JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ukatili kwa mwanamke mjamzito ni jambo la hatari kwani huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba, uchungu wa kabla ya muda na kujifungua #MtotoNjiti au mwenye uzito pungufu.
Katika maeneo ya kazi Mama wajawazito na wanaonyonyesha wanapaswa kulindwa dhidi ya ubaguzi/unyanyapaa na dhidi ya kuwa katika mazingira hatarishi kwa afya zao.
Pia wanapaswa kutengewa muda wa kunyonyesha au kunywesha #Watoto maziwa yao yaliyokamuliwa.
Wapewe stahiki zao za likizo ya uzazi, uhakika wa ajira zao, mafao ya matibabu na msaada wa kifedha inapobidi
Upvote
1