Ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa wapamba moto

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya ziara Uwanja wa Benjamin Mkapa hivi Septemba 17, 2023 jijini Dar es salaam kujionea ukarabati wa uwanja huo ambao utatumika kwenye ufunguzi wa michuano ya African Football League Oktoba 20, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukarabati wa Uwanja huo Bw. Abel Shirima ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema taa za uwanja huo zote zimetolewa na hatua inayofuata ni kutandaza nyaya za umeme ili kufunga taa mpya za uwanja huo.

Ziara ya Katibu Mkuu huyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro aliyotoa hivi karibuni kutaka ukarabati wa uwanja huo ukamilike ifikapo Oktoba 15, 2023.
 

Attachments

  • IMG-20230918-WA0003.jpg
    63.2 KB · Views: 7
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya ziara Uwanja wa Benjamin Mkapa hivi
30bn zinaweza kujenga viwanja vya wastani vyenye kiwango cha CAF, viwanja sita mkoani, mbali mbali, kama kile kilichopo St Mary's kitende kilitumia $1.5m ambao ni sawa sawa na $3bn za kitanzania huo ulikua mwaka wa 2012, na sasa hivi kina hold michezo ya CAF, ila Tanzania hapana, wizi kwa wazawa ni too much, mimi hata wakipendekeza wizara zingine zipewe DP world waziendeshe kwa niamba na sapoti tu.
 
Kwahiyo hapo ukarabati umefika hatua gani yani asilima ngapi?

Mbona kama tuna ona watu wana nyoosha vidole, utofauti ata kwa picha hatuoni... uchakavu bado ni mkubwa sana

Labda tuwape Muda! Maana ata mchina aliyepewa tenda haonekani🤣🤣🤣 au hapo kuna nani sijui mshauri!?
 
Osha nendeni mkampige faini MKANDARASI anayejenga hapo LUPASO, aliruhusu vipi hawa Viongozi kuingia eneo la Ujenzi bila KOFIA NGUMU na REFLECTOR? Hiii ni kuhatarisha Maisha ya Viongozi. Aidha mje na Majibu kwamba hakuna Ujenzi unaoendelea au Mtwambie kampuni iliyopewa kazi ni makanjanja wasio na weledi kazini. Hali hii inaaashiria kwamba kazi inayofanyika haitakuwa na ufanisi. Over
 
BILIONI 30.

Hadi Leo.

1. Hakuna Rangi na urembo Nje ya Uwanja.

2. Hakujabadilishwa viti vya namba

3. Hakuna ELD SCREEN.

4. Hawajafumua Majani na kuweka underground Utilities lake Geiser.

Bomba za maji zinazonyeshea na kuanza kurusha maji wakati wa Mapumziko nk.

5. Bado Kuna Blonde la kutuamiaha maji Katikati BADALA ya muonuko WA kutiririsha maji ya Mvua.

TUTAENDELEA KUIBIWA HADI TUSEME PO
 
Kwanini wanasiasa wetu wanatoa muda wa kitu kukamilika badala ya wahusika au wataalamu wa hayo mambo
 
Hakuna ukarabati wa maana hapa, kimeandaliwa tu kipindi cha upigaji, hapa zitapigwa rangi tu na blaablaa watu wanavuta chao
 
Waboreshe ili mvua ikinyesha uwanja ubaki na ubora ule ule kama tunavyoona ulaya viwanja vyao vikinyeshewa mvua na sio mvua kidogo tu uwanja unakuwa wa hovyo mara maji kutuama , kuteleza n.k
 
Cha ajabu kuna watu watakuja hapa kuponda hata hili.
Siyo kuponda mkuu, sasa hapo anatoa maelekezo ya nini?
Angalau tungeona hard hats, wachina etc ... la sivyo nahisi kuna ubadhirifu fulani unaendelea maana hautjui nini kinakarabatiwa na hawajaweka wazi hata tenda haipo wazi.
Yeye siyo mhandisi na hakuna mhandisi hapo, sasa anafanya nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…