Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

GEBA2013

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2014
Posts
4,880
Reaction score
6,047
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi, UKAWA wana mpango wa kuweka Mgombea Urais 2015

- Aidha, wana mpango wa kusimamisha mgombea ubunge mmoja katika majimbo

- Mbowe, Mbatia na Lipumba wazungumza na kudai ni mapema mno kutoa maelezo juu ya umoja wao!

- Vyama vimeshapeleka mapendekezo kwenye sekretarieti za vyama husika kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi wa kufanikisha hili

- Mbowe adai kuunganisha nguvu ya vyama vya upinzani ni suala ambalo halikwepeki kwakuwa Siasa za sasa ni dynamic (zinabadilika) na fikra za jana ni tofauti na za leo.

- Lipumba adai Katiba imewaunganisha wapinzani na kuongeza kuwa huu ni mwanzo mzuri unaoweza kutoa mwanga wa nini kitatokea mbeleni.

- Mbatia asisitiza kuwa suala la wapinzani kuungana si la kujadili maana ndiyo mahitaji ya wananchi kwa sasa!

Tunataka tuwapime kwanza kwenye hili la katiba kama mtaweza,,,uchaguzi bado sana shughulikrni na katiba kwanza tuone kazi yenu, either isipatikane au ipatikane ya wananchi na c ya ccm
 
pia kwenye ubunge vyama vyote kusimamisha mgombea mmoja sehemu ambapo chama kinakubalika mfano kigoma nccr.mwanza chadema na lindi mtwara na lengo ni kuitoa ccm marakani. my take.ccm mwisho wao hatimaye umefika source.mwananchi
 
Tunataka tuwapime kwanza kwenye hili la katiba kama mtaweza,,,uchaguzi bado sana shughulikrni na katiba kwanza tuone kazi yenu, either isipatikane au ipatikane ya wananchi na c ya ccm

Uwapime nini tena? every step ahead in liberation is already a movement! Au unaogopa sana wakiunganisha nguvu hawa jamaa? Habari ya mujini ndo hiyo sasa kaa sawa kufungasha virago 2015!!
 
pia kwenye ubunge vyama vyote kusimamisha mgombea mmoja sehemu ambapo chama kinakubalika mfano kigoma nccr.mwanza chadema na lindi mtwara na lengo ni kuitoa ccm marakani. my take.ccm mwisho wao hatimaye umefika source.mwananchi
Tunaelekea mahala pazuri sasa
 
pia kwenye ubunge vyama vyote kusimamisha mgombea mmoja sehemu ambapo chama kinakubalika mfano kigoma nccr.mwanza chadema na lindi mtwara na lengo ni kuitoa ccm marakani. my take.ccm mwisho wao hatimaye umefika source.mwananchi

imekaa safi sana hiyo.
 
ukawa umeamua kusimamisha mgombea mmoja wa urais na ubunge uchaguzi ujao.ni gazeti la mwananchi la leo

Sasa hadi wakati huo wa uchaguzi bado watakuwa UKAWA au watatafuta jina lingine, maana ukawa limekuja kwa ajili ya kazi ya katiba. Hata hivyo, ni wazo zuri kama watapata wabunge wengi katika Bunge la JMT ili kuibana Seraikali katika utendaji kuliko ilivyo sasa ambapo Bunge liko dominated na chama kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…