Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Haya ndio Mazito ???
 
Amenunuliwa huyu. Hata, haiwezekani aseme hivyo.
 
Huyu jamaa ataitwa msaliti very soon.
 
Halafu huyu mtu asili yake ni Ukerewe sasa aliacha na akaona ni vyema watu aliokua nao wengine wakubwa kidogo kwake wengine wadogo kbsa kwake wateketee tu
 
Daah pole sana mkuu...najua umetumia ujasiri mkubwa kuweza kuandika hivi ijapokuwa upo majonzini.....msamehe mleta mada!!!
 
Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao.......

mimi John Kisekwa..."
 
Mkuu inawezekana kuzama kabisa nchi kavu kama ilivyotokea! mimi kidogo nimewahi kuwa dereva wa mitumbwi ziwani! injini ikiwa inatembea au chombo kikiwakinatembea kule mbele kwenye mtumbwi kunainuka kwa sababu ya mkandamizo wa injini/propela zilizoko nyuma. kwa hiyo wakati meri ikiwa inatembea inaweza isiwerahisi kuzama kwa sababu ya mzigo uliokombele! lakini kunauwezekano mkubwa wa chombo kuzama kama ukipunguza mwendo gafla na kukawa na mzigo mzito kwa mbele! mimi naamini kwa 80%. inaweza kuwa ni sababu iliyopelekea chombo kile kuzama!! Mzigo ulikimbilia mbele wakati injini tayari ilikuwaimepunguzwa mwendo gafla!
 
Vipaumbele ndo tatizo..tutapata tabu sana kwakweli..
Nchi hii ni ubatili mtupu. Hii haitofautiani na Mama yuko nyumbani anajifanya yuko busy na kufua nguo, huku mwanae katumbukia kwenye sufuria la chakula likiwa jikoni likichemka na kupelekea mtoto kufariki. Sasa huyo mama mtamuona kuwa ana akili? ndo uongozi wetu ulivyo, watu hawawajibiki wako kujikweza tu ningeona la maana nchi ingekuwa na mipango thabiti ya maisha ya watu badala ya kutafuta misifa isiyo na tija
 
Hapo kwa nahodha bado kuna utata, mara anashikiliwa na jeshi la police mara amefariki yupo chini....sasa ipi sahihi??. Watulie hadi mwisho na kama hawamjui nahodha bado wafunge vinywa vyao tu
Nahodha aliyefariki ni Deiwaka tu(alipewa aendeshe ingawa hausiki na uendeshaji wa Mv nyerere).Nahodha ambaye ndo alitakiwa kusafiri na chombo ndo huyo ameshikiliwa na polisi kwa kosa la kumuachia Deiwaka aendeshe.
 
Na mbunge wao pia aongea;

 

Huwa kwenye investigation tunaangalia chanzo kikuu kilicholeta tatizo na kusababisha maafa.
Load capacity ya chombo ni 25tons, designer hatujui ameweka factor of safety kiasi gani hii huwa ni siri ya manufacturer.
Unataka kuniambia kivuko kikibeba 25tons na hizo 25 tone zote zikakaa upande mmoja basi kivuko lazima kipinduke? hiyo tutaita poor design ndio chanzo cha tatizo... Kwenye design ya vyombo vya baharini hasa vinavyobeba abiria consideration huwa nyingi kwa ajili ya usalama wa watu, hivyo design ya hicho chombo kwa ajili ya usalama wa watu lazima iangalie vitu vingi ili ku countebalance every possibilities, Binadamu huwa ni mzigo unaotembea kwenye chombo kinapikuwa kinaelea ni kama tanker inayobeba mafuta au maji hivyo lazima ziwepo assumption kama hawa binadamu wameshift left wawe counterbalanced right na kama wameshift mbele wawe counterbalanced nyuma hizo ni factor za kawaida kwenye design..

Binafsi naweza sema tatizo ni overloading, 25tones ukaweka nyingine 20tones kwa mfano kufikia 45tons na tuchukulie ukawa umevuka hata factor of safety ya designer na manufacturer na hizo 45tones zikaenda upande mmoja let say mbele hakutakuwa kuwa na namna ya kucountebalance mind you design iko kwa ajili ya kucounterbalance 25tones + factor of safety (siri) na wewe umeload beyond all factors hapo manufacturer na designer watasema sorry..
 
Kuna haja ya kufanyia kazi vyombo vyote vya usafiri na miundombinu kwa ujumla ambavyo vina majina ya wanasiasa.
 
Mkuu sijaona sehemu amemshukia kama mwewe.Au ulikusudia tu kunogesha uzi
Mtoa mada ana viashiria vyote vya mwenye kichaa cha kurithi. Ana tabia ya kuandama mtu wakati wote kwa visababu vya kuokoteza. Pili hakuna tiba ya kawaida iwezayo kumsaidia. LAKINI akikubali kuliweka wazi tatizo lake anaweza KUOMBEWA, akapona akawa mtu mpya. Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…