CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
Mwaka 1879 Malkia aliyekuwa anaiongoza Ufaransa Bi Marie Antoniette aliambiwa wananchi wake hawana Mikate akajibu kwa kifaransa “Qu’ils mangent de la brioche” kwa maana ya kiingereza “Let them eat cake" kwa kiswahili kisicho rasmi Sana ni kuwa Waambie wale Keki.
Inatajwa kuwa Brioche waliyoambiwa wale kilikuwa Chakula Cha matajiri Sana Ufaransa, ambacho kwa walalahoi wa Ufaransa walikuwa hawawezi kukinunua ndio maana walikuwa wanahitaji mikate. Baada ya kauli ile Kutoka Malkia alipinduliwa na wananchi wenye hasira Kali.
Leo naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bi Stella Manyanya ameambiwa Sukari imepanda Bei na kufikia shilingi 3000 kwa kilo Moja yeye akajibu watu watumie asali. Kitu ambacho Manyanya hajui ni kuwa asali Ni ghali kuliko Sukari na asali kwa Sasa Ni Chakula Cha matajiri.
Lita Moja tu ya asali ni shilingi 10,000 sawa na kilo tatu za Sukari za mlalahoi. Manyanya yeye kununua hata ndoo ya Asali si big issue kipato kinaruhusu. Nafikiria familia ya watu watano pale kijijini ambao kipato cha Kaya Ni shilingi elfu 3 kwa siku au chini ya hapo wanaweza kununua lita Moja ya Asali? Je, wataitumia siku ngapi?
Asali siku hizi ni anasa kubwa Sana kwa watu Manyanya asitutukane. Najiuliza je, asali inafaa kutumika kwenye kuoka Mikate? Kwenye utengenezaji wa vinywaji huku kijijini? Kwenye maandazi tutaweka asali?
Ni kweli kuwa Manyanya hawezi kutengeneza Mbinu za Sukari kushuka Bei? Yaani akili yake imeshindwa kumnasua mlalahoi wa Tanzania ambaye Chai ndio kinywaji chake Cha kifahari? Sasa tunamlipa mshara na kumpa V8 la Nini Kama hata Jambo dogo hivi anashindwa kulitatua?
Akili kubwa ni Mali ya Rais, ndio wanaotakiwa kumzunguka Rais hawa ndio akili kubwa ya Tanzania ambayo inatakiwa kuhudumia watanzania?
Albert Einstein aliwahi kusema "We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them" huyu jamaa alikuwa na akili sana yaani akili iliyotengeneza tatizo haiwezekani ikatatua tatizo hilo.
Tunawaza kidogo sana Manyanya aangalie hata wenzetu huko njee wanafanyaje hasa katika kipindi hiki Cha Korona.