Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ya kuanza ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ziara ya kujipanga kutekeleza maagizo hayo, Machi 5, 2023 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Saidi Yakubu amesema ukarabati huo utaanza mara baada ya mshauri mwelekezi kukamilisha kazi yake.
"Ukarabati huu utakua na awamu tatu, ya kwanza itakua ni ukarabati katika maeneo ya kubadilishia nguo, maliwato, kurekebisha viti vilivyoharibika, kuongeza taa ndani ya uwanja na maeneo mengine, kubarabati mfumo wa umeme na maji pamoja na eneo la waandishi wa habari ambapo tutawahamisha wanapokaa hivi sasa na kuwatengea eneo zuri zaidi" amesema Katibu Mkuu Yakubu.
Awamu ya pili itakua ni ukarabati mkubwa ambao utatekelezwa na wakandarasi wa kimataifa na utahusisha eneo la kuchezea ( pitch) kupanua sehemu ya watu mashuhuri, kuweka televisheni kubwa yenye muonekano ang'aavu.
Katibu Mkuu Yakubu ameongeza kuwa awamu ya tatu itahusisha kupanua uwanja pamoja na kujenga viwanja vingine vidogo ikiwemo vya kuogelea katika eneo lililobaki, kuweka viti vya kisasa, kutenga eneo la kupumzika watu mashuhuri na kuufanya uwe kivutio kwa jiji la Dar es Salaam.
Ukarabati huo utafanyika chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kama mshauri mwelekezi.