UKARA Kisiwa cha Tanzania kilichobadili Uhumi wa Dunia kimfumo

UKARA Kisiwa cha Tanzania kilichobadili Uhumi wa Dunia kimfumo

chijin

Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
5
Reaction score
2
UKARA KISIWA CHA TANZANIA KILICHOBADILI uchumi wa dunia kimfumo .

JUNE 20, 1920
Gazeti maarufu la marekani lijulikanalo kama The New York Times( NYT) lilichapisha habari kuhusu kisiwa cha ukara (bukara) habari hii iliwavutia wasomaji wengi duniani kutokana na Akili wqliyokuwa nayo ukilinganisha na kudharaulika kwa watu weusi wakati ule.Akielezea kuhusu ukara mwandishi alisema "wakara hawana vitabu kuhusu siasa ya uchumi lakini wanaishi kufuatana na nyendo za wazee wao wa zamani wakitumia kila zao la ardhi yao bila kupoteza punje wala kipande cha jani hakikupotea bila kazi katika ardhi ya ukara".Mwandishi wa the NYT kuonesha maajabu ya taarifa hiyo alisema "ukara haiko Asia Bali iko afrika ni kisiwa chenye watu 19000 na maili za mraba 36 nikisiwa tu cha watu weusi kabisa na wabaya kuliko wote duniani lakini vizazi hadi vizazi walikuwa wakipambana na mbweha siyo binadamu na vita ya kukuza uchumi wao ilikuwa haikomi" .

Kipindi hicho mataifa mengi yalikuwa yakipigana vita ili kupata mahala pa kuishi ,kuinua uchumi na tawala zao lakini Dr.H.LYNDHURST DUKE alisitajabishwa na kukutana na kisiwa kilichokuwa kikijitawala bila msaada wa Mzungu huku kukiwa na idadi kubwa ya wakazi waliokadiliwa kuwa 19,000.kabla ya kuja wageni wakara walifanya maajabu mengi ambayo inchi nyingi duniani wamejaribu kwa udogo nakujinufaisha kiuchumi ;

1.wakara
Waliweza kulinda ongezeko la watu bila njia za kisasa jambo ambalo limeigwa kuleta uzazi wa mpango japo hawakufanikiwa kama walivyo fanikiwa wakara ikumbukwe inakadiliwa kuwa 1/5 ya population ya Tanganyika ilipatikana ukara ,wakara walihamisha familia kutafuta makazi sehemu zingine za milki yao bila kusahau kisiwa chao tamaduni zao za kiuchumi na kulikuwa na njia thabiti zilizoepusha uzao wa mapacha jambo lililoifanya jamii hiyo kuwa na idadi ya watu takribani 16000 kwa karne nyingi.

ukara ilikuwa alama ya utawala bora usiyo na mabavu wala uimla duniani japo haki za wanawake kumiliki ardhi haikutiliwa maanani.

2; Pamoja na kilimo walipotaka kuinua uchumi wao vijana walienda kuvua samaki maeneo ya mbali na kuijenga ukara yao, mfumo huu ulikuwa wa uwekezaji inje ya ukara na kujenga ndani ya ukara.
Baada ya makoloni kujitawala mataifa makubwa yalirejea historia ya ukara wakaja na hoja ya uwekezaji na ubinafisishaji.

,walichunguza namna wakara walivyoweza kujitawala kiuchumi kwa kutumia watu binafsi .

3;Ukara lilikuwa eneo la kwanza afrika kuandikwa kama eneo linalotumia njia zilizoendelea katika kilimo.lakini walitumia mbolea ya samadi na majani huku wakibeba ndoo kichwani.
kila ardhi ilikuwa na mmiliki na mtemi wao alimiliki kiasi fulani. kila mti ulikuwa na mtu hakuna aliethubutu kuokota jani la mti wa mtu lakini kila mwenye mti alihakikisha jani lake linatumika kwa chakula cha mifugo ya ukara ili kuzalisha mbolea .wandishi wanakili kuwa neno wizi halikuwepo katika lugha ya wakara hao.

4; Ikiwa katika mfumo huo wakiuchumi ukara haikuwahi kukumbwa na njaa ukame,vita wala janga lolote inaelezwa kuwa kulikuwa na bustani nzuri kwa mtemi wao huku ukara kwa ujumla ikizungukwa na hewa safi. Mtemi alifanya kazi katika masuala nyeti na utoaji adhabu hakuwahi kujenga Barabara lakini zilikuwepo hakuwahi kukopesha Bali uchumi ulikua hawakuwahi kuomba msaada ,urafiki wao ulikuwa ni wakibiashara na ulirisishwa kizazi hadi kizazi watemi wa ukelewe na ukara walipendana sana hapo mwanzo maana kulikuwa na usawa katika urafiki wa kiuchumi.

kiufupi kila mara matatizo ya uchumi yalipojitokeza duniani wachumi wengi walipendekeza wasomi kurejea katika historia ya bukara. Wageni waliifurahia bukara wakaiga tamaduni za kiuchumi za wakara na kuwapa za kwao Natamani nifike ukara siku moja kabla sijafa nione baada ya ujio wa wageni Leo ukara ikoje . ukipewa kuupa jina mfumo wa uchumi wa ukara uuite "the origin of economic ideology "wachumi wetu muishauri serikali kuirejea historia hii muhimu huku kila mwanainchi akihakikisha hakuna jani litakalo potea katika mti wake wala neno litakalo potea katika kinywa cha mtanzania bila kuinufaisha Tanzania .
Wenye akili walisema ukiujenga uchumi wa inchi kama ukara ilivyojengwa shida hadi ianzishwe na wanainchi wenyewe kwa kuichoka shibe nakuijaribu njaa kuichoka amani na kuijaribu vurugu kuichoka misingi yao ya utawala na kuitamani ya wageni .

Mungu ibariki tz
 

Attachments

  • 1477891163565.jpg
    1477891163565.jpg
    44.6 KB · Views: 115
Mkuu, wazungu walikuja ili wachukue rasilimali. Kutimiza lengo lao hilo ni lazima wakutawale kimtizamo na kimfumo.
Ili kufanikisha hilo ni ilikuwa ni lazima wavunje utaratibu wote walioukuta (hata kama ulikuwa mzuri kiasi gani) na kuweka wa kwao ili azma yao ikamilike. Hiyo haikuwa kwa Bukara tu, hata sasa ndivyo tunavyotawaliwa kifkra na hao watu toka nje ya Afrika.
 
umesahau uchawi .....na uganga.

wakara ni wataalam.wa madawa ya kienyeji.

kila wakoloni wakipanga kwenda hapo kwa shughuli zao,au kipindi kile kukamata watumwa,walikuwa hawakioni kisiwa,au kinahama,kwa hiyo watakuwa wanakiona kiko mbali wanaongeza spidi wee hawafiki,

pia wana utaalam wa kutumia mamba,wakara wanakutumia mamba,wanakuseti unasogea mwenyewe ziwani,mamba anakukamata,anakupeleka,
 
Wakara, nasikia mwalimu Nyerere aliwalazimisha kulipa Pamba, wakapewa mbegu na serikali wakapewa amri kila mtu lazima alime pamba. WALICHOKIFANYA WALIKAANGA ZILE MBEGU ZA PAMBA THEN WAKAZIPANDA, matokeo yake hazikuota na serikali iliwaacha kama walivyo walime wanachokitaka
 
Ni hadithi nzuri....ila ni kiongozi mmoja tu Afrika aliyethubutu na kuweza kufanya yale ya wana BUKARA katika nchi ya jangwa na akafanikiwa....kiongozi MUAMMAR GHADAFI.....mpaka pale wananchi wake walipoikinai SHIBE....R.I.P.....
 
Back
Top Bottom