Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Amani iwe nanyi wapendwa.

Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.

Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Rais Magufuli amewataka wanasiasa hao kuviachia vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi wake bila kuingiliwa na mtu yoyote na amewashauri kama wana ushahidi wowote wasubiri watuhumiwa wa ajali hii wakifikishwa mahakamani wataenda kusema ushahidi wao huko badala ya sasa kupiga porojo za kisiasa ambazo zinaweza kuharibu ushahidi.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.

Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .

Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote kwa waliopatwa na ajali hii!!!

Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..
 
Kuna mtu hapo juu amesema mwanzisha uzi una dna za kijani

Nimecheka sana looh
 
Sawasaw
 
UPUUZI.
 
Mkuu wa nchi yuko sawa mno
 
Wewe ni certified bwege.
 
Pole Tanzania, pole wafiwa, pole majeruhi - MUNGU awape pumziko la milele waliopoteza maisha

Lkn awape faraja waljopoteza ndg, jamaa, rafiki. Kipindi hiki tushirikiane kuomboleza na kuwasitili kwa heshima nyingi marehemu wetu.

R. I. P fellow Tanzanians
 
Upo sahahi sana mzee, nchi hii siasa za majitaka ndo zinapewa kipaumbele. Hili swala la kivuko kibovu na watu kutumia mitumbwi inaonekana mbunge alishatoa malalamiko yake muda mrefu lakini watu hawajali ndo wanaanza kucheza midundiko kwenye chaguzi za marudio. Mindege ambayo haina tija kwa hao wanaoita wananchi wanyonge imenunuliwa kwa kasi ya kimbuga bila kuwepo mijadala ya kueleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…