John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Jamii imetakiwa kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike ili kuleta usawa.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Mpanju amesema kuwa ni vyema jamii ikapambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.
Amesema jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.
Kwa upande mwingine Mpanju amesema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kwa kuwezesha wanawake kufikia kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.
Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia kumefanyika mapinduzi makubwa na hatua kubwa imepigwa katika kujenga kizazi cha haki na usawa huku wanawake wakichaguliwa na kuteuliwa kuongoza Idara nyeti katika taifa.
“Wanawake ni nguzo ya maendeleo duniani. Ndani ya mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia tumepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja, tuna Rais Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke, Katibu Mkuu wa Bunge mwanamke, tuna Mawaziri wanawake 9 katika Wizara nyeti wanafanya kazi vizuri na maendeleo tunayaona, mambo yanakwenda vizuri,” amesema Mpanju.