Pre GE2025 Ukatili wa Kijinsia wakati wa uchaguzi unachangia kuzima ndoto za Wanawake kuwa viongozi Zanzibar

Pre GE2025 Ukatili wa Kijinsia wakati wa uchaguzi unachangia kuzima ndoto za Wanawake kuwa viongozi Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
"Niliishiwa na nguvu, baada ya kutolewa katika chumba cha kupigia kura, wakati Mimi nilikuwa ni mgombea halali wa uwakikishi Jimbo la Malindi Mwaka 2020," anasema Khadija.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, alitolewa katika chumba cha kupigia kura, na kuvumilia ukatili wa Kijinsia, wa kimwili na vitisho kutoka Vyombo vya Dola.

Hii, ni baada ya kutakiwa kutoka katika Kituo cha Kupigia Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Khadija Seif (ambaye si jina lake halisi) anasema aligombania uwakilishi kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Malindi, lenye wadi mbili na Shehia 11, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Khadija , ambaye alianza harakati za Siasa tangu Miaka ya 1993, anasema vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wagombea wa upizani. wakati wa uchaguzi vinawavunya moyo, Wanawake kurudi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi za uongozi.

Kupata Taarifa na Matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 pamoja na Zanzibar

"Kila nikikumbuka Jinsia nilivyotolewa katika chumba cha kupigia kura na kunyimwa haki yangu ya kuangalia hesabu za kura zangu na mwenzangu wa chama X akaachwa ashuhudie kura zikihesabiwa, nilipata maradhi," anasema Khadija.

Anasema kama hali haitabadilika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, basi Wanawake wengi wa Vyama vya upizani, hawatagombea na ile 50/50 itakuwa ni ndoto kufikiwa.

"Tunataka Siasa safi, ambazo zitakuwa hazina vurugu, wala vitisho ili tuengeze wingi wetu katika kugombea nafasi za Majimbo," amemaliza Khadija .

Ukatili wa kijinsia wakati wa uchaguzi ni suala linalowatafuna Wanawake wengi wa Vyama vya SIASA kama ulivyokuwa kwa Fatma Saidi (sio jina lake halisi pia) ambaye alikatisha ndoto zake za hafla za kuwa Kiongozi Mwaka 2020.

Fatma, (43) ambaye aligombania nafasi ya Ubunge kutoka Chama cha CHADEMA katika Jimbo la Kikwajuni lenye wadi mbili na Shehia 11, Mkoa wa Mjini Unguja.

Ni miongoni mwa Wanawake waliokatisha ndoto zake za kuwa kiongozi kwa sababu ya ukatili alioumpata, wakati wa Uchaguzi wa Mwaka 2020, wakati anagombea.

Anasema aliambiwa na Vyombo vya Dola atokee nje ya Kituo cha Kupigia Kura, baada ya kushuhudia Mwanachama wa chama X, anapewa karatasi za kura zaidi ya moja.

"Ndipo nilipotolewa nje ya Kituo cha kupigia kura, eti sijulikani kama mimi ni Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Kikwajuni," anasema Fatma.

Anasema kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, kumekuwa na mwamko mdogo wa ushiriki wa Wanawake kutoka vyama vya upinzani, kutokana na ukatili unaowakuta.

Fatma, ambaye aligombea Ubunge Jimbo la Kikwajuni, lenye Wakaazi 22,673, anasema kuwa Wagombea wa Upizani wanapitia ukatili na udhalilishaji kutoka Kwa Vyombo vya Dola ambao wao hawahusiki na uchaguzi.

"Jukumu la kulinda uchaguzi ni la Jeshi la Polisi na si la Vyombo vya Dola, kwani wao ndio wanaovuruga uchaguzi," anasema.

Zanzibar imesaini mikataba kadhaa ya kumlinda Mwanamke dhidi ya aina zote za ukatili na udhalilishaji kama mkataba wa cedaw.

Mkataba wa cedaw umeanzishwa Mwaka 1979, lengo la mkataba huo ni kumlinda mwanamke na ukatili na Udhalilishaji lakini utekelezaji wa mkataba huo bado unasua sua.

Chama Cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA ZNZ) ni Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishuhulisha na utetezi wa haki za Mtoto wa kike,na kuhamasisha Wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi, Mkurugenzi Mtendaji, Dkt Mzuri Issa amesema Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inapaswa iwe na vikosi maalumu vinavyolinda uchaguzi na viwe chini ya tume hiyo, ili kuepusha vurugu wakati wa uchaguzi.

"Tumekuwa tukishuhudia vurugu na ukatili dhidi ya wanawake wakati wa uchaguzi na kupelekea ushiriki mdogo wa wanawake katika Majimbo," amesema Dr Mzuri.

Anasema kuwa ili kuengeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi katika vyama vyote vya Siasa, ni lazima tuwe na Siasa safi ambazo hazina vurugu.

Utafiti uliyofanya na Taasisi ya Kitaifa ya Kidemokrasia (NDI) ikishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ), imesema Zanzibar imekumbwa na vurugu zinazohusishwa na uchaguzi, hasa Uchaguzi wa Mwaka 2020.

Kwa mujibu wa ripoti, iliyoandaliwa na ACT Wazalendo, kuhusu matukio ya vurugu zinazohusishwa na uchaguzi wa Mwaka 2020, jumla ya matukio 343 ya Udhalilishaji yanayohusishwa wanaume 256 na wanawake 87 yalitokea wakati wa Uchaguzi, watu 14 walikufa na 55 walijeruhiwa kati ya Oktoba 26 hadi 30 mwaka 2020.

KWANINI WANAWAKE HAWAONEKANI KATIKA NAFASI ZA UONGOZI?
Kwa mujibu wa ripoti ya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, inaonesha kuwa Zanzibar ina Wakaazi 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915,492 na wanawake ni 974,281.

Hii ina maana kwamba, wanawake ni Asilimia 51.6 ya Wakaazi wote wa Zanzibar lakini wingi huo hauonekani katika nafasi za uongozi kutokana na mambo mengi lakini pia, ukatili unaowakuta wanawake kipindi cha uchaguzi.

Anna Athanas Paul ni Naibu Waziri wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, anasema Tathimini iliyofanywa na wizara hiyo, inaonesha wanawake bado wako kidogo katika nafasi za uongozi, ukilinganisha na wanaume jambo ambalo linahitaji kuangalia.

"Takwimu zilizokusanywa na Wizara kutoka katika Taasisi mbalimbali kwa mwezi wa Machi Mwaka 2024, ni Asilimia 30 tu ya Wanawake ambao wako katika uongozi, ukilinganisha na wanaume ambao wako asilimia 70," anasema Naibu Waziri Anna.

Anna, ameongeza Serikali inaendelea na jitihada katika kufikia malengo yaliyowekwa, kupitia Dira ya 2050 na mpango wa maendeleo (ZADEP) 2021/2026 ambapo lengo katika nafasi za uongozi ni kufikia 50/50.

Ziko mamlaka ambazo, zinahusika na maswala ya usalama wa raia, Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Unguja, SP Daniel Shila,anasema jeshi la polisi limejipanga na litaendelea kulinda raia na Mali zao kama inavyowataka ,Sheria ya jeshi Hilo ,sura ya 322.

Anasema kuwa katika kuhakikisha wanawake wanagombea nafasi za uongozi, watasimamia Sheria za nchi kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya Sheria.

"Tutamchukulia hatua yoyote atakae husika na vurugu wakati wa uchaguzi, ikiwemo wataka toa maneno machafu Kwa wagombea wanawake," anasema S P Daniel.

Thabiti Idarus Faina, ni mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) anasema kuwa tume haina takwimu za makosa ya ukatili na Udhalilishaji unaotokea wakati wa uchaguzi,kwani takwimu hizo zinaripotiwa Kituo cha Polisi.

"Tume haina ripoti ya matukio ya Udhalilishaji, kwani matukio hayo yanaripotia moja Kwa moja kituo Cha polisi," anasema Faina.

ANDIKO LA MARYAM NASSOR
 
Back
Top Bottom