Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa wafikia asilimia 95

Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa wafikia asilimia 95

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Ukarabati wa Awamu ya Kwanza unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 95 na asilimia tano zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo.

Akikagua ukarabati huo leo Oktoba 9, 2023, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema tayari vyumba vinne vya wachezaji, sehemu ya kuchezea, vyumba vya waamuzi, afya na eneo la video za marejeo (VAR) umekamilika.

" Tayari taa za kisasa 320 za mfumo wa LED zimefungwa na kuna huduma ya mtandao wa bure kabisa kwa ajili ya watazamaji wa mechi ambao tutauzindua kati ya tarehe 17 hadi 19 mwezi huu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa African Football League kati ya Timu ya Simba na Al Alhy ya nchini Misri tarehe 20,2023 " amesema Mhe. Ndumbaro.

Ameongeza kuwa, katika eneo la watu mashuhuri na sehemu ya wandishi wa Habari kazi iliyobakia ni ndogo ambayo itamalizika ndani ya siku hizo tano akiongeza kuwa mfumo wa sauti uwanjani tayari umerekebishwa.

Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Kampuni ya Formula 360, itafunga mfumo wa matangazo kidijitali ambao utaanza kufanya kazi rasmi Oktoba 20, 2023 huku akisistiza kuwa baada ya mchezo huo, ukarabati mkubwa wa awamu ya pili utaendelea.
IMG-20231009-WA0057.jpg
IMG-20231009-WA0058.jpg
IMG-20231009-WA0062.jpg
IMG-20231009-WA0061.jpg
IMG-20231009-WA0060.jpg
IMG-20231009-WA0059.jpg
 
Wameweka na viti vya namba au bado ni mwendo wa kuuza tiketi nyingi kuliko uwezo wa uwanja
 
HAO ni WEZI tu kwa sababu ZIFUATAZO...

1. Hadi sasa hakuna ELD screen za Matangazo.

2. Hakuna viti vipya na vyenye Namba kwaajili ya kuwa Directed na Tiketi yako sehemu ya kukaa.

3. Haojabadilishwa pich Wala kuweka zile underground utilities na Drainage system za KUTOLEWA maji wakati wa mvua.

4. Nje ya uwanja upande wa Uhuru uwanja Ni mchafu mno. Mvua zimeharibu kuta na Rangi .

5.Bado Vyooni Kuna shida,

5. waweke MIFUMO ya Camera kuzuia UHALIFU Nje na ndani ya Uwanja

IMETUMIKA UHUNI KUWAONGA HIYO INTERNET PAONEKANE PAMEFANYIKA JAMBO LA MAANA KUMBE NI UPUMBAFU MTUPU

Ni UHUNI
UHUNI.
UHUNI
 
BILIONI thelathini za kihuni.

Hakuna kinachofanyika.

Nelson Mandela Bay Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270 upo katika mji wa Port Elizabeth na unauwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake limetoka na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela
 
Huo uwanja kama ni matengenezo waliyofanya basi ni 15% ya eneo la uwanja wote...

Hiyo 95% wanayoitaja ni katika hizo 15% tu za uwanja wote...
 
Maelezo mbona yamejitosheleza awamu ya kwanza ya ukarabati yamefikia 95% bado awamu ya pili ya ukarabati mkubwa aijaanza sasa hizi lawama za tumepigwa zinatoka wapi? Au ni yale mazoeazoea ya kupingapinga kila kitu ndio yanatufanya kuwa hivi?
 
UTAPELI TU HAMNA CHOCHOTE VYOO BADO VINANUKA HADI NJE
 
Maelezo mbona yamejitosheleza awamu ya kwanza ya ukarabati yamefikia 95% bado awamu ya pili ya ukarabati mkubwa aijaanza sasa hizi lawama za tumepigwa zinatoka wapi? Au ni yale mazoeazoea ya kupingapinga kila kitu ndio yanatufanya kuwa hivi?

UKIONA MIMI NINEANDIKA KITU UJUE NI UHAKIKA KWA ASILIMIA ZOTE.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu
" amesema uwanja huo utafanyiwa 1.marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji,

2.chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo (UONGO)

3ubao wa kuonesha matokeo,

4.kuweka mfumo mpya wa TEHAMA.

5.kubadilisha eneo la kuchezea

6.na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

7.Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba,

8.mfumo wa umeme,

9. mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha,

10. chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa,

11.mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.
 
ANGALIA HAPA JINSI JAMAA YALIVYOKUA MAONGO NA MAJIZI.

'Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo'.

SELIKALI NI WAONGO MNO
 
Hayo ulioandika ni ukarabati wa uwanja wote utakapokamilika ulioambiwa ni awamu ya kwanza sasa hapo tatizo nini?
 
Uongo wa Serikali ni nini maana mimi no navyojua hivyo viti vya Tff na gharama wanazotoa CAF Pamoja na pesa watakazotoa Serikali jumla yake ndio hiyo bil30 mpaka hapo bado sijaona tatizo wala uongo wa Serikali
 
Hayo ulioandika ni ukarabati wa uwanja wote utakapokamilika ulioambiwa ni awamu ya kwanza sasa hapo tatizo nini?

Soma kwa makini utanielewa.

UKISHINDWA kuelewa nitakufafanulia kwa makini.

Kwa sasa Soma kwa Umakini.
 
Siku ya game ya simba na al ahly uongo wao utadhihirika.
Hapo bilioni 30 ndio zishaenda na maji

Wabongo sisi vyoo havichukui round, vitakiwa hovyo.
Huo mtandao(WiFi) sina imani nao, na sijui kwanini🤣
 
Back
Top Bottom