Ukatili waliofanyiwa watumwa kutoka Afrika huko Amerika

Ukatili waliofanyiwa watumwa kutoka Afrika huko Amerika

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
PICHA za kusikitisha zilizopigwa miaka zaidi ya 150 iliyopita zinaonyesha ukatili wa kutisha waliokuwa wanafanyiwa watumwa kutoka Afrika waliosombwa kupelekwa barani Amerika kwenda kufanyishwa kazi ngumu.
Huko walichapwa mijeledi, wakafanyishwa kazi nzito kama wanyama kwenye mashamba ya pamba na miradi ingine migumu wakitishwa kwamba polisi wangewasaka popote na kuwakamata iwapo wangethubutu kutoroka.

Picha hizo zimeibuliwa katika kumbukumbu ya kutimia mwaka wa 153 tangu kupigwa marufuku kwa utumwa nchini Marekani, Januari 1, 1865 kufuatia Badiliko la 13 la Katiba ya nchi hiyo ambalo lilisainiwa na Rais Abraham Lincoln, Februari 1, 1865.

Miongoni mwa picha hizo ni pamoja na zilizopigwa mnamo miaka ya 1700 zikionyesha maisha ya watumwa nchini Marekani ambapo kuna moja inayoonyesha mgongo wa mtumwa ulivyochanwa kwa mijeledi na picha nyingine nyingi zikionyesha wakifanya kazi za kitumwa kwenye mashamba ya pamba.
slave1.jpg

Mgongo wa mtumwa kutoka Afrika uliojaa makovu ya kuchanwa kutokana na kuchapwa mijeledi wakati wa kufanyishwa kazi za kitumwa.
slave2.jpg

Watumwa na watoto wao wakifanyishwa kati katika shamba la pamba.
slave3.jpg

…Wakivuna pamba.
slave4.jpg

…Wakiwa wamepangwa kwa ajili ya kununuliwa mnadani.
slaves5.jpg

Kazi ya kuvuna pamba ikiendelea katika mojawapo ya mashamba.
slaves6.jpg

Hapa ni kwenye mnada wa watumwa.
slaves7.jpg

Mzungu Joseph Carpenter aliyepiga vita utumwa, akiwa na mtoto wa familia ya watumwa.
slaves8.jpg

Mtumwa Samuel Harper na mkewe wakiwa Ontario, Canada, baada ya kutoroka kutoka Marekani.
slaves9.jpg

Moja ya wakazi waliyokuwa wanalundikwa watumwa.
 
Back
Top Bottom