Serikali Imechukua Hatua Au Ina Mpango Gani Kukabiliana Na Janga Ja Ukame Na Njaa Kali Mwaka Huu?

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Nimetembea karibia mikoa yote Tanzania,hali ni ile ile,ukosefu wa mvua.

Mikoa yenye mvua za wastani nchini ni Dar,Kigoma,Kagera,pamoja na Lukwa,kingine ni tia maji tia maji tu.

Kwa upande wa kilimo cha mpunga wakulima wameandika hamna. Mahindi ni kwa wale waliowahi kulima,ila wale wenzangu na mimi wameambulia patupu,mazao yamekaushwa na jua kali,hata kama ukiwasha moto shambani, moto unawaka vizuri tu.hakuna matumaini kabisa.

Kuna dada yangu alikuwa Katavi akahamia Luhogi Morogoro kwa ajiri ya kilimo sasa amehama tena kutokana na jua kali,ameenda Mpanda kulima angalau maharage mwishoni mwa msimu huu. Hali ni mbaya sana

Kutokana na hali hii Tanzania inakabiliwa na njaa kali sana huku ukame utazisakama jamii nyingi ambazo hazina maji ya bomba na zitathirika pakubwa,

Wakuu,inatubidi tujipange mapema,tuhifadhi akiba ya chakula kwani tunakoelekea sihitaji kusimulia.

Sudan,Ethiopia,Elitrea,na kwingineko tunajua hupigwa na majanga ya ukame na njaa,sasa ni zamu yetu

Tujipange.
 
Wakuu,
Mwaka huu sote tunafahamu kuwa hakuna mvua za kutosha, ambapo wakulima hasa wanaotegemea msimu wa kilimo wa muua wamefeli pakubwa

Mazao ya chakula hasa mahindi na mpunga hayakustawi na badala yake mazao yamekaushwa na jua kali kabla hata kukomaa

Karibia nchi nzima hali ni moja,ukame,kutokana na hali hii uwepo wa chakula cha kutosha nchini unatia mashaka,hali hii itapelekea mfumuko wa bei za mazao hasa mahindi hivyo wananchi wa kawaida kushindwa kumudu gharama,wengi tutawapoteza

Serikali yetu sikivu ya awamu ya sita,tunaiomba iweke mikakati mathubuti ili kulinda chakula tulichonacho,ikiwezekana mipaka ifungwe,kusiwepo na utokaji wa mazao kwenda nje ya nchi.

Karibuni wadau.
 
Imejiandaa kugawa kofia na tshirts na mabango ya mitano tena.
 
Ngoja kwanza tumuombee Mama ili ashinde kwa kishindo uchaguzi wa mwaka huu, ndipo tutakuja kuiombea Mvua inyeshe.
 
Angalau kwa mikoa ya nyanda za juu kusini kama Mbeya ,Rukwa na Songwe kwa mazao ya mahindi watabatua .Ila changomoto ambayo itafanya bei ya za zao hili kuwa juu ni nchi majirani kama Zambia na Malawi nao walikumbwa na ukosefu wa mvua msimu ulio pita hivyo licha ya kwamba wanatarajia kuwa na mavuno , watakuwa wakijaza maghala yao ya taifa,hivyo watafunga mipaka kitu ambacho kitafanya muhindi uwe dhahabu msimu huu .
 
Serikali haicheki na wowote. Inajipanga na uchaguzi. Maana kila sehemu mitano tena.
Ukilia njaa na kiu utaambiwa mitano tena
 
Utauza bila kuvuna,stupid
stupid mwenyewe.
Matatizo ya kukaa sehemu 1 ulipozaliwa hadi unafia hapo. Hujui misimu ya kilimo inatofautiana kanda na kanda.

msimu wa kilimo cha mwezi 10 mwaka jana watu tunavuna mahindi tangu mwezi 2 hadi sasa.
 
Nimezurura sana ndani na nie ya nchi
 
Wakuu,
Mwaka huu sote tunafahamu kuwa hakuna mvua za kutosha, ambapo wakulima hasa wanaotegemea msimu wa kilimo wa muua wamefeli pakubwa

Mazao ya chakula hasa mahindi na mpunga hayakustawi na badala yake mazao yamekaushwa na jua kali kabla hata kukomaa

Karibia nchi nzima hali ni moja,ukame,kutokana na hali hii uwepo wa chakula cha kutosha nchini unatia mashaka,hali hii itapelekea mfumuko wa bei za mazao hasa mahindi hivyo wananchi wa kawaida kushindwa kumudu gharama,wengi tutawapoteza

Serikali yetu sikivu ya awamu ya sita,tunaiomba iweke mikakati mathubuti ili kulinda chakula tulichonacho,ikiwezekana mipaka ifungwe,kusiwepo na utokaji wa mazao kwenda nje ya nchi.

Karibuni wadau.
Wajinga kama nyinyi ni tatizo kubwa ndani ya nchii hii,hivi aliye kwambia mkulima anashinda juani na kwenye mvua akilima ili kukurahisishia maisha ww na familia yako ni nani?
Mwenye jukumu la kukurahisishia maisha yako ni serikali yako uanayo ilipa kodi na si wakulima,mkulima analima mazao kwa ajili ya manufaa yake na familia yake.
Unacho takiwa kuishauri serikali ni inunue mazao kutoka kwa wakulima kwa bei nzuri alafu hayo mazao wayasambaze kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo kwa bei nafuu.
Na sio kuishauri serikali ianze kuwaingilia wakulima na kuanza kuwapangia bei na sehemu ya kuuzia mazao yao ambayo hawakuwahi kuwasaidia kuyalima.
Huu ujinga wa kuingilia biashara za mazao aliufanya magufuri akasababisha mazao yaozee mashambani kwa kukosa wanunuzi.
Mnataka vijana waachane kubet na kuendesha badaboda badala yake
wajiajili kwenye kilimo alafu wakati huo mnataka gunia la mahindi liuzwe 30,000 hata hamjui mnataka nini.
 
Back
Top Bottom