Nadil Kheri Ali
New Member
- Jul 29, 2021
- 1
- 2
Kwa mujibu wa shirika la watu duniani UNFPA, ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni moja ya majanga makubwa ya ukandamizaji wa haki za binaadamu duniani ikiwemo Tanzania. Inakadiriwa kuwa asilimia 40% ya wanawake wenye miaka 15 - 49 wamewahi kuwa wahanga wa ukatili ambapo asilimia 20% yao wakitendewa ukatili huo na mtu wao wakaribu. Ukandamizaji huu umeathiri makundi yote kwenye jamii, hata hivyo baadhi ya wahanga hususan wale wa kiume huwa na uwoga kuripoti matukio kama hayo yanapo wakumba. Hii husababishwa sana na itikadi na Imani kwenye jamii dhidi ya vitendo vya ukatili haswa dhidi ya wanaume.
Kwasababu hiyo pamoja na nyengine, matukio mengi ya ukatili ya kijinsia yanayo ripotiwa kwa sana ni yae dhidi ya watoto. Kwa mwaka 2021 peke matukio ya udhalilishaji 11,499 yali ripotiwa ambapo matukio 9,759 yalikuwa dhidi ya watoto wa kike na 1,740 dhidi ya wakiume. Hata kwenye matukio ya watoto wa kiume bado kuna ugumu katika uwasilishaji wa matukio sababu moja wapo ikiwa uwoga wa kulalamika kwenye ngazi husika. Matukio ya udhalilishadi dhidi ya watoto kikawaida huwa yanapewa uzito na kukemewa zaidi juu ya uhalisia kuwa wa hanga wao bado ni wadogo kiakili na kiumri na wanauhitaji na uangalizi wa wakubwa wao. Hata hivyo, matukio kama haya ni kwa mara chache sana kuripotiwa na watoto wenyewe. Badala yake huripotiwa nawazazi na welezi wa watoto. Na hii muda mwingi ni hutokea baada ya kuona mabadiliko ya tabia na afya za mtoto. Hii husababishwa si tu na wahanga hasa watoto wa kiume kuwa na aibu na woga bali pia sababu kuu ni juu ya uhalisia kwamba muda mwingi waliotenda huo ukatili huwa ni mtu wao wa karibu.
Ni kwasababu kama hizo na nyengine nyingi msisitizo mkubwa umewekwa katika kukomeza ukatili dhidi ya watoto na kwa ukubwa umewaacha wahanga wengini wa ukatili. Wahanga kama wa ukatili unao tendwa na mtu mzima dhidi ya mzima mwengine, au dhidi ya wazee. Ukatili kwa kijana dhidi ya kijana mwenzake wa jinsia zote, kike au kiume. Ule anao tendwa na mtu wa jinsia ya kike dhidi ya kiume, na hata kwa watoto. Pia kuna ukatili wa kimtandao na kwenye ndoa.
Kutotambuliwa ama kupewa uzito aina zengine za ukatili hutokana kwa kiasi kikubwa na jinsi jamii inavyo tafsiri neno "ukatili wa kijinsia" ama "ukatili wa kingono". Kwa mfano, kuna fikra kwamba ukatili huo hauwezi kusema umetendeka kama mtendaji ni mwanamke na muathirika ni mwanaume. Ama kama ukatili umetokea ndani ya ndoa. Ukuaji wa teknolojia pia umeleta aina mpya ya ukatili ambapo mtu anaweza kujikuta picha zake za siri zikitembweza mtandaoni, kutokemea au kupinga vikali tabia kama hizi huleta taswira kuwa hichi kitendo ni cha kukubalika, wakati kiuhalisia ni ukatili.
Kwa kipekee, moja ya imani iliyokubalika kwa kiasi kikubwa zaidi ni kwamba ukatili wa kijinsia haswa ubakaji hauwezi kusema umetendeka kama wawili hao wapo kwenye ndoa. Wahanga wa ukatili wa aina hii hujikuta kwenye wakati mgumu na kugubwika na aibu wanapo ambiwa na wao kuamini kwamba tendo hilo ni "haki za mume" na hivyo basi wanapaswa kutumiza hitaji hilo kwa wanaume zao. Imani na itikadi hii huchochea muendelezo wa ukatili huu, sababu moja wapo zikiwa wahanga wengi kuhisi hawatapata msaada. Lakini ni muhimu pia tukatambua kuwa hadi mwaka 2021, ambapo Mahakama ya rufaa ilipokubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu kwenye kesi namba 204 ya 2017 The AG v Rebecca ambayo ilifuta ibara 13 ya Sheria ya ndoa kuwa inakiuka Katiba kwa kuruhusu Binti wa 15 kuolewa, zaidi ya asilimia 30% ya wanawake walikuwa wanaolewa kabla ya kutumiza miaka 18.
Ndoa kama hizi ilimanisha kuwa mabinti wadogo walikuwa wanaingia kwenye ndoa. Mara nyingi zaidi ndoa hizi hutokea bila mapendekezo ya mtoto mwenyewe, bali husababishwa na mila za jamii anayoishi. Inapotokea binti anaishi kwenye jamii ambayo ndoa za utotoni huwa na ukawaida kutokea, inakuwa ni ngumu kwake kupinga kwani huwa kuna mifano mingi ya ndoa kama hizo. Ila kwa uhalisia ni kwamba muda mwingi mabinti hawa huwa "watumwa wakingono" na hii umegundulika kwenye tafiti nyingi zilofanywa juu ya athari za ndoa za utotoni. Kibaya zaidi ni kwamba binti anapoolewa hupoteza Kinga yake kama mtoto na hivyo huwa ana njia chache zakujikwamua.
Baadhi ya sababu nyengine za ndoa za utotoni ni umaskini ila pia kutokuwa na elimu juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike. Tukiangalia umaskini, kama familia inahangaika kupata mlo wa siku, baadhi ya familia huchukua hatua ya kufungisha watoto wa kike ndoa si kama njia ya kupata kipato bali kama njia ya kupunguza mzigo kwa familia. Ndoa kwao huwa ni ufumbuzi peke. Pia wengi wao hawana uelewa juu ya madhara ya ndoa za utotoni na ukatili wanaweza kupata na pia kusahau umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike.
Imani za dini, mila na desturi kwa kipekee ina nafasi yake katika kuendeleza itikadi ya ndoa za utotoni bali pia na mtazamo wa ukatili wa kijinsia ndani ya ndoa
Hata hivyo mafunzo hayo yana ushawishi mkubwa katika kutokomeza aina nyengine za ukatili wa kijinsia, hasa zile ambazo zipe nje ya ndoa. Kipengele kikubwa ya njia hizi ni kwamba mafunzo hayo hulenga katika kukataza ufanyaji wa matendo yenyewe zaidi "Abstainance". Falsa hii kwa bahati mbaya huwaacha wahanga kwenye wakati mgumu kwasababu wao huwa hawakuridhia tendo hili lifanyike kwao. Hivyo basi kuna umuhimu wa kuongezea elimu ziada ambayo itakuwa na manufaa kwa wahanga pia, kama vile hatua za kuchukua ili kuzuia maambukizi ya VVU na mimba zisizo za lazima pia na misaada mbali mbali ya kisheria ambayo mtu anaweza kuipata. Ni maoni yangu kuwa hiyo ni moja ya njia bora ya ufumbuzi.
Ni kwa bahati mbaya ipo imani kwamba kuwapa elimu haswa watoto na vijana juu ya njia bora za kujikinga watakuwa na ushawishi mkubwa wa kutenda vitendo hivyo. Lakini tufikirie kidogo, kwa mfano usafiri haswa wa majini na angani wangekuwa na fikra kama hiyo juu ya usalama wa vyombo vyao. Kwa kuamini kwamba vyombo vya ni salama na hawataki kuwasitua wateja wao, na hata kama ajali kwa bahati mbaya ikitokea wanajua kuwaokoa wateja wao! Lakini vyombo hivi hutoa elimu na kusisitiza hata kama wewe ni msafiri wa kawaida pia kuna haja ya kusikiliza tena kwa usalama wako. Elimu hii hutolewa kwasababu husaidia kutoa hofu kwao pindi janga linapotokea, kwani watakuwa wanajua wateja wao wana elimu hata kama ndogo ya nini cha kufanya. Kutoa ama kutotoa elimu hii hauzidishi wala kupunguza uwezekano wao ajili kutokea bali husaidia kuongeza idadi ya watakao okolewa.
Ni dhahiri kwa kiasi kwamba elimu ya njia bora ya kinga haiwezi kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia, hata hivyo itasaidia sana katika kupunguza madhara yatokanayo na vitendo hivyo kama maambukizi ya VVU na mimba zisizo mpango. Kwa mfano ukiondoa elimu zinazojulikana na kuongelewa sana, watu wengi bado hawajui kuwa endapo binti kabakwa bila kinga yoyote anaweza kupewa matibabu ambayo yatamsaidia kutopata mimba endapo ataitumia ndani ya masaa 72 hadi 120 kutoka mdaa wa hilo tendo lililofanyika. Pia anaweza kujikinga na kupata VVU endapo atapata matibabu ndani ya masaa 72. Utoaji wa elimu hii haswa kwa makundi hatarishi, kwa kuanzia na wanafunzi angalau Form One kwani hawa huwa hawapo tu kwenye miaka hatarishi bali pia wamekuwa kiakili na mwili pia.
Kwa umuhimu pia ni kutoa elimu kwa watoto wote juu ya njia bora ya kuongelea matukio haya. Endapo watoto na jamii kwa ujumla wakijua namna bora ya kuongelea na kuripoti vitendo hivi itasaidia katika kukomeza tabia hii. Katika utafiti uliofanywa na Dr. David Lisak (M.D) na Paul Miller (2002) ilibaini kuwa asilimia 60% ya wale wanaotenda ukatili wa kijinsia hurudia tena kutenda dhambi hiyo. Ukitazama matokeo ya utafiti huu, ni vyema pia ukumbuke kuwa wapo wahanga wengi ambao hawajawahi kuripoti matukio yaliyo wasibu na hivyo kukaa nayo hadi ukubwani.
Kujua namna bora ya kuongea na kuripoti hivyo basi itasaidia kwa kiasi, haswa kwenye kupunguza watendaji wa matukio haya mtaani.
Tunapaswa pia kujikita kwenye kinga zaidi kuliko adhabu kali za kisheria, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawapa umuhimu wahanga na kuwapa msaada na sio kuadhibu tu wakosaji. Ni maoni yangu, mwenendo hu wasasa iliyojikita sana katika utoaji adhabu kali zaidi hauleti mafanikio yoyote bali kuongeza tu idadi ya wafungwa wa makosa haya. Kwani kama tukisoma kwa wenzetu waliotumia njia za adhabu "criminalization" zaidi tutagundua athari kubwa zinazotokea kwenye jamii, wakati huohuo bila hata kutokomeza au kupunguza vitendo husika adhabu hizo ziliwekwa kutokomeza. Tukiangalia mfano mzuri wa vita dhidi ya dawa za kulevya Marekani ambavyo kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka kumi hakija fanikiwa tu kupunguza idadi za utumiaji wa dawa hizo na badala yake imeengeza idadi ya wafungwa kwa zaidi ya watu milioni moja. Hivyo basi ni ushauri wangu nguvu zaidi ziwekwe pia katika kutibu na kuwasaidia wahanga kwani wao wanahitaji muangalizo zaidi. Kwani kwa kuwafunga wakosaji hauleti unafuu kwa wahanga, na wala haisaidii kupunguza maumivu ya athari zilizowapata.
Na hii itafanikiwa kwa kutoa "counselling services" na pia kwa kuweka miundombinu bora ya afya ya uzazi.
Pia naona kuna umuhimu mkubwa wa kwenda zaidi ya maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Rebecca na kuweka miaka ya kufunga ndoa kuwa 21 na sio 18 kama kwenye maamuzi ya kesi hiyo. Hii ni kwasababu kwa asilimia kubwa na kawaida haswa kwa mabinti wanakuwa wamemaliza Elimu ya Sekondari na wanauwezo wakujichagulia kama kuenda na elimu ya juu kuwafunga Muhimu kutambua kuwa kutakuwa na pingamizi labda kwasababu ya imani zao lakini lazima tutambue kuwa kuna watu hata miaka 18 walipanga wakitumia kipengele hiko hiko.
Kwa kuhitimisha, lazima pia kama jamii tujiulize faida ya kuwafunga Baba watarajiwa. Ni imani yangu kuwa ndoa nyingi za utotoni zipo kwasababu baadhi ya wazazi huwa hawako tayari kulea wajukuu wakati baba mtu yupo jela na hivyo kulazimisha "ndoa za mkeka" Ni maoni yangu pia kwamba tukianza kuzungumzia njia bora za kusaidia na kuwaongoza wahanga wa majanga ya ukatili na kutoa elimu juu ya athari za ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni na sio kuanzisha adhabu mpya na kali tutakuwa tunachukua hatua bora na zenye tija katika kukomeza ukatili wa kijinsia.

Upvote
3