UKAWA, CHADEMA, CUF na jiwe la pembeni

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Kama wako ni Makata, wangu mie Subiani,
Kama Nungwi amepita, tukutane kilingeni,
Umeianzisha vita, nduguyo kumfitini,
Nasema waja kujuta, mpewa hawezekani.
Kama mi' niliokota, nawe uende jaani.

Sasa umekuwa paka, wataka ongeza kimo,
Kwa nguvu wabinuka, ili uongeze kimo,
Maungo yaja kuchoka, huwezi refusha kimo,
Majaliwa ya Rabuka, kuumbwa na mbili kimo,
Hadharani nayaweka, sitasema mumo kwa mumo.

Limetupwa na wajenzi, limekuwa kuu pembeni,
Sa mmejifunga tanzi, hamshindi ka' zamani,
Ndio zao la ushenzi, mliopanda kondeni,
UKAWA rudisha enzi, kazi ya chini kwa chini,
Mwaja ambulia konzi, hamrudi ka zamani.

Hukuweza mikundeni, uweze michorokoni?
Kwa mlango wa uwani, jiwe lirudi kundini,
Wa mbele uko na nini, au ndio mwaona soni,
Mlilitupia nini? jiwe hili la thamani,
Ndio mkisema cha nini, wale watakipata lini.

Ya Chalinze na Kalenga, pesa tatu kata tatu,
Mbona mna kasosenga, mliupiga upatu,
Jiwe si mlilitenga? Aso fedha wake watu,
Makundi mloyafunga, si watu hao viatu,
Hawana kitu kupinga, mbwa mfuata chatu.

Hivi mtu kama Tundu, anaweza kuwa mtu?
Ameufanya utundu, sheria kuwa kiatu,
Amekuwa mburumundu, utu wa mtu ni utu,
Ameusuka ukindu, chama chaliwa na chatu,
Mmebaki na matandu, wali umeliwa na watu.

Tutaimarika sana, tukilitupa jiwe hili,
Wameimarika sana, kwa zile kura mbili,
Sasa wanasonona, hawana lile wala hili,
Fukuza ni nzuri sana, pale penye mushkeli,
Mambo ya kuoneana, nani mwenye kukubali?

Wa kisamvu wala nyama, wa maziwa wanywa tui,
Simba amekuwa ndama, paka amekuwa chui,
Jahazi ndio lazama, wasafiri hawatambui,
Kwa UKAWA wafichama, ka' mbuni hamjijui,
Wali wataka heshima, vema wapunguze tui.

Tatizo hasa ni kiti, wajuzi tumebaini,
Ati wa kukonda kiti, afaidi mwana jini,
Tulime sote tikiti, avune mkaskazini,
Kuna saa na wakati, viatu mwaja baini,
Mkubwa wenu afriti, hatakiwi kanisani.

Tamati nimeshagonga, mengi leo mwajifunza,
Msiikimbie nyanga, kazi ndio imeanza,
Ndio kazi ya kiganga, nyayoni habaki funza,
Walio una pakanga, n'nani atakutunza,
Pia huko kujigonga, kwa CUF kutawaponza.

Njano5.

0784845394.
 
Mashairi na vina ni sawia haswa....Sema maudhui yake ni hafifu kwa kuwa yaelekea kuaminisha watu kuwa huyo MTU mwenye thamani bila yeye kundi fulani haliwezi kufanikiwa. Kumbuka hata ronaldo hawezi cheza pekee na kundi lingine la timu...atafungwa...thamani ya mtu huonekana kundini....upekee peke yake hufifisha thamani hiyo aliyonayo.....Umoja (Ukawa) ni nguvu na utenganao au umimi(p..a..c) ni udhaifu
 

nimepokea,,, ni mazao yko,,, sina budi kuyaheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…