Tetesi: Ukawa kazi ipo

baba prosper

Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
9
Reaction score
7
::KWANINI UKAWA ITASHINDA KESI YA UMEYA KINONDONI!::

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]: Akidi ya kikao haikutimia. Sheria inataka 2/3 ya wajumbe wote kuhudhuria na kusaini mahudhurio ndipo mkutano upate uhalali wa kufanyika. Wajumbe HALALI wa mkutano huo ni 34, kwa hiyo 2/3 ni wajumbe 23. CCM ilikua na wajumbe 18 (kati yao walikuwepo wasio halali). Hata hivyo iadi ya wajumbe 18 wa CCM haikutimiza akidi, kwa sababu wajumbe wa UKAWA hawakusaini mahudhurio. Kwahiyo mkutano wa jana ni batili. Mahakamani CCM hawawezi kujitetea ktk hili. #Moja_bila.!

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]: Kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo ya serikali za mitaa, taatifa ya mkutano mkuu wa uchaguzi inapaswa kutolewa angalau masaa 72 kabla ya uchaguzi (i.e siku 3 kabla). Lakini barua za mkutano wa uchaguzi zilitumwa tar.22 zikielekeza kuwa mkutano mkuu ni tar.23. Notification ilikua chini ya masaa 24 kinyume na sheria inavyotaka. Mahakamani DED hawezi kujitetea kwenye hili. #Mbili_bila.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: Sheria ya marekebisho ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 2006 (Local Government Laws - Miscellaneous Amendments), Sheria No.13 ya mwaka 2016 kifungu cha 17 (d) inasema, Mbunge yeyote atakayeteuliwa na Rais atakuwa mjumbe katika Halmashauri anayoishi (Any member of Parliament appointed by President shall be a member to a Council in which that member ordinarily resides).

Lakini Dr.Tulia Akson amepiga kura Halmashauri ya Kinondoni wakati yeye ni mkazi wa Kibamba na Halmashauri yake ni Ubungo. Kwahiyo Tulia si mjumbe halali wa Kinondoni kwa mujibu wa sheria. Mahakamani Tulia hawezi kujitetea ktk hili. #Tatu_bila.!

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]: Sheria ya marekebisho ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 2006 (Local Government Laws - Miscellaneous Amendments), Sheria No.13 ya mwaka 2016 kifungu cha 17 (e) inasema wabunge ambao ni wateule wa Rais wakizidi watatu kwenye Halmashauri moja, wale waliozidi wanaweza kuhamishiwa Halmashauri za jirani provided Waziri ataujulisha umma kupitia gazeti

(Provided that where members of the Parliament appointed by the President are more than three, the Minister shall by order published in the Gazette direct that the rest of the Members of Parliament in excess of the three to become members of the neighbouring council as if they were ordinarily resident in those councils).

Kwa mujibu wa kifungu hiki cha sheria, hapa kuna mambo mawili. Jambo la kwanza ni kwamba wabunge wa kuteuliwa na Rais wawe zaidi ya watatu kwenye Halmashauri moja, pili Waziri atoe tangazo kwenye gazeti la serikali kuwahamisha waliozidi.

Sasa Ndalichako na Mahiga kuhamishiwa Kinondoni kutokea Ilala, je Ilala walizidi watatu? Jibu ni Hapana, hawakuzidi watatu. Sheria inasema wakishazidi watatu ndio wahamishiwe kwenye halmashauri ya jirani. Lakini Wabunge wa kuteuliwa na Rais kwa Ilala walikua wawili tu (Ndalichako, na Mahiga). Kwa hiyo uhamisho wao kwenda Kinondoni ni BATILI kwa mujibu wa kifungu hicho cha sheria. Si Mahiga wala Ndalichako anayeweza kujitetea mbele ya mahakama. #Nne_bila.!

Pia sheria inasema kabla hawajahamishwa Waziri husika lazima atoe taarifa gazetini kuelezea sababu za uhamisho wao. Waziri wa TAMISEMI Ndg.George Simbachawene hajawahi kutoa tangazo lolote gazetini kuhusu kuwahamisha Ndakichako na Mahiga kutoka Ilala kwenda Kinondoni. #Tano_bila.!

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]: Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa pamoja vinataja suala la serikali za mitaa kuwa SIO SUALA LA MUUNGANO. Kwahiyo Mbunge wa Z'bar haruhusiwi kuwa mjumbe kwenye halmashauri za Tanzania Bara, na Mbunge wa bara haruhusiwi kuwa mjumbe wa halmashauri yoyote upande wa Zanzibar. Kwahiyo kitendo cha Prof.Mbarawa kupiga kura Kinondoni sio tu ni kinyume cha sheria bali pia ni kinyume cha Katiba ya nchi ambayo ni sheria mama.

Kwahiyo haihitaji degree kujua kwamba uwakilishi wa Profesa Mbarawa ni batili na hata Kura yake ni batili pia. Prof.Mbarawa hawezi kujitetea mbele ya Mahakama kuhusu. #Sita_bila.!

Kwa kifupi ni kwamba Wabunge wote walioteuliwa na Rais walioshiriki kupiga kura Kinondoni jana ni wajumbe batili. Wawili (Ndalichako na Mahiga) ni wa Ilala, Tulia ni wa Ubungo na Mbarawa ni wa Zanzibar. Wote wanne hawana uhalali wa kushiriki vikao vya Halmashauri ya Kinondoni.

Kwahiyo nategemea Mahakama itangaze uchaguzi wa jana kuwa batili, na kuitisha upya uchaguzi halali, (in absence ya wajumbe wanne feki ambao ni wateule wa Rais). Kwahiyo kati ya wajumbe 18 wa CCM toa wanne (feki), wanabaki 14.

Mahakama pia nategemea itawaruhusu wajumbe halali wa Halmashauri ya Kinondoni walioondolewa bila sababu zozote za msingi waweze kushiriki vikao vya Halmashauri hiyo. Wajumbe hao ni wabunge wawili wa UKAWA (viti maalum) na madiwani wawili (viti maalumu).

Kwahiyo ktk uchaguzi wa marudio, utakaofanyika baada ya Mahakama kutoa hukumu, nategemea UKAWA itakua na wajumbe 20, na CCM wajumbe 14. Jumla 34. Hawa ndio wajumbe halali wa mkutano mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

The good thing about Law ni kuwa "Sheria haipendagi ujinga". Lissu alisema tutawashinda Mahakamani na tutawasinda nje ya Mahakama", kwa ujinga wao wa kupenda namba wakati hawajui hesabu. #Sita_bila, kama mmesimama vile.!
 
tunaitajika kuiombea sana Mahakama
 
Yani Lisu umekuja na ID mpya siku hizi unaitwa baba prosper?

Mwenyekiti CCM JF
 
Umeshamaliza......... The only trusted organ in this country nowadays ni Court, Justice is always delayed and not denied
 

Haya weee hivi ule uchaguzi wa meya wa Dar es sallam ambao UKAWA peke yenu mlipiga kura kumpata meya na akapatikana kwa kura zenu tu baada ya CCM KUSUSA Uchaguzi na nyie mkaendelea tu ilikuwaje vile????!!! TANGULIENI MAHAKAMANI tutakutana huko huko
 
Amaa kweli sheria inakanyagwa na watunga sheri mnategemea nn,kina Tulia siniwabunge na naibu speaker? Sasa sheri hajui acha wafanyiwe kazi na mhimili unaojali sheria.
 
Duuh
Duuh, mimi sio mtaalamu, lakini kama yaliyoandikwa yatatimia na kutoa matokeo chanya basi tunayo safari ndefu kama Taifa. Inakuwaje figisufigisu nyingi katika chaguzi kama hizi? Tuliingia katika mfumo wa vyama vingi kwa kulazimishwa? Kama vipi si ipitishwe tena kura ya maoni tujue moja?
 
Yani Lisu umekuja na ID mpya siku hizi unaitwa baba prosper?

Mwenyekiti CCM JF

Kesi gani ya uchaguzi aliyowahi shinda Lissu?? Lisu anajua kujitetea mwenyewe tu kikimbana cha kumbana kesi za wengine huwa hawezi
 
Haya weee hivi ule uchaguzi wa meya ambao UKAWA peke yenu mlipiga kura kumpata meya na akapatikana kwa kura zenu tu baada ya CCM KUSUSA Uchaguzi na nyie mkaendelea tu ilikuwaje vile????!!! TANGULIENI MAHAKAMANI tutakutana huko huko
Mbona unauliza maswali ya jikoni upo sawa kweli au mlango ulisha funguliwa
 
Yani Lisu umekuja na ID mpya siku hizi unaitwa baba prosper?

Mwenyekiti CCM JF
Sheria sio vijembe na mipasho unasikia wewe mwenyekiti killazza wa ccm JF!
Mlipata aibu Jiji, lakini badala ya kujifunza akili zenu zinebaki vilevile sasa mnaaibika tena. Mbona wenzenu hawaletei figisu Temeke na Kigamboni?
Jifunzeni kuwa wastaarabu, chama chenu kikongwe lakini uhuni kama panya road!
 
Ndugu chama chetu sio panya road tutake radhi, si mshasema mnaenda mahakamani nendeni nasikia mshamtanguliza Kibatala, ila nyie dawa yenu iko jikoni.

Mwenyekiti CCM JF
 
Kweli kazi tunayo,hapo ni kugombea umeya wa manispaa tu,je kura za nchi nzima nani atakuwa mwaminifu?
 
Hawa jamaa wabakaji wa kila kitu wanaweza wakaendesha hiyo kesi hadi 2020, mihimili yote yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…