hakuna aliyenielewa. Nikarudia tena kuwaelesha, kuwa mmoja wao amkojolee kinywani kwa sababu mkojo utamfanya atapike, lakini hawakunitii japo si kawaida yao.
Nilipokosa ushirikiano wao, niliamua kuachana na hilo wazo. Lakini njiani tulinunua maziwa freshi na kumnywesha.
Tulimfikisha hospitalini na alipata huduma, na kesho yake aliruhusiwa.
Ilikuwa kila nikilikumbuka hilo najikuta nacheka. Sikujua kuwa na mimi nilikuwa ninaamini katika kutumia mkojo kama dawa ya kupunguza makali ya sumu.
Nilijikuta ninawaza
1. Kama hao wanafunzi wangetii, na katika harakati za kumnywesha mkojo kwa kutumia viungo vyao(hatukuwa na chombo cha kukingia mkojo), na ikatokea akang'atwa na anyenyweshwa mkojo, ingekuwaje?
2. Tungefika hospitalini na kuwaambia kuwa tulimnywesha mkojo, ningeelewekaje?
3. Wanafunzi wenzake wasingemkejeli baada ya kupona?
Ingawa mwanzoni niliwakasirikia hao wanafunzi, baada ya kutulia, nilijikuta nashukuru kwa kutokutii kwao!
1. Waliniepusha na sintofahamu ambayo ingeibuka!
2. Walimwepusha mwenzao kunywa mkojo wa binadamu!
Ingawa sina uhakika kama kweli mkojo wa binadamu ni tiba ya mtu aliyekunywa sumu, lakini nafurahi kwa kutokutii kwa hao wanafunzi.
Na cha kumshukuru Mungu zaidi ni kuwa ingawa huyo mwanafunzi hakunyweshwa mkojo, aliweza kupata huduma hospitalini na kesho yake kuruhusiwa.