Ukarimu usikuue - jihadhari

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,392
"Mtanzania anaweza kutoka na biashara yake kuja kuuza Afrika Kusini, baada ya hapo anapanda ndege ya moja kwa moja kwenda China. Akiwa uwanja wa ndege anakutana na Mnigeria muuza madawa ya kulevya.

"Mtanzania anakuwa hana mizigo mingi, kwa hiyo yule Mnigeria anamwomba Mtanzania amsaidie kupitisha begi lake moja kwenye mzani, akidai kuwa yeye mizigo yake ni mingi, anaogopa atatozwa fedha nyingi.

"Kumbe lile begi linakuwa na unga. Sasa Mtanzania kwa kutojua, atakubali, baada ya hapo lile begi litaandikwa jina la Mtanzania. Mbele ya safari kama litavuka salama, Mnigeria atamshukuru Mtanzania na kuchukua begi lake lakini likikamatwa, Mnigeria atakimbia, Mtanzania atabaki na mashtaka ambayo mwisho wake ni kunyogwa China."

Tafakari chukuwa hatua,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…