Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Habari mbaya hizi jamani. Napiga picha pale Ukara, karibia kila familia wanamsiba, hakuna wa kwenda kumliwaza mwenzie!!!

Mimi mke wangu ni wa nansio ila kapoteza ndugu zake 4, kaka wawili na mke wa kaka na mwanaye mdogo. Sasa huko Ukara nadhani kila familia imeguswa, ni hatari kubwa sana kwa hao ndg zetu.
 
Ikiwa kila ufunguzi wa miradi, matamko bila kuhoji na sifa huwa zinamwendea mtu mmoja wa CCM , basi pia ktk majanga na ajali vivyo hivyo lawama / kuwajibika ziende huko huko.
 
Mmh unanikumbusha mkasa mmoja nilikuwepo, kuna siku nilikuwa natoka mombasa nakuja tz miaka ya 2000 mwanzoni barabara upande wa kenya kabla hazijatengenezwa zilikuwa nyembaba sana.

Tukiwa njiani tukakutana na lorry limeangukia bondeni ilikuwa na watu wanne, tukasimama ili twende kutoa msaada maana watu wawili walikufa na wawili walikuwa hai wamenasa, before hatujashuka kuna mkenya mmoja akawa anasema twendeni watapata msaada mnatuchelewesha tuna haraka! Alikuwa mkali sana lkn wengi wape bus lili park pemben tukashuka na yule mtata akaamua naye kushuka kule bondeni siyo mbali sana na barabara.

Huwezi amini lkn ndivyo ilivyokuwa mmoja kati ya walionasa alikuwa ndugu wa karibu kabisa na yule mtata alimtambua! Baada ya kuwasaidia kuwatoa yule mtata alibaki na ndugu yake kumrudisha hospital za mombasa maana ndo palikuwa karibu zaidi, nasi tukaendelea na safari, true story.
 
Unatenganisha vipi siasa na matukio ya kizembe kama haya iwapo kina watu wanapaswa kuwajibika?
Mkuu wa Mkoa awajibike
Waziri wa uchukuzi awajibike
Polisi wawajibike kwa uzembe
SUMATRA wawajibike
Kwani hii ndio ajali ya kwanza ya uzembe hadi watu wawajibike?!. MV Bukoba aliwajibika nani?. MV Spice Island amewajibika nani?.
Kifo cha Daudi Mwangosi, amewajibika nani?!. .
Kifo cha Akwiline amewajibika nani?!
Mpaka watu wangapi wafe ndipo watu wawajibike?.

Utamaduni wa kuwajibika, umekufa na Nyerere!,
Mimi ni muhanga wa uwajibikaji, wakati wa Nyerere, baba yangu, Mzee Andrew Mayalla, ndiye alikuwa RSO wa Mwanza, kuna mahabusu wawili, Masanja Makulla Mazengenuka na Issack Mwanamkoboku, walikufa mikonani mwa polisi katika mahojiano baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya vikogwe.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hasssan Mwinyi alijiuzulu!,
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mzena, alijiuzulu!,
Mkuu wa jeshi la Polisi, IGP, Pundugu alijiuzulu!.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alijiuzulu!
RSO wa Mwanza, RPC, RSO na OCD kwanza walistaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakafunguliwa mashitaka ya Kesi ya Mauaji Mwanza!.

Uwajibikaji ni enzi za Nyerere!.

Ingekuwa Nyerere yupo, hata mtu aliyeuza Nyumba za serikali kwa kuwagawia hata vimada wake, hadi kuuza nyumba za line police!, asingethubutu hata kuwaza kuchukua fomu!. Mtu amelitia taifa hasara ya kulipishwa fudia kibao kwa maamuzi tuu ya papara!.Mtu amenunua kivuko mtumba kwa mabilioni ya shilingi, halafu hakikufanya kazi! na bado has the audacity of running for the highest office!.

Kuwajibika kumekwenda na Nyerere, sasa ni zama za kupeana pole tuu!.

Poleni kwa yote!.

P.
 
Mimi nimefiwa Na school mate wangu Olevel Na mke wake Wameacha Watoto wao Wawili
 
unataka kusema chadema tunapinga hadi AJALI?
OK.ngoja tukae kimya.
AJALI KAPANGA MUNGU.TUSIPINGE.
 
Mimi pia sababu hiyo imenisikitisha sana! Lakini binafsi naamini hiyo imechangia ila si sababu kuu wasitudanganye. Chanzo kikuu aidha ni hiyo ya kuweka abiria wengi kupita uwezo wa kivuko, ama kuwe na sababu za kitaalam.

Nimekuwa nikisafiri kwa vivuko vya Nyamagana-Ukerewe mara kwa mara na mara zote huwa tunapokaribia kufika tunatoka nje na kusogea kwa mbele kwaajili ya kuwahi kushuka. Hivyo basi nina hakika hata kwenye kivuko hicho kulikuwa na utaratibu huo siku zote ila jana uzembe ulikuwepo tu.

Katika stori na hao mabaharia wa vivuko hivyo nilibaini walishaendekeza uzembe kiasi kwamba hata itokee hitilafu ya namna gani wao husema ni vigumu kuzama labda waamue wao! Kwakuwa hakuna hata ukaguzi wa maana wanaofanyiwa wamekuwa wakizidisha uzembe kila kukicha, kwa ninavyofahamu endapo isingetokea ajali jana kukiwa na watu 400+ si ajabu kesho tungesikia kivuko kimezama na watu 600+...

Kwakweli serikali haijarejesha nidhamu kazini, bali imeleta uoga uliopitiliza (nidhamu ya uoga) kwa watumishi katika baadhi tu ya kada. Kuna kada hazijawahi hata kutishiwa nyau.
 
Huo ni uzembe, usituletee ujinga wako hapa
Siamini kama wewe umefikia hatua ya kuniita mjinga, je kwa vigezo gani ulivyovitumia nakutambua ujinga wangu?? Je nini nilichokukosea hadi unite mjinga?? Heshima nikitu chenye thamani sana, sijapendezwa na kauli yako. Binafsi sijamlenga mtu wala kumshambulia mtu binafsi, naomba tuheshimiane tu, kama mada yangu imekuudhi, basi nakuomba msamaha, tafadhali Kidamwa tusivunjiane heshima.
 
As if kuwa ya kitaifa ni jambo la kuwafariji hao wafiwa….shame on them.
 
Mimi mke wangu ni wa nansio ila kapoteza ndugu zake 4, kaka wawili na mke wa kaka na mwanaye mdogo. Sasa huko Ukara nadhani kila familia imeguswa, ni hatari kubwa sana kwa hao ndg zetu.
Inasikitisha!
 
Ndo muanze kudai mnunuliwe meli na boti za uhakika.
Sio mnanunuliwa ndege mnashangilia.wakati wanaopanda wengine.
Nyie mnapanda boti chakavu.
Mkuu siyo tuu kudai meli na boti but watanzania sasa tujifunze kudai kila haki ya msingi badala ya kuwaachia tuu akina Mbowe, Lissu, Zitto and the likes....
 
Kwa hili serikali ilitakiwa iwajibishwe na wananchi
...kwani wamesikia watu hawana uwezo wa kuzika hao marehemu mpaka watoe msaada

Itasaidia mini angali uzembe wao ndio umechangia watu kupoteza maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…