Ukame wa kutisha Jimbo la Califonia nchini Marekani na cha kujifunza

Ukame wa kutisha Jimbo la Califonia nchini Marekani na cha kujifunza

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Najiuliza endapo ukame ulio ikumba Califonia ukitokea huku kwetu itakuwaje? Make kuna Ukame wa kufa mtu ambao haujawahi tokea Calfonia na kila kitu kimesimama na hakuna kinacho fanyika

CaliforniaDroughtFolsom.jpg

california-drought-before-after.jpg

California-Drought-before-and-after-pics-04-685x886.jpg

Kwa Tanzania inabidi kuchukua hatua make nahisi ikitokea huku hakuna jiwe litakalo salia, juu ya jiwe jingine,
 
Mimi ni miongoni mwa wanaharakati wa mazingira tanzania ambaye najihusisha na swala la utunzaji mazingira.............jamani kiukweli na sisi tunaelekea hukohuko.........tazamia mikoa kama Kilimanjaro Dar inavyochosha kwa joto kali.........hii ni kutokana na ongezeko la watu linalochangia uharibifu wa mazingira kwa kasi ya ajabu!
Mkoa kama mbeya wakati huu wa joto.......ukiwa kule ni burudani tupu......unatembea huku umevaa sweater hata koti maana hali ya hewa ipo moderated na uoto uliolizunguka eneo zima........lakini sasa mkoa kama Kilimanjaro......Dar......Morogoro ni hapakaliki kutokana na joto kali kupita kiwango.........wahusika wamekaa na matumbo yao utadhani koba la kinyozi kwenye maofisi yenye viyoyozi wakijitoa ufahamu kuhusu yanayojiri huko nje..........pumbavu sana nakerwa sana na hili swala naomba MUNGU anipe nafasi na uwezo zaidi nipambane na hili janga ..........!
 
Ukitaka ujue jinsi East Africa tunavyoungua, pia angalia Congo rainforest inavyopungua kulinganisha na Amazon.

DroughtRisk_Daily.png
 
njia pekee ya kuzuia haya ni kuhakikisha gas na umeme vinashuka bei ili watu waache kutumia kuni na mkaa. hilo likitokea tutakufa kama wadudu maana kilimo chetu ni duni sana.
 
Kukabiliana nayote nilazima tubadilishe mfumo wa io ngozi wa Nchi yetu kutoka utawala bora hadi Kuwa na uonhozi bora Kwa kuifuta Kabisa CCM 2015
 
njia pekee ya kuzuia haya ni kuhakikisha gas na umeme vinashuka bei ili watu waache kutumia kuni na mkaa. hilo likitokea tutakufa kama wadudu maana kilimo chetu ni duni sana.
Hili litawezekana kama wapiga deal, watakubali, Ama sivyo tutaendelea kuona gesi ni kwa wneye unafuu kidogo
 
Tuweke sheria kali kuhusu ukataji miti.
Tupande miti mingi sehemu ya makazi yetu na iwe sheria kuwa ukiwa na sehemu yakuishi hakikisha uwe na miti isiyopungua kumi
 
Ni ukweli ila ukama kama huu wa Califonia tusiombe utokee huku make naamini litakuwa ni moja kati ya majanga mabaya kabisa na huko wenyewe haijawahi tokea ndo kwa mara ya kwanza, na hata Kenya wame experience ukame ingawa si wa kiwango hiki,
 
Wataalam elezeni kwanza kilichotokea huko, walichokosea ni nini hasa kwenye inchi iliyoendelea kama hii! Tukue kosa ndiyo tutajifunza jinsi ya kujikinga
 
njia pekee ya kuzuia haya ni kuhakikisha gas na umeme vinashuka bei ili watu waache kutumia kuni na mkaa. hilo likitokea tutakufa kama wadudu maana kilimo chetu ni duni sana.

Kukabiliana nayote nilazima tubadilishe mfumo wa io ngozi wa Nchi yetu kutoka utawala bora hadi Kuwa na uonhozi bora Kwa kuifuta Kabisa CCM 2015

Niko pamoja na ninyi wadau wangu......mpo sahihi sana............kiukweli hii serikali ya viongozi wenye vichwa mabuyu.......hatutafika popote tusipowatoa kwenye uongozi.........
 
Mijitu imekaa tu ofosini haifanyi chochote ni kusubiria posho na udokozi tu........shenzi taipu.................
 
Najiuliza endapo ukame ulio ikumba Califonia ukitokea huku kwetu itakuwaje? Make kuna Ukame wa kufa mtu ambao haujawahi tokea Calfonia na kila kitu kimesimama na hakuna kinacho fanyika

CaliforniaDroughtFolsom.jpg

california-drought-before-after.jpg

California-Drought-before-and-after-pics-04-685x886.jpg

Kwa Tanzania inabidi kuchukua hatua make nahisi ikitokea huku hakuna jiwe litakalo salia, juu ya jiwe jingine,

Umelinganisha kichuguu na mlima kilimanjaro? Ni kweli hapa California kuna ukame lakini mazao yanaiva na shughuli zote zinaendelea kwa sababu ya nchi yenyewe imeshaendelea! Mbali na chakula cha mashambani lakini nchi hii inatumia processed food kilichomo madukani kwa wingi ikiwamo jimbo la CA.

Wenzetu wanamipango ya muda mrefu ya kila kitu na wengi wao wana fight kwa ajili ya miaka ijayo na ndiyo maana chakula tunachokula hapa siyo cha shambani jana. Kinachoiva leo kitatumika miaka mingi ijayo. Huko kwetu kila mtu anatamani ale mafanikio yake leoleo kabla hajaingia kaburini na ndo maana hakuna cha mipango ya muda mrefu. Kukitokea ukame leo wa miaka miwili tu, tunafanana na South Sudan.

Mahindi leo yanaozea Rukwa, Iringa na Mbeya bila hatua yoyote. Watu wanakula escrow account na kuangalia kutoa rushwa katika uchaguzi sembuse kujiandaa kwa majanga.
 
Back
Top Bottom